Msaada: Nifanyaje kuhusu matatizo haya ya gari?

Kuna mdau mmoja amesema mtoa mada kakimbia , hapana , sijakimbia nipo na nilikuwa napitia michango ya watu , hii porte ni cc 1490, na ilikuwa inatumiwa na mwanamke , kwaiyo ilikuwa inaletwa kigoma kwa mteja , sasa hayo majanga yaliyotokea hapo mwenye aliuza gar kakubali kununua engine nyingine ivishwe,
Inaonesha mtu aliekuwa anafanya services hakuwa anafanya services vizuri
Ila yote kwa yote asanten kwa michango yenu
 
Siku ambayo utamwaga oil mwambie fundi wako aifungue rejeta isafishwe alafu uanze kutumia coolant.
 
Wanawake wanaonewa sana na mafundi. Unakuta anatoa hela gari haifanyiwi service wanamlia hela tu.
 
Point ya msingi sana umeongea hapa.....
Poor beautiful B ladies...[emoji29][emoji29][emoji29][emoji29][emoji29].

Magari mengi yanayomilikiwa na wanawake huwa na hali nzuri sana kwa upande wa body...

Ila engine huwa miozo kwa sababu...
Wadada wengi hawana knowledge na mashine, na wengi wao hawapendi kuumiza kichwa kuhusu mashine....

Hii inapelekea wao kumpigia fundi simu, fundi anachukua gari na kwenda kulifanyia service wakati dada yupo, Home, Saluni au Kazini...

Matokeo yake fundi anaweza kuweka oil ya kupima ili apate cha juu...


Sent using Jamii Forums mobile app
 

Umepata madini ya kutosha. Elimu haina mwisho kwa hiyo mkuu next time chukua tahadhari
 
Siyo kweli, nina fielder 1500cc napiga nayo trip za mikoa sana, na haijasumbua hata

Sent
 
Tatizo siyo kuwekwa kila siku...
Hata kama inawekwa mara moja ndani ya miaka 10

..gari linaweza kupata msukosuko wowte na kupelekea coolant kuisha..mfano kuvuja kwa baadhi ya pipes au kupata ajali na kupasua radiator..
Matengenezo yakishafanyika, baadhi ya watu wanakwepa gharama za coolant wanajaza maji ya bomba..

Lakini pia kuna magari yanavuja mifumo ya upoozaji, unakuta zile pipes za mipira zimekakamaa na kutoboka matundu madogomadogo hivyo unaku ta kila baada ya siku 3, unalazimika kuongeza coolant....hizo gharama za coolant mfano nusu lita kila baada ya siku 3, kuna watu wanazikwepa....akiamka asubuhi anaongeza maji ya bomba...

In the long running, baada ya kama miezi miwili hivi, automatically coolant inakuwa replaced na maji ya kawada...

Suala la kuongeza coolant mara kwa mara ni suala la kawaida sana kwa magari ambayo yameshakaa muda mrefu..
Lakini pia unaweza ukawa safarini, katikati ya vijiji vya watu gari likachemsha, ukafungua mfuniko wa radiator coolant ikaruka nje, wasamaria wanakusaidia maji ya kawaida unajaza, siku ukirudi mjini hufanyi badiliko unaendwlwa na maji ya bomba...
Ha ha kwani coolant inawekwa kila siku.. Ni kukosa akili tu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana... Badilisha engine...


Cc: mahondaw
Sawa , iyo itafanyika ! Ila kuna mtu alishauribakasema baala yakuingia gharama zote za kununua engine , bora kununua kitu kinaitwa mswaki , kureplace hiyo engine, hapo mnasemaje wadau mnaushauri gan
 
Sawa , iyo itafanyika ! Ila kuna mtu alishauribakasema baala yakuingia gharama zote za kununua engine , bora kununua kitu kinaitwa mswaki , kureplace hiyo engine, hapo mnasemaje wadau mnaushauri gan

Duu!! Hapo kwenye mswaki mimi mgeni...


Cc: mahondaw
 

Je mkuu kwa VITZ RS c.c 1500 vp haifai kwa safar mdefu


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakati fundi wa Manyoni amekwambia head imepinda ulinunua head nyingine au ndo alikufungia tu kwa wewe kudhani urahisi na yeye kutamani pesa yako
JAH Rastafari Morning Africa.Trust JAH respect nature
 
Pole sana,niliwahi kupata na mfumuko huo wa engine ilikuwa ni Ipsum old model na engine 3s,nilitoka vizuri Manyara kufika Morogoro gari ikawa na misfire,nikandelea nazo mpaka kufika Dar,kesho yake nikampa fundi,yule fundi akawasha gari na ilipowaka alikanyaga moto kwa nguvu sana,nilichoshuhudia ni mzinga mkubwa kwenye engine na gari ikazima,tulipoangalia chini ya gari ni vipande vya piston na cylinder head,na tundu kubwa limetokea kwenye engine block,engine ilipofunguliwa uharibifu ulikuwa mkubwa sana,solution ilikuwa ni kununua engine nyingine au half engine,kwa uwezo wangu mdogo nikaopt half engine,ingawa gari ilipona ila haikurudi kwenye normal perfomance.Kwahiyo kwa yaliokukuta ndugu wala usipoteze pesa,ulizia bei ya engine na kama mfuko unaruhusu bandika nyingine...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sio kweli mkuu. Huwa nassfiri na toyota passo 990cv mara kadhaa dar mwanza haijawahiniletea shida, hizi ni engine tu kama hizo kubwa unazozisema cha msingi acha ligi. Kama mimi speed yangu huwa 100 ikizidi 120. Tena kwenye miteremko na vile vitambarale. Engine huwa haichoki mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…