Habari wakuu,
Niende moja kwa moja kwenye mada.
Nilipata shida miezi miwili iliyopita nilikuwa nasikia maumivu kwenye tumbo upande wa kulia kwa chini. Baada ya kwenda kupima niligundulika nina kidonda kwenye utumbo mkubwa Doctor alisema ugonjwa nilio nao unaitwa chlons disease. Nilipewa dawa nikatumia mwezi 1 nikamaliza dose kwa sasa nina week 2 toka nimalize dose lakini naona bado shida ipo kwa sababu bado napata maumivu kama mwanzoni.
Naomba ushauri wa kitaalam ni aina gani ya dosage itanifaa.
Naomba mnisaidie napata shida sana.
Asanteni.
Pole sana,
Unapozungumzia Crohn's disease haushughuliki na vidonda vya tumbo(Peptic Ulcers disease). Huu ni ugonjwa ambao uko kweye kundi la Inflammatory bowel syndrome. Hapa kuna magonjwa mawili: Crohn's na Ulcerative colitis. Magonjwa haya yana asili ya kurithi kwenye uzao.
Suala la kwanza la msingi ni kuhakiki tatizo la msingi/ugonjwa husika. Suala la pili ni kuelewa kuwa kama ni kweli una ugonjwa husika hauponi moja kwa moja ila utaweza kuweka dalili nje ya mfumo wa maisha yako.
Hakuna dawa moja yenye kufanya kazi kwa uhakika kwa wagonjwa wote. Dawa zipo ila huweza kuwakubali au kutokukubali mgonjwa mmoja na mwingine kwenda vyema na dawa aina fulani. Pia, kiasi cha tatizo huweza kuwa msingi wa kurejea vyema mapema. Jambo jema ni mgonjwa kuendelea na tiba ukimjulisha mtoa tiba maendeleo yako.
Tiba halisi inahusisha:
1: kushirikiana kwa karibu na daktari bingwa wa njia ya chakula.
2: Tumia dawa kwa kadri ulivyoelekezwa.
3: Zingatia aina ya vyakula ambavyo ukivitumia huleta shida kwenye tumbo, mfamo: kuharisha, tumbo kujaa, maumivu ya tumbo au choo kuwa kigumu.
4: Kufanya vipimo vya ufatiliaji wa mwenendo wa mwili wako, kwani huu ni ugonjwa unaoathiri mifumo mingine ya mwili pia.
NB: Ukizingatia 1,2 na 3 hapo juu utaweza kuishi vyema na tatizo husika.