Yawezekana una msongo wa mawazo, ondoa kwanza msongo wa mawazo kisha hakikisha kuwa hufanyi zinaa maana yake awe mke wako wa ndoa maana wakati mwingine performance inachangiwa na amani ya rohoni mwako, kama ni uzinzi huwezi kuwa na hiyo amani hivyo utaishia kushindwa tu na mwisho utaanza kumeza viagra.
Kama uliyenaye ni mke wa ndoa, hakikisha unapata chakula bora, epuka sana nafaka zilizokobolewa na tumia asali na mdarasini badala ya chai. Kabla ya kulala koroga asali na mdarasini kama kijiko kimoja kimoja hivi, weka kwenye maji ya moto unywe au ule mchanganyiko huo bila ya kuchanganya na maji.