Nyamtala Kyono
Senior Member
- Sep 23, 2010
- 163
- 34
Nunua gold detector upime zinaanzia milioni moja zinapima kuanzia fut 0-3 kwenda chini na kuendelea, hata mwanza zipo
msaada wenu nataka kununua ardhi yaani shamba eneo flan ambalo nimeambiwa ni mwambao wa madini...swali langu je nawezaje kujua kabla sijapanunua na utaratibu ukoje? asanteni
Nunua gold detector upime zinaanzia milioni moja zinapima kuanzia fut 0-3 kwenda chini na kuendelea, hata mwanza zipo
Utaratibu ni kumuomba ruhusa mwenye shamba chukua jembe anza kuchimba. Utakayoyaona ndo yaliyomo.
Hizo gold detector zinapima Gold tu peke yake?
If yes....
Na vp kama madini yanayopatikana kwenye hilo eneo ni tofauti na Gold atawezaje kuyagundua?
bab-D hukunijibu maswali yanguNdugu inadetect aina zote pia inakuonyesha umbali yalipo, ukitaka kununua nitafute nikusaidie kuchagua, usiangukie feki,
Pia ukitaka uzoefu tembelea nigodi (maduara) ya wachimbaji wadogowadogo vifaa hivyo baadh wanavyo au mtafute quter
Ndugu inadetect aina zote pia inakuonyesha umbali yalipo, ukitaka kununua nitafute nikusaidie kuchagua, usiangukie feki,
Pia ukitaka uzoefu tembelea nigodi (maduara) ya wachimbaji wadogowadogo vifaa hivyo baadh wanavyo au mtafute quter
bab-D hukunijibu maswali yangu
Ndugu yangu angalia usidanganyike. Tafuta GPS au mtu mwenye GPS mchukue coordinates za eneo husika kisha tumia hizo points uende ofisi za madini kwenye mkoa wako uwaambie wakupe QDS (Quarter Degree Sheet) yenye points hizo.
QDS kama inavyojieleza ni geological map ambayo ina details nyingi sana za eneo husika kuhusu aina za madini (pamoja na details zingine za kijiolojia).
QDS pia zinapatikana GST Dodoma kwa bei ndogo tu ambayo ni affordable. Chukua tahadhari ndugu haya mambo ya madini yamegubikwa na utapeli mwingi.
Kama una swali uliza.
bab-D kuna mtu aliniambia pia nisikurupuke kununua sababu wakti mwingine unakuta hilo eneo liko alocated kwa mtu na idara ya madini na mwenye shamba hajui hivo anakuuzia...mwisho wa siku huwezi kufanya kitu...kwa hiyo nimemuuliza gwamahala swali i hope atatusaidia sisi wachanga tunaojifunza hii kitu kabla ya kuingia kichwakichwaGwamahala
Unataka kuniambia sehemu zote zenye madini zinajulikana? ingekua hivyo mbona hao jamaa wa huko ulikomuelekeza wangekua washanunua maeneo yote yenyemali aisee,
Gwamahala
Unataka kuniambia sehemu zote zenye madini zinajulikana? ingekua hivyo mbona hao jamaa wa huko ulikomuelekeza wangekua washanunua maeneo yote yenyemali aisee,
Gwamahala. nilisahau. na je hizo QDS zinaweza onyesha ni nani mmiliki wa hiyo site kama imegawiwa ama la?
asante sana mkuu kwa jibu lako zuri sana. nakubaliana na wewe kuwa uangalifu ni muhimu sana. swali langu ni je. hizo gps ni hizi hizi za maofisa ardhi wale wa kuangalia mipaka ya viwanja au zipo gps special kwa madini?...halafu je katika nchi hii hakuna maeneo yenye madini ambayo inawezekana hayapo kwenye geological map ya nchi?
GPS ni hizo hizo ndugu...na procedures ni hizo hizo wanazotumia hata hao wa ardhi.
Wajerumani walishatengeneza geological map ya Tanganyika yote kabla hata ya uhuru...kwahiyo kila sehemu zinajulikana, BUT unaweza kupata aina fulani ya madini ambayo haijaonyeshwa hapo kwenye ramani la eneo husika...tunaita abnormal occurrences. Hiyo inakuwa ni bahati yako coz kwenye QDS labda wameonyesha aina fulani ya madini ambayo si "hot cake", lakini abnormally unakuta precious metals/gemstones.
Kimsingi haya mambo yanahitaji uvumilivu na uweledi sana...nakutia moyo usikate tamaa.
Kama kuna mambo/maswali private...waweza kunitembelea PM.
shukrani sana mkuu gwamahala umenisaidia sana...nikiwa na maswali mengine usinichoke