The Donchop
JF-Expert Member
- Jan 10, 2014
- 294
- 378
Habari wanajamii...
Mimi ni mwanamke mwenye umri wa miaka 25. Hii ni mara yangu ya kwanza kuwa na mpenzi tuliyedumu nae kwa miaka mitatu sasa. Mpenzi wangu aliwahi kuwa na mtoto mmoja kabla hatujakutana naye. Ni mtumiaji mzuri sana wa pombe za kila aina.
Suala lililonileta hapa ni juu ya kushika ujauzito. Mimi na mwenzangu tumekubaliana kuzaa lakini ni miezi zaidi ya sita inakatika bila kushika ujauzito. Tumejaribu mara nyingi kufuata kalenda na mzunguko wangu ni wa siku 28. Lakini bado hatujafanikiwa. Nilienda hospitali napo wakaniambia niko fiti kabisa. Kila kitu kipo sawa.
Naomba msaada wanajamii juu ya hili...
Nifanyeje nishike ujauzito?