Wadau naomba kwa wenye uelewa juu ya hili suala...
Mzazi alikua mfanyakazi wa shirika moja linaitwa PLAN INTERNATIONAL hapa Dar, lifariki mwaka 2014,
Baada ya msiba ndugu wakakaa kikao wakamteua mdogo mmoja wa marehemu (hakimu hapa Dar) msimamizi wa mirathi ,na wakaamua hela itakayopatikana kutoka katika mafao ya marehemu inunue nyumba Dar es Salaam,alafu hiyo nyumba itakua ni mali ya mtoto pekee wa marehemu
Mafao yake yakatoka 2015,
Hela baada ya kutoka (ambayo cheque pia ilikua ktk jina la mtoto wa marehemu) ikaingia katika account ya mtoto wa marehemu.
Baada ya hapo mdogo wa marehemu(msimamizi wa mirathi) anakabidhiwa ATM card ili atimize maamuzi ya kikao.
Kilichotokea huyu mjomba amekula baadhi ya hela,maadhimio ya kikao kwamba anunue nyumba hakutekelezä,baada ya kuanza kuulizwa akawa mbogo, mpaka sasa kanunua nyumba ambayo bado hakumalizia kulipia na hataki kuilipiä mpaka sasa hAna dalili.
Ushahidi upo baada ya ku print bank statement inaonesha huyu msimamizi wa mirathi amekula Milioni 10,
Huyu mtu anafanya hivi kwasababu ni hakimu wa mahakama moja hapa dar kwaiyo anaona yeye anaijua sheria kuliko wengine.
Kwasasa sitataja jina lake wala mahakama anayofanya kazi.ila kama atatokea mtu wa kunisaidia nitamwanika hapa yeye, namba yake ya simu na picha yake.
Na amewahi kufanya kazi mahakama ya mwanzo Kariakoo.
Msaada ni naomba kujua jinsi ya kumshtaki ili
1.Alipe hela aliyokula takribani milioni 10
2.Akabidhi nyumba kwa muhusika
3.Naomba kujua kama ninaweza kudai fidia maana tangu hela itoke 2015 mpaka leo Ananizungusha na matusi ananitukana nikiuliza.
Kama kuna mwanasheria yupo tayari kunisaidia kupata haki yangu basi reward ipo.
View attachment 698328