Usiondoke hapo. Ukijiengua kila pasipo na amani hata nchini kwako utaondoka maana kote kuna mapichapicha. Shukuru hata una kazi, wengne tunazitafuta hatari.
Wewe ni mwanaume. Jisemeshe kwamba hili nalo litapita. Ni nyakati tu ambazo huwa hazilast muda mrefu. Afu nikupe tip..acha kusikiliza maneno ya watu. Ingia ofisini, fanya kazi, ondoka. Kaa katika nafasi yako vizuri. Afu saiv shukuru umepata ample time ya kufanya mitikasi mingine. Buni mambo kichwani, umiza akili yako ili upate mradi ama biashara ingine (kama huna) ambayo itakuingizia kipato.
Makazini hakunaga true friends kunakuwaga na unafiki sana, hvyo establish boundaries..afu usipende kushiriki katika kuongelea ama kujadili co-worker wenzako. Ukishiriki katika hayo mambedha, na wewe utakua unajadiliwa tu. Maana unakua umepanda mbegu..utavuna matunda yake.
Lakini pia nakuasa..sikulazimishi, sijui wewe ni dini gani ndugu. Katika dini ama imani yako..tafuta kumjua muumba wako. Jizoeze kuishi maisha ya uchaji na ibada. Sisemi uwe addicted kwenye mambo ya Imani..nope, namaanisha seek your Lord because kuna this peace huwa inakuja. Hasa pale unapokumbuka ahadi au neno kutoka katika vitabu vya dini. Kuna namna ufahamu wako utakuwa rejuvinated vizuri mno. Ila kama ulikuwa mchaji, ongeza kiwango chako cha ibada more and more. Panda viwango..kama ulikua hufungi, funga atleast once or twice per week. Kufunga huwa inasaidia sana kushape nafsi zetu..na kutiisha miili yetu.
Maisha sio kwenda staight..hamna iyo. Maisha yana kupanda na kushuka. Accept hapa umeshuka..lakini hiyo ni stepping stone...kuna accelerator unaiendea itakayokulift higher than stage uliyotoka...Stay strong..it shall pass.