Tatizo siyo kuwekwa kila siku...
Hata kama inawekwa mara moja ndani ya miaka 10
..gari linaweza kupata msukosuko wowte na kupelekea coolant kuisha..mfano kuvuja kwa baadhi ya pipes au kupata ajali na kupasua radiator..
Matengenezo yakishafanyika, baadhi ya watu wanakwepa gharama za coolant wanajaza maji ya bomba..
Lakini pia kuna magari yanavuja mifumo ya upoozaji, unakuta zile pipes za mipira zimekakamaa na kutoboka matundu madogomadogo hivyo unaku ta kila baada ya siku 3, unalazimika kuongeza coolant....hizo gharama za coolant mfano nusu lita kila baada ya siku 3, kuna watu wanazikwepa....akiamka asubuhi anaongeza maji ya bomba...
In the long running, baada ya kama miezi miwili hivi, automatically coolant inakuwa replaced na maji ya kawada...
Suala la kuongeza coolant mara kwa mara ni suala la kawaida sana kwa magari ambayo yameshakaa muda mrefu..
Lakini pia unaweza ukawa safarini, katikati ya vijiji vya watu gari likachemsha, ukafungua mfuniko wa radiator coolant ikaruka nje, wasamaria wanakusaidia maji ya kawaida unajaza, siku ukirudi mjini hufanyi badiliko unaendwlwa na maji ya bomba...
Sent using
Jamii Forums mobile app