wasaalam
kama kichwa cha habari kinavyojieleza
niliajiriwa serikali kuu mapema mwaka huu baada ya kusota kwa zaidi ya miaka miwili mtaani katika masharti ya kudumu na mafao ya uzeeni na probation period ya mwaka mmoja
baada ya miezi 7 tangu nianze kazi niliandikiwa barua ya kuachishwa kazi huku sababu iliyoelezwa ni missconduct
lakini kinachoshangaza ni kwamba tangu nianze kazi sikuwahi kuitwa kuhusu shauri lolote linalohusiana na missconduct kati yangu na msimamizi wa kituo cha kazi na nilikuwa nafanya kazi kama kawaida na kiukweli kabisa sikuwahi kufanya kosa lolote lile
kubwa zaidi nimeandikiwa barua nikiwa katika mapumziko baada ya kumaliza matibabu ambapo yaliyotokana na mimi kupata ajali ya bodaboda wakati natoka kazini ambapo dereva aliingia mtaron na kunisababishia kuvunjika mkono wa kulia ambapo nilipewa rufaa na kuletwa dsm kwa ajili ya matibabu
baada ya kufanyiwa upasuaji nilirudi kazin (mkoani) na kuwasilisha ed niliypewa na daktari inayonitaka nipumzike kwa wiiki 4 kuuguza mkono
nimeandikiwa barua ya kuachishwa kazi sku mbili baada ya kuanza mapumziko mara baada ya kurud kutoka kwenye matibabu
ieleweke kuwa mwajiri wangu yupo dsm na kule mkoani yupo msimamizi
pia ieleweke nilipewa ruhusa kama kawaida na kupewa fedha za kunisaidia nauli na kujikimu na msimamizi wangu
nimejaribu kufatilia kupata ufafanuzi nijue makosa niliyofanya lakini mwajiri haoneshi ushirikiano wowote
je, nichukue hatua gani???
Je, kuna uwezekano wa kurejeshwa kazini?
Naombeni msaada na kama kuna mwanasheria aliye tayari kunisaidia tafadhali, naomba anichek kwa inbox
nb: Sijawahi kuitwa kuhsu shauri lolote la maadili au utendajj kazi. Kwa lugha rahsi sjawahi kusikilizwa wala kujitetea
natanguliza shukrani n mbarikiwe