Msaada: Ndugu yangu ambaye ni hakimu anataka kunitapeli mirathi

Microsoft

JF-Expert Member
Joined
Mar 18, 2011
Posts
623
Reaction score
366
Wadau naomba kwa wenye uelewa juu ya hili suala.

Mzazi alikuwa mfanyakazi wa shirika moja linaitwa PLAN INTERNATIONAL hapa Dar, alifariki mwaka 2014.

Baada ya msiba ndugu wakakaa kikao wakamteua mdogo mmoja wa marehemu (hakimu hapa Dar) msimamizi wa mirathi, na wakaamua hela itakayopatikana kutoka katika mafao ya marehemu inunue nyumba Dar es Salaam, alafu hiyo nyumba itakuwa ni mali ya mtoto pekee wa marehemu. Mafao yake yakatoka 2015.

Hela baada ya kutoka (ambayo cheque pia ilikua katika jina la mtoto wa marehemu) ikaingia katika account ya mtoto wa marehemu.

Baada ya hapo mdogo wa marehemu (msimamizi wa mirathi) anakabidhiwa ATM card ili atimize maamuzi ya kikao.

Kilichotokea huyu mjomba amekula baadhi ya hela, maadhimio ya kikao kwamba anunue nyumba hakutekeleza, baada ya kuanza kuulizwa akawa mbogo, mpaka sasa kanunua nyumba ambayo bado hakumalizia kulipia na hataki kuilipia mpaka sasa hana dalili.

Ushahidi upo baada ya ku print bank statement inaonyesha huyu msimamizi wa mirathi amekula Milioni 10.

Huyu mtu anafanya hivi kwasababu ni hakimu wa mahakama moja hapa Dar kwahiyo anaona yeye anaijua sheria kuliko wengine.

Kwa sasa sitataja jina lake ila tarehe 28/Feb nitaleta picha yake hapa, jina kamili Hapa
Najua anasoma kwahiyo uamuzi ni wake.

Msaada ni naomba kujua jinsi ya kumshtaki ili:

1. Alipe hela aliyokula takribani milioni 10
2. Akabidhi nyumba kwa muhusika
3. Naomba kujua kama ninaweza kudai fidia maana tangu hela itoke 2015 mpaka leo ananizungusha na matusi ananitukana nikiuliza.

Kama kuna mwanasheria yupo tayari kunisaidia kupata haki yangu basi reward ipo.



Updates:
Baada ya kufungua huu uzi napata simu za watu nisiowajua wanajifanya wao wananijua na wanataka eti tuonane.

Na kwa habari nilizopata huyu mtu yupo mahakama ya UPANGA kwa sasa.
 
Wapo wanasheria wengi tu humu, Watakuja baadae au kesho
 
NENDA RITA, KWA KABIDHI WASII UKAWASILISHE KADHIA YAKO. ALAMSIK
 
JENGO LA RITA, MTAA WA MAKUNGANYA, ILIPOKUWEPO CLUB BILICANAS. WANAPOTOA VYETI VYA KUZALIWA NA VIFO.
 
Mkuu Microsoft , kwanza niwie radhi kwa kuchelewa kuitikia wito wako kwakuwa jana nilitingwa mno na majukumu ya kulijenga taifa letu. Pili, nataka kujua kama wewe ndiwe mtoto pekee wa marehemu uliyemzungumzia. Tatu, wakati wa uteuzi wa Msimamizi wa Mirathi (naamini uteuzi ulifanyika rasmi Mahakamani), ulikuwa na umri gani? Kwanini hukuteuliwa wewe kama ni mtoto pekee wa marehemu?

Nne, Mkuu Microsoft , kisheria, Msimamizi wa Mirathi si mtu anayepaswa na mwenye haki ya kufaidi mirathi kuliko yeyote awaye. Yeye hupewa majukumu ya kisheria na Mahakama inayomteua kusimamia mirathi kwa faida ya warithi. Wakati mwingine, Msimamizi wa Mirathi naye huwa mmoja wa warithi (akitajwa hivyo na Hukumu ya Mirathi ya Mahakama). Kikubwa ni kuwa Msimamizi wa Mirathi ni msimamizi tu, si aliyerithishwa pekee na kupewa haki ya kufaidi mirathi kuliko wengine.

Kimahakama, jalada la mirathi huwa halifungwi. Yaani, jalada la mirathi halifiki mwisho kirahisi. Sababu kubwa ni pamoja na kurekebisha kasoro zozote zinazoweza kujitokeza katika mirathi husika. Kasoro hizo ni pamoja na zinazomhusu Msimamizi wa Mirathi. Kimsingi, Msimamizi wa Mirathi aweza kubadilishwa au kuondolewa. Ni pale anapofariki au kuugua kwa muda mrefu au hata anapokiuka majukumu yake. Ndiyo kusema, Msimamizi wa Mirathi si mtu wa kudumu katika kuteuliwa kwake.

Kama yeyote mwenye maslahi kwenye mirathi husika ana malalamiko yoyote dhidi ya Msimamizi wa Mirathi, anapaswa kuyawasilisha malalamiko hayo Mahakama ile ile iliyomteua Msimamizi huyo. Labda kama Mahakama ile husika itakataa kuyapokea na kuyasikiliza malalamiko hayo. Mlalamikaji, katika muktadha wako hapa, atapaswa kuthibitisha kuwa Msimamizi wa Mirathi amekiuka au anakiuka wajibu wake wa kisheria wa kusimamia mirathi husika ikiwa ni pamoja na kwenda kinyume na maagizo ya kimahakama wakati wa uteuzi wake.
 
Asante kwa ufafanuzi ndugu Petro,nimefaidika na mimi kidogo japo sina tatizo kama hilo naimani nitaweza kusaidia watu wenye uhitaji kama wa microsoft.Samahani ningependa kuuliza kwa niaba ya Microsoft ili tuzidi kupata ilmu,Je hakimu hawezi kushirikiana na huyo hakimu tajwa kwa vile wanajuana kumkandamiza mlalamikaji?Je Huyo hakimu hawezi kufunguliwa mashataka kwa ubadhirifu wa fedha za mlalamikaji kwa kosa la kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu?Je hakimu hawezi kufunguliwa mashtaka kwa kushtakiwa na mlalamikaji akawa na mwanasheria wa kusimamia swala hili?
Natanguliza shukurani kwa majibu yako mazuri.
 
Mkuu, si jambo jema kuwa na wasiwasi na Mahakama tangu mwanzo. Pili, masuala ya mirathi yanamalizwa katika taratibu za kimirathi, si kama jinai. Msimamizi wa Mirathi akiondolewa rasmi, masuala ya kijinai yanaweza kuripotiwa na hatua stahiki kuchukuliwa. Katika kesi za jinai hapa Tanzania, Jamhuri ndiye mwendeshaji kupitia Waendesha Mashtaka wa Serikali. Bado hakuna mazoea ya Mwendesha Mashtaka binafsi.
 
Ameshafafanua kwamba taarifa za benki zinaonyesha tayari jamaa keshachota kiasi cha pesa milioni kumi.
Nadhani hapa ndipo penye tatizo kubwa na anauliza je anaweza kumshitaki ili amrudishie pesa zake?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…