Msaada: Nawezaje kujua kama ardhi yangu ina madini?

Nyamtala Kyono

Senior Member
Joined
Sep 23, 2010
Posts
163
Reaction score
34
msaada wenu nataka kununua ardhi yaani shamba eneo flan ambalo nimeambiwa ni mwambao wa madini...swali langu je nawezaje kujua kabla sijapanunua na utaratibu ukoje? asanteni
 
Nunua gold detector upime zinaanzia milioni moja zinapima kuanzia fut 0-3 kwenda chini na kuendelea, hata mwanza zipo
 
Hizo gold detector zinapima Gold tu peke yake?
If yes....
Na vp kama madini yanayopatikana kwenye hilo eneo ni tofauti na Gold atawezaje kuyagundua?
 
Utaratibu ni kumuomba ruhusa mwenye shamba chukua jembe anza kuchimba. Utakayoyaona ndo yaliyomo.
 
Nunua gold detector upime zinaanzia milioni moja zinapima kuanzia fut 0-3 kwenda chini na kuendelea, hata mwanza zipo

asante bro.si ninahitaji pia na mtaalam wa madini? kuna mtu aliniambia kuwa baada ya kujihakikishia kuna madini nitahitaji kujua kama eneo hilo halikuwahi kugawiwa kwa mtu kutoka idara ya madini...je utaratibu ukoje?
 
Hizo gold detector zinapima Gold tu peke yake?
If yes....
Na vp kama madini yanayopatikana kwenye hilo eneo ni tofauti na Gold atawezaje kuyagundua?

Ndugu inadetect aina zote pia inakuonyesha umbali yalipo, ukitaka kununua nitafute nikusaidie kuchagua, usiangukie feki,
Pia ukitaka uzoefu tembelea nigodi (maduara) ya wachimbaji wadogowadogo vifaa hivyo baadh wanavyo au mtafute quter
 
bab-D hukunijibu maswali yangu
 
Acha uongo ndugu yangu...!
 
bab-D hukunijibu maswali yangu

Ndugu yangu angalia usidanganyike. Tafuta GPS au mtu mwenye GPS mchukue coordinates za eneo husika kisha tumia hizo points uende ofisi za madini kwenye mkoa wako uwaambie wakupe QDS (Quarter Degree Sheet) yenye points hizo.

QDS kama inavyojieleza ni geological map ambayo ina details nyingi sana za eneo husika kuhusu aina za madini (pamoja na details zingine za kijiolojia).

QDS pia zinapatikana GST Dodoma kwa bei ndogo tu ambayo ni affordable. Chukua tahadhari ndugu haya mambo ya madini yamegubikwa na utapeli mwingi.

Kama una swali uliza.
 
Gwamahala
Unataka kuniambia sehemu zote zenye madini zinajulikana? ingekua hivyo mbona hao jamaa wa huko ulikomuelekeza wangekua washanunua maeneo yote yenyemali aisee,
 
Last edited by a moderator:

asante sana mkuu kwa jibu lako zuri sana. nakubaliana na wewe kuwa uangalifu ni muhimu sana. swali langu ni je. hizo gps ni hizi hizi za maofisa ardhi wale wa kuangalia mipaka ya viwanja au zipo gps special kwa madini?...halafu je katika nchi hii hakuna maeneo yenye madini ambayo inawezekana hayapo kwenye geological map ya nchi?
 
Gwamahala. nilisahau. na je hizo QDS zinaweza onyesha ni nani mmiliki wa hiyo site kama imegawiwa ama la?
 
bab-D kuna mtu aliniambia pia nisikurupuke kununua sababu wakti mwingine unakuta hilo eneo liko alocated kwa mtu na idara ya madini na mwenye shamba hajui hivo anakuuzia...mwisho wa siku huwezi kufanya kitu...kwa hiyo nimemuuliza gwamahala swali i hope atatusaidia sisi wachanga tunaojifunza hii kitu kabla ya kuingia kichwakichwa
 
Last edited by a moderator:
Gwamahala
Unataka kuniambia sehemu zote zenye madini zinajulikana? ingekua hivyo mbona hao jamaa wa huko ulikomuelekeza wangekua washanunua maeneo yote yenyemali aisee,

Swali lako lina mantiki sana.
Ni kweli zaidi ya asilimia 85-90 zinajulikana. Maeneo ambayo hayajulikani ni machache sana...less than 10%. Pia sehemu ambazo "hazijulikani" ni zile tunaita abnormal occurrences...mfano yaani sehemu ambayo usingetegemea kupata dhahabu kijiolojia afu ukaipata.

Kuhusu wanaojua hayo maeneo...yaani wafanyakazi husika kujilimbikizia maeneo, hiyo ipo but ni kwa kiwango kidogo. Ila unatakiwa ufuate mbinu nilizozisema jana...chukua coordinates za eneo husika, tafuta QDS ya/za eneo husika ili upate details za hilo eneo geologically, i.e. minerals available.

Hatimaye ukishajirisha...nenda ofisi za madini uwape hizo coordinates then watakwambia kama hilo eneo linamilikiwa na mtu/kampuni au la.

Kama una swali la ziada uliza tu...pia nimechelewa kukujibu kutokana na majukumu mbalimbali.
 
Last edited by a moderator:
Gwamahala. nilisahau. na je hizo QDS zinaweza onyesha ni nani mmiliki wa hiyo site kama imegawiwa ama la?

Hapana...QDS hazionyeshi nani anayemiliki eneo. Ili ujue kama eneo linamilikiwa au la...cha msingi ni kuchukua coordinates za eneo husika ili uzipeleke ofisi za madini ndipo watakwambia kama lina mtu/kampuni au la.

Ukienda bila coordinates itakusumbua coz itabidi uwaombe muende site ili wachukue coordinates then wakaziingize kwenye database waone status ya eneo ikoje. Tatizo la njia hii ya kuwategemea wao ni URASIMU!!!
Watakuzungusha sana.
 
asante sana mkuu kwa jibu lako zuri sana. nakubaliana na wewe kuwa uangalifu ni muhimu sana. swali langu ni je. hizo gps ni hizi hizi za maofisa ardhi wale wa kuangalia mipaka ya viwanja au zipo gps special kwa madini?...halafu je katika nchi hii hakuna maeneo yenye madini ambayo inawezekana hayapo kwenye geological map ya nchi?

GPS ni hizo hizo ndugu...na procedures ni hizo hizo wanazotumia hata hao wa ardhi.

Wajerumani walishatengeneza geological map ya Tanganyika yote kabla hata ya uhuru...kwahiyo kila sehemu zinajulikana, BUT unaweza kupata aina fulani ya madini ambayo haijaonyeshwa hapo kwenye ramani la eneo husika...tunaita abnormal occurrences. Hiyo inakuwa ni bahati yako coz kwenye QDS labda wameonyesha aina fulani ya madini ambayo si "hot cake", lakini abnormally unakuta precious metals/gemstones.

Kimsingi haya mambo yanahitaji uvumilivu na uweledi sana...nakutia moyo usikate tamaa.
Kama kuna mambo/maswali private...waweza kunitembelea PM.
 
shukrani sana mkuu gwamahala umenisaidia sana...nikiwa na maswali mengine usinichoke
 
Back
Top Bottom