Msaada: Nateseka na Hali Hii

Msaada: Nateseka na Hali Hii

Habari wakuu,

Nimwaka wa tano sasa nasumbuliwa na :
Maumivu makali shingoni yakiambatana na misuli ya shingoni kukaza.

Uti wa mgongo unakaza pamoja na maumivu kila siku. Siwezi kukaa kwa muda mrefu bila kuegemea sehem.

Taya za mdomo zinakaza, nikipiga mwayo huwa Nasikia Kama mifupa iliyokaza inaachia.

Kifua Kina kaza kiasi nikivuta pumzi kwa nguvu husika mifupa inaachia Kama vile ilikuwa imekaza.

Uchovu wa mwili kila siku ni sehemu ya maisha yangu.

Nimeenda Sana hospital lakini nimeishia kuandikiwa Mi antibiotics mpaka nimechoka.

Msaada nifanyenini ili niondokane na maumivu haya?
Nawasilisha.

Geogismimi etc..
Nina historia cwez isahau aisee ya tatizo linaloshabihiana na lako,ila mm ilikuwa ni maumivu ya kiuno tu.kiuno cha ajabu hiki kiliwahi niuma mpaka nilihisi mwisho wa maisha yangu umefikia maana ilikuwa siwezi kukaa mpaka niegemee nyuma,sikuweza kuinama wala kubeba kitu chenye uzito wa zaidi ya kilo 1.

Nilikwenda Hosp weee nikapewa dawa lakn wapi mpaka nilimtafuta shekh kwa ajili ya dua,akanisomea na kunipatia kombe yaani baada ya hapo sikujua hta kiliishaje maana it took only 3 days niko fit kabisa na hakikurud tena mpaka leo
 
Mimi nna tatizo kama lako nimefanya kipimo juzi tu cha tumbo Barium meal x ray baada ya kuhangaika mda mrefu nimeambiwa nna tatizo linaloitwa Chronic gastritis fuatilia nawe kipimo hiko Mara nyingi ni matatizo ya gesi iliyojaa tumboni na kupanda mpaka kifuani na kuleta msokoto unaoathiri muscles na viungo vingine..bado cjapata tiba muafaka bado nami tatizo hilo linanitesa.
 
Back
Top Bottom