Mkuu pole sana kwa kuua injini...yes..the simple and genuine answer is you have killed your engine...
Hapo hakuna suluhisho zaidi ya kununua Engine nyingine ufunge hapo..
Sababu za kuua hiyo injini....
1...Inaonekana ulikuwa unafanya service za bei rahisi bila kutumia bidhaa zenye ubora....pengine ulifuata ule ushauri wa watu wanaosema service za Toyota ni bei rahisi.
2....Pengine gari yako ulishauriwa utoe thermostat na mafundi wa mtaani, na wewe ukafanya hivyo, au ulianza safari bila kukagua kiwango cha coolant, au unatumia maji ya bombani...hii ndiyo imepelekea kuunguza head pamoja na gasket yake...Too Sad[emoji29][emoji29][emoji29]..kuunguza head si swala la kitoto inaonekana kuna makosa makubwa yalifanyika.
3...Toyota porte nadhani haizidi cc 1300, isijekuta ulikuwa unafukuzana na V 8 zinazowahisha viongozi kwenye majukumu yao....engine ikawa over heated na kupelekea kuunguza head na gasket..
4....Service ya oil uliyofanya kabla ya safari ilikuwa ya kiwango cha chini.....zaidi oil filter kama ulitumia zile za 3500/- mpaka 5000/- hizi huwa hazimudu safari ndefu...zinavimba na kuchanika yale makaratasi ya ndani yanayochuja oil na kufanya kuziba njia ya oil....hapo ndipo ulipoona vyuma vinaanza kudondoka vyenyewe....
HIZI ZOTE NILIZOTAJA HAPA NI ASSUMPTIONS LAKINI ZINAWEZA KUWA NDIYO ZIMEUA ENGINE YAKO.
ANGALIZO...
Gari ikishakuwa chini ya cc1500, usiilazimishe safari ndefu, ibembeleze.... accelerate reasonably...usifanye ligi, acha gari ichanganye yenyewe...waache wenye Subaru, V8, Brevis, Fuga waende zao.
Fanya service zenye ubora kwa kutumia bidhaa bora, coolant, oil na filter.
Ni hayo tu machache.
Sent using
Jamii Forums mobile app