kindikinyer leborosier
JF-Expert Member
- Jan 6, 2018
- 456
- 833
Assalam wanajamvi? Bila shaka mpo salama na mnaendelea vyema na majukumu!
Bila kupoteza muda niende moja kwa moja kwenye mada, mimi ni mwajiriwa wa taasisi moja binafsi, mwaka jana nilipata changamoto mbaya sana inayonipelekea kukosa amani sana.
Kazini mimi ni mchangamfu sina shida na mtu, na hua mara nyingi nakaa kimya, kwenye kujadili mambo ya watu, January 2022 nilipewa vitengo viwili nivisimamie, kimoja nisimamie mwenyewe kingine nisimamie na mwenzangu, nilikubali kwa mikono miwili lkn baadae mwenzangu akaniambia kwasababu yeye amepangiwa kitengo kizito kidogo anaomba mm nimsaidie tuu, kama kutakuwa na shida atakuwa na mimi!
Nilikubali maana jamaa ni mtu wa maneno mengi na mjuaji sana nikaanza kukomaa!
Kazini kuna mashindano sana ya kampuni mbili za mmiliki huyu (ana kampuni mbili) wanashindana sana uzalishaji, kwa upande wa kampuni ya pili idara yangu aliwekwa jamaa moja ambae alifukuzwa kutoka kwetu na mkuu wetu pale, hivyo alikua mshindani wangu mkubwa japo mimi mwanzo sikujali sana!
Ahafla mapema mwezi wa sita nikapata ajali mbaya sana, niliumia sana nyonga, na ajali hiyo niliipata nikiwa naenda kazini, ilikuwa mbaya sana maana nilifikishwa kitengo cha dharura hospitali ya dharura na baadae nikapelkwa hospitali ya taifa kwa kutazamwa zaidi, kwani niliumia sana njia ya mkojo na ilibidi nifanyiwe opereshen.
Picha linaanza:
1. baada ya kutoa taarifa kazini walikaa kimya ikawa ni zile pole za kishkaji tuu, lkn kuhusu fedha nikawa najigharamia, kikao kikakaa nasikia walibishana sana kwenye kikao hatimae wakachanga laki 3, na ofisi ya mkurugenzi ikatoa laki moja huku mm nikitumia zaidi ya mil 3 kwani bima yangu iliisha muda wake mwaka huo.
2. Wakati nipo hoi hospitali napigiwa simu na makamu mkuu wa kitengo, mwanzo sikutaka mupokea lkn alipiga mara nyingi sana, ikabid nipokee, akawa ananiomba nikiweza nikodi pikipiki hivyo hivyo nifike kazini ili nipate ruhusa niliumia sana kwan muda huo nilikua natoka chumba cha opereshen! lkn nilijikaza tuu nikamwabia nitaangali!
3.Baada ya siku mbili kupita alikuja mkuu wa idara kuja kunitazama, kuthibitisha, doh!! alipofika akanipa fedha zile za watumishi na za mkurugenzi, na kupiga picha, alipofika kazini akatangaza "Kindikinya amepata ajali mbaya sana, hata kama atapona, hata kuwa na uwezo tena wa kuwa na mwanamke" nilipata simu nyingi za pole na wengine kuniambia nisijali nitakuwa sawa, niliachana nao kwani nilihakikishiwa nitakuwa sawa na madaktari!
Miezi miwili baada ya kupita, nilijikaza sana nikarudi kazini, kwakweli nilikuta kila kitu kipo hovyo, ilibidi nijikaze sana kupambana, kurudisha hali sawa, nilijituma sana, hadi kufikia desemba hali ikawa walau!
Sasa yote hayo mwaka huu, repoti baada ya kutoka, idara yangu imeshusha sana utendaji kazi, kwa kunilinganisha na yule mshindani wangu wa pili amenizidi sana!
Picha likaanza nikashushwa idara, pili akaletwa mtu mwingine kushika kitengo kile cha ziada, nimekaa kimya, jana nimeshushwa kabisa na kuwa mtumishi wa kawaida, nilikua kimya tuu sikusema kitu, ila maneno yamekuwa mengi sana, yule mkuu aliekuwa akitangaza siwezi kuwa sawa tena, anatangaza kuwa kama si yeye ningefukuzwa kazi, kwakweli nimeumia sana, lkn hua nakaa kimya sana. kila ukitulia linakuja jipya, ninaumia sana, imefikia hatua mpaka nattaka kuacha kazi nitafute kazi nyingine, lkn changamoto za sasa kidogo kupata kazi sio, ushirikina ni mwingi sana, majungu, kutokupendana ah!!
Naombeni ushauri ndugu zangu nifanyaje hapa niwe na amani? asanteni sana