Msaada: Natafuta digital camera na printer nzuri kwa ajili ya biashara ya passport size photos

Msaada: Natafuta digital camera na printer nzuri kwa ajili ya biashara ya passport size photos

Bajeti muhimu, kama una simu inayopiga vizuri unaweza uka anza nayo, watu wengi tu wanatumia simu biashara hio. Pia kumbuka simu inapiga picha nzuri kuliko point and shoot camera, ni either unatumia simu ama kama unanunua Camera hakikisha ni Dslr level, ukiweka tu hio keyword jiji ama fb marketplace zitakuja.

Kuhusu printer za passport sina uzoefu nazo, ila kama printer nyengine hakikisha running cost ni ndogo, vyema pitia kwa wahusika wenyewe mtaani watakupa details zaidi ama kama kuna Anayefanya hio kazi humu atakuja.
Simu ninayo ila sio muda wote nitakuwa eneo la biashara ndio maana nikataka iwepo camera. Nitacheki iyo DSLR ila ningeomba kufahamu hiyo inakuwaje na unaijua vipi?
 
Simu ninayo ila sio muda wote nitakuwa eneo la biashara ndio maana nikataka iwepo camera. Nitacheki iyo DSLR ila ningeomba kufahamu hiyo inakuwaje na unaijua vipi?
Dslr ni kama unavyo sema smartphone ni aina fulani ya camera ambayo inakubali kubadili lens, ina save picha kwenye digital format etc...

Kitu kikubwa ambacho kitakujulisha ni hizo lens zake ambazo zinachomoka. Kimuonekano zipo kama hivi
images-18.jpeg

Second hand unazipata around 300-500K.

Pia unaweza nunua simu ya kazini, kuna simu refurbished kibao around 100K ambazo camera zake ni flagship level za 2019 mfano Xperia 5.
 
Back
Top Bottom