Msaada: Nifanyaje kuhusu matatizo haya ya gari?

NYAGI DRY

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2011
Posts
379
Reaction score
165
Habari zenu humu,

Juzi nilikuwa natoka Dar es salaam na gari aina ya Toyota Porte, nikatoka vizuri Dar es salaam tulipofika Manyoni gari ikachemsha, tukaenda kwa fundi akafungua injini akasema gasket zimeungua na tena cylinder head imepinda, sasa ikarekebishwa pale ikakaa vizuri,

Tukiwa njian kulekea Singida mjini taa ya check engine ikawaka tukakagua gari tukagundua kwamba oil ilikuwa haipandi sasa tukatafuta fundi usiku ule ule akarekebisha chujio la oil kule kwenye sample,

safari ikaendelea tulipofika Nzega tukasikia kitu kama kimedondoka kusimama kuangalia, tukakuta vichuma kama piston, na inaonesha injini imefumukia karibu na sample, sasa safari ikaishia hapo.

Je, wataalam humu ndani, nifanyeje? Makosa yalikuwa wapi? Manake service nilifanya wakati naanza safari

÷÷÷÷÷÷÷MREJESHO÷÷÷÷÷÷÷÷÷÷
Wapendwa niwashukuru sana kwa maoni yenu, nilifanikiwa kutafuta engine nyingine ya porte , manake ilikuwa ni 1NZ ..CC 1490 .. nilinunua ilala mwenyewe milion moja na laki 3 nkishirikiana na mafundi, nikaisafirisha mpk kigoma, nikamtafuta fundi mjuz akaishusha engine akaipandisha , nikamlipa elfu 60
Chombo imekuwa kama mpya , gari imepona iko poa , chombo inataka safari , chombo inaita,
Nilifanya road test kigoma mpk kibondo nakurudi ,
Nitazingatia service na maelekezo yote ..nawashkuru sana wadau .
 
Umenikumbusha Toyota Port nilikuwa nayo ikafanya mchezo huu huu ya kwako iliyokufanyia.

Nadhani hizi gari toyota zenye cc chini ya 1700 si recommended kwa safari ndefu. Ni in town cars.

Safari ndefu inabidi uende mwendo wa kobe kwa kupumzika pumzika.

Kama ni mtu wa safari utlist pendelea cc kuanzia 2000 kwenda mbele. Ikiwa six unaenjoy safari zaidi.
 
Nunua engine ingine. Ushakaanga engine. Hapo sababu zinaweza kuwa 100 au zaidi.
 
Watu wanazi-overwork hizo gari. Hizi ni gari za stop start mjini. Sasa unakutana na mtu anatoka Dar Arusha na unamkuta analeta ligi na Brevis,Crown matokeo yake ndio haya.
 
Watu wanazi-overwork hizo gari. Hizi ni gari za stop start mjini. Sasa unakutana na mtu anatoka Dar Arusha na unamkuta analeta ligi na Brevis,Crown matokeo yake ndio haya.
Kuna Porte nishawahi weka nayo ligi duh, aisse yule dere hatari. Sema pona yake hafuati vibao vya 50kph ndio maana ila duh kwa ile speed na ile safari, usikute ndio mtoa mada.
 
Kuna Porte nishawahi weka nayo ligi duh, aisse yule dere hatari. Sema pona yake hafuati vibao vya 50kph ndio maana ila duh kwa ile speed na ile safari, usikute ndio mtoa mada.
Yaani mtu anaanzisha ugomvi ambao anajua atapigwa tu. Hao huwa nawadhalilisha unaenda kumkata kwenye speed over 150kph akiangalia anaona kifo nje nje!
 
Watu wanazi-overwork hizo gari. Hizi ni gari za stop start mjini. Sasa unakutana na mtu anatoka Dar Arusha na unamkuta analeta ligi na Brevis,Crown matokeo yake ndio haya.
Ni kweli mkuu, tatizo ni kwamba umaskini wa fedha na mawazo unatufanya tusiwe na matumizi sahihi ya magari.

Unakuta mtu kanunua mark x halafu kainyanyua juu ili ifanye kazi ya SUV.
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji119][emoji119][emoji1787][emoji1787][emoji1787]huwa inaleta muonekano mbaya sana...utafikiri drone ya US inaenda kupiga Iran.
Ni kweli mkuu, tatizo ni kwamba umaskini wa fedha na mawazo unatufanya tusiwe na matumizi sahihi ya magari.

Unakuta mtu kanunua mark x halafu kainyanyua juu ili ifanye kazi ya SUV.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu pole sana kwa kuua injini...yes..the simple and genuine answer is you have killed your engine...

Hapo hakuna suluhisho zaidi ya kununua Engine nyingine ufunge hapo..

Sababu za kuua hiyo injini....
1...Inaonekana ulikuwa unafanya service za bei rahisi bila kutumia bidhaa zenye ubora....pengine ulifuata ule ushauri wa watu wanaosema service za Toyota ni bei rahisi.

2....Pengine gari yako ulishauriwa utoe thermostat na mafundi wa mtaani, na wewe ukafanya hivyo, au ulianza safari bila kukagua kiwango cha coolant, au unatumia maji ya bombani...hii ndiyo imepelekea kuunguza head pamoja na gasket yake...Too Sad[emoji29][emoji29][emoji29]..kuunguza head si swala la kitoto inaonekana kuna makosa makubwa yalifanyika.

3...Toyota porte nadhani haizidi cc 1300, isijekuta ulikuwa unafukuzana na V 8 zinazowahisha viongozi kwenye majukumu yao....engine ikawa over heated na kupelekea kuunguza head na gasket..

4....Service ya oil uliyofanya kabla ya safari ilikuwa ya kiwango cha chini.....zaidi oil filter kama ulitumia zile za 3500/- mpaka 5000/- hizi huwa hazimudu safari ndefu...zinavimba na kuchanika yale makaratasi ya ndani yanayochuja oil na kufanya kuziba njia ya oil....hapo ndipo ulipoona vyuma vinaanza kudondoka vyenyewe....

HIZI ZOTE NILIZOTAJA HAPA NI ASSUMPTIONS LAKINI ZINAWEZA KUWA NDIYO ZIMEUA ENGINE YAKO.

ANGALIZO...
Gari ikishakuwa chini ya cc1500, usiilazimishe safari ndefu, ibembeleze.... accelerate reasonably...usifanye ligi, acha gari ichanganye yenyewe...waache wenye Subaru, V8, Brevis, Fuga waende zao.

Fanya service zenye ubora kwa kutumia bidhaa bora, coolant, oil na filter.

Ni hayo tu machache.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naona Sae-40,maji ya bomba,kutoa thermostat kumeshaleta majibu kwny engine tayari.
 
Na mimi napata hisia hizo zaidi ya asilimia 95...[emoji37][emoji37]
Kwa sababu nina mshkaji wangu yupo Dar ana Toyota porte...kwao ni Kagera na ameshaenda nayo Kagera mara mbili bila shida..

Sent using Jamii Forums mobile app
Hahah hisia zako ziko sahihi mkuu,maana 1NZ-FE/2NZ-FE hazinaga magonjwa ya ajabu ajabu.

Hapo ni poor services au mambio barabarani kila saa mshale uko kwny red line,shughuli ndo inakuaga hivyo.
 
Vp kuhusu hivi vi IT kama passo na ist tunavyokimbizana navyo barabarani kwenye mikoani na nje ya nchi, madereva wao wanavicharaza ipasavyo
 
Hahah hisia zako ziko sahihi mkuu,maana 1NZ-FE/2NZ-FE hazinaga magonjwa ya ajabu ajabu.

Hapo ni poor services au mambio barabarani kila saa mshale uko kwny red line,shughuli ndo inakuaga hivyo.
Yes.[emoji4][emoji4]...poor services ndiyo inyowacost watu wengi bila wao kujua...

Waswahili wanasema. Rahisi ni ghali.....na Ghali ni rahisi..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukiviendesha kwa adabu na kuzingatia service zenye ubora, na kuwaacha wanaume wa Fuga, Crown, V8, Forester waende zao..utawakuta mbele ya safar....wala hakuna taabu...
Taabu ni kuanzisha ligi...unazungusha injini mpaka kwenye Red zone......Hatari sana...[emoji119][emoji119][emoji119][emoji119][emoji119][emoji119][emoji119]
Vp kuhusu hivi vi IT kama passo na ist tunavyokimbizana navyo barabarani kwenye mikoani na nje ya nchi, madereva wao wanavicharaza ipasavyo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vp kuhusu hivi vi IT kama passo na ist tunavyokimbizana navyo barabarani kwenye mikoani na nje ya nchi, madereva wao wanavicharaza ipasavyo

Vile vinaendeshwa kwa speed hio wkt vikipelekwa huko nje ya nchi na ni safari 1 tu,sasa akiendeshe hivyo kila siku ajionee mziki wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…