Habarini ndugu zangu, poleni na majukumu niende moja kwa moja kwenye maada
Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 31, nahishi Dar
Kumetokea sintofahamu kati yangu mimi na mzee wangu (baba yangu mzazi)
Baada ya kumuambia mazuri yaliofanywa na serikali ya awamu ya 5 na 4
Baba yangu aliniambia kama nataka siasa niondoke kabisa nyumbani kwake niende huko kwenye chama changu nikafanye siasa
Kuna kipindi nilipewa kazi na mjumbe niorodheshe majina ya wanachama wapya wa CCM, nikaenda nyumbani kuanza nimshawishi mzee achukue nae kadi, huwezi amini baba yangu mzazi wa kunizaa alinishikia koleo akitaka kunipiga nalo usoni
Sikulala nyumbani siku mbili akiniambia kama nataka mambo ya CCM nihame kabisa kwakwe na nisikanyage
Mimi nimemaliza chuo mwaka 2016, ngazi ya degree kwa sasa sina kazi nipo home nimemueleza mzee wangu jana usiku kuwa nahitaji kugombea udiwani mwaka huu kwa tiketi ya CCM, nikaomba awe na kadi ya chama ili anipe support mimi mtoto wake kwenye kura za maoni
Baba yangu alitaka kunipiga na panga, na anasema niondake kwake haraka sana na nisikanyage tena,
Wakuu sina pa kwenda na hapa ndio nyumbani kwetu
Baba yangu anachofanya sio hekima kabisa, naombeni mnisaidie nipate haki yangu ya kukaa kwetu wakuu
Natanguliza shukrani sana, Mungu awabariki
Sent using
komputa mpakato