Msaada ndugu zangu, baba hanitaki kwake kisa naipenda CCM

Msaada ndugu zangu, baba hanitaki kwake kisa naipenda CCM

kikoozi

JF-Expert Member
Joined
Jun 24, 2015
Posts
2,094
Reaction score
3,108
Habarini ndugu zangu, poleni na majukumu niende moja kwa moja kwenye maada

Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 31, nahishi Dar

Kumetokea sintofahamu kati yangu mimi na mzee wangu (baba yangu mzazi)

Baada ya kumuambia mazuri yaliofanywa na serikali ya awamu ya 5 na 4

Baba yangu aliniambia kama nataka siasa niondoke kabisa nyumbani kwake niende huko kwenye chama changu nikafanye siasa

Kuna kipindi nilipewa kazi na mjumbe niorodheshe majina ya wanachama wapya wa CCM, nikaenda nyumbani kuanza nimshawishi mzee achukue nae kadi, huwezi amini baba yangu mzazi wa kunizaa alinishikia koleo akitaka kunipiga nalo usoni

Sikulala nyumbani siku mbili akiniambia kama nataka mambo ya CCM nihame kabisa kwakwe na nisikanyage

Mimi nimemaliza chuo mwaka 2016, ngazi ya degree kwa sasa sina kazi nipo home nimemueleza mzee wangu jana usiku kuwa nahitaji kugombea udiwani mwaka huu kwa tiketi ya CCM, nikaomba awe na kadi ya chama ili anipe support mimi mtoto wake kwenye kura za maoni

Baba yangu alitaka kunipiga na panga, na anasema niondake kwake haraka sana na nisikanyage tena,

Wakuu sina pa kwenda na hapa ndio nyumbani kwetu

Baba yangu anachofanya sio hekima kabisa, naombeni mnisaidie nipate haki yangu ya kukaa kwetu wakuu

Natanguliza shukrani sana, Mungu awabariki

Sent using komputa mpakato
 
Kila mtu aheshimu anachokiamini.

Huenda kipaumbele chake ni masuala ya IMANI(DINI)

Au inawezekana siasa(bila kujali zinatoka mlengo gani) zimemsababishia maumivu ambayo kamwe hataki mwanae yampate.

Heshimu fikra zake usiendekeze Kikoozi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi niliachana na mpenzi wangu kwa ushabiki wa kivyama CHADEMA Vs CCM!
 
Umemaliza chuo na una miaka 31 bado unataka kushindana na babako nyumbani.. Change bro. kuna mambo mengi ya kufanya
 
Huyo Mzee anahitaji ushauri nasaha aishi kwa matumaini.. Tanzania upinzani kushika dola wasahau ama wakae parking kwanza..
31 old man upo nyumbani unatuabisha.
 
Mimi niliachana na mpenzi wangu kwa ushabiki wa kivyama CHADEMA Vs CCM!
Afadhali wewe mpenzi mimi mchumba...Nilipiga chini kwa kushabikia upuuzi! na wala sikujuta,na sijajuta!
Utawezaje kukaa na mtu ambaye kwenye Mambo ya Msingi hamuendani afadhali hata awe mwanachama wa vyura kindakindaki ...hilo lina nafuu!
Kwako wewe kijana ,mleta mada ; Mzee wako yupo sahihi kabisa .you derseve it!
 
Huyo Mzee anahitaji ushauri nasaha aishi kwa matumaini.. Tanzania upinzani kushika dola wasahau ama wakae parking kwanza..
31 old man upo nyumbani unatuabisha.
Babaake hajamchagulia chama.
Ila nadhani baba anajutia kupoteza ada kwa kumsomesha mtoto ambaye miaka 31 analalama kufukuzwa kwao.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo mzee anaakili sana..anajua matatizo yote ya nchi hii likiwepo ukosefu wako wa ajira yamesababishwa na hilo lichama unaloshabikia...anshindwa kuelewa hiyo shule ulikuwa unafanya nini...Ushauli ni sasa wew nenda kwa mwenyekiti wako ccm ulipo atakusaidia mkuu
 
kitaa kwetu kuna dingi anamlalamikia mwanae kuwa anajaza shimo la choo, huyo mwana lazima atakuwa ndo huyu mtoa mada.

30 age bado unakaa kwa mshua.! ahh kweli ccm haiwezi kutoka madarakani kwa mambo kama haya
Watoto wa matajiri kijana ana miaka 35 na yuko kwa wazazi wake akisimamia/kuendesha miradi ya kifamilia,kijana wa maskini miaka 23 anaambiwa aende akapange geto huku hata uhakika wa kula ukiwa haupo,anapata demu anapiga mimba anaongeza mtoto mwingine wa kwenda kusoma elimu bure,chain ya umaskini inazidi kuongezeka.

dodge
 
Babaake hajamchagulia chama.
Ila nadhani baba anajutia kupoteza ada kwa kumsomesha mtoto ambaye miaka 31 analalama kufukuzwa kwao.


Sent using Jamii Forums mobile app
Baba anajuta 31 yupo nyumbani. Ada alilipiwa na Mama yake. Mkuu vipi pitia abdiko nujta kwa nukta ongeza na umri wa mleta mada utagundua ni mtoto wa Mama from BAVCHAA.
 
Back
Top Bottom