Msaada: Nataka kupata ujauzito.

Msaada: Nataka kupata ujauzito.

The Donchop

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2014
Posts
294
Reaction score
378
Habari wanajamii...
Mimi ni mwanamke mwenye umri wa miaka 25. Hii ni mara yangu ya kwanza kuwa na mpenzi tuliyedumu nae kwa miaka mitatu sasa. Mpenzi wangu aliwahi kuwa na mtoto mmoja kabla hatujakutana naye. Ni mtumiaji mzuri sana wa pombe za kila aina.
Suala lililonileta hapa ni juu ya kushika ujauzito. Mimi na mwenzangu tumekubaliana kuzaa lakini ni miezi zaidi ya sita inakatika bila kushika ujauzito. Tumejaribu mara nyingi kufuata kalenda na mzunguko wangu ni wa siku 28. Lakini bado hatujafanikiwa. Nilienda hospitali napo wakaniambia niko fiti kabisa. Kila kitu kipo sawa.
Naomba msaada wanajamii juu ya hili...
Nifanyeje nishike ujauzito?
 
Pombe ukinywa kupitiliza kila siku huharibu kizazi kwa mwanaume tena shukuru Mungu kama kifanyio kinafanya kazi wengine huwa kinapalalaizi kabisa
 
wish ingekuwa nafasi yangu nataman sana kupata mtoto any way Mimi sio mtaalam ila nenda na mwenzi wako hospital kama iki fail plz ni Pm tuone tunasaidiana vip
 
Kuna dawa inachanganywa na mafuta ya ng'ombe iyo ukitumia siku tatu tu lazima upate
 
Jaribu mechi za nje
Mhh, ndo yale yanayoleta matatizo kwenye ndoa hasa hili la kubambikiwa watoto. Ni vyema huyo mwanamume ukamshauri aache pombe na ikishindikana ukae na ndugu wa muhusika ili myajenge.
 
Mnatafta mtoto huku mnakunywa pombe Kali huko hata ka ungeshika mimba huyo mtoto angepata matatizo. Kunywa pombe si sifa zaid ya kuharibu afya na mwili.
 
Habari wanajamii...
Mimi ni mwanamke mwenye umri wa miaka 25. Hii ni mara yangu ya kwanza kuwa na mpenzi tuliyedumu nae kwa miaka mitatu sasa. Mpenzi wangu aliwahi kuwa na mtoto mmoja kabla hatujakutana naye. Ni mtumiaji mzuri sana wa pombe za kila aina.
Suala lililonileta hapa ni juu ya kushika ujauzito. Mimi na mwenzangu tumekubaliana kuzaa lakini ni miezi zaidi ya sita inakatika bila kushika ujauzito. Tumejaribu mara nyingi kufuata kalenda na mzunguko wangu ni wa siku 28. Lakini bado hatujafanikiwa. Nilienda hospitali napo wakaniambia niko fiti kabisa. Kila kitu kipo sawa.
Naomba msaada wanajamii juu ya hili...
Nifanyeje nishike ujauzito?

Nenda hospitali mkafanyiwe uchunguzi; kwa upande wako ukifanyiwa kipimo cha utra sound inaweza kugundulika kama kuna matatizo maeneo ya uzazi kama vile uvimbe nk ama ikionekana huna tatizo, hata mumeo anaweza kupima ili kujua labda mbegu zake ni dhaifu au lah, mengi mtayapata kwa daktari wa magonjwa ya uzazi.
 
Nendeni hospital wote, yeye kuwa na mtoto sio kipimo, huenda huyo mtoto 49% inahusu
 
  • Thanks
Reactions: BAK
risasi za jamaa hazina madhara badili mboga unaweza bahatika ukashiba tena kwa ki1tu na kuvimbiwa
 
Nenda na mwenz wako mkachekiwe lakin naiman mungu atakujalia utazaa tu kwa sababu miez sita nimichache sana watu wanakaa miaka ming lakin anakuja kuzaa tu
 
wish ingekuwa nafasi yangu nataman sana kupata mtoto any way Mimi sio mtaalam ila nenda na mwenzi wako hospital kama iki fail plz ni Pm tuone tunasaidiana vip
Utazaa tu usijali mungu atakusaidia jaribu kwenda kuchekiwa na mwenz wako
 
Back
Top Bottom