Fanya biashara ya mekyuri, nakupa mfano nanunua mekyuri kg 1 kwa laki 5 maana sasa ni adimu ila kabla ilikuwa laki 3 nauza gram 1 kwa shs elfu 1, Ila sasa kwa kuwa ni adimu nauza shs 1500 kwa gram 1, piga hesabu utaona faida yake
Ila changamoto yake haitoki upesi inachukua muda hivyo lazima uwe na biashara nyingine ndogo ya kukupa hela ya kula
Wazo la pili kwa hiyo 1m tafuta till za uwakala wa mpesa, tigo, halopesa na Airtel kisha nenda mgodi wwt wa dhahabu uliochangamka ambapo utakuta kutokana na changamoto za upatikanaji wa huduma hizo mteja akirusha hela kuna hela nyingine anakulipa tofauti na ile commission unayopewa na mtandao itakusaidia sana