Msaada: Nimefikia hatua ya kunywa Pepsi 4 kwa siku, nifanyeje kuacha?

Msaada: Nimefikia hatua ya kunywa Pepsi 4 kwa siku, nifanyeje kuacha?

Habarini za mchana,
Wakuu Mimi huwa situmii pombe ni juice na soda tu...soda yangu pendwa ni Pepsi Kila siku huwa nakunywa Pepsi tena napenda ikiwa baridi saaana nilianza kunywa moja kwa siku ikaja mbili ikaja 3 now nakunywa nne kwa siku mbili mchana mbili usiku izo mbili nakunywa kwa mpigo ....nifanyeje kuacha....pia Mimi sio mpenz wa chai asubuhi Niko radhi Nile vitafunwa vikavu au na maji au soda ...na usiku siwez kulala bila kunywa maji baridi huaga nalala na jug LA maji pembeni ....nkinywa maji baridi akil hua inarelax nalala kwa haraka tofaut na nisipokunywa maji....nifanyeje
R.i.p in advance
 
Kama ulivyoanza kujenga tabia ya kuzinywa taratibu, tumia njia hiyo hiyo yakupunguza, kunywa moja kwa siku, then ifike mahali unywe moja kila baada ya siku 2 na hatimaye utaacha kabisa.

Vyema ukapanga ratiba ya kunywa maji nzuri ambayo itakufanya usiku ukilala usiamke hovyo hovyo kukojoa,

Jitahidi ulale masaa 8 mfululizo kuondoa stress na misongo ya mawazo inayokuchagiza kutafuta Pepsi ilipo ukidhani inakupunguzia stress kumbe inakuongezea maradhi.
 
Anza kupunguza. Kama hizo mbili za usiku unakunywa nyumbani usinunue kabisa. Fridge lako lijae maji. Na mchana kunywa moja tu. Jizoeshe kutembea na chupa ndogo ya maji uwe unakunywa badala ya Pepsi.
Tatizo friji nimejaza soda nkitaka kunywa naiweka kwenye freezer dk chache ipate ubarid nzuri ndo nakunywa inakua inanisisimua
 
Kama ulivyoanza kujenga tabia ya kuzinywa taratibu, tumia njia hiyo hiyo yakupunguza, kunywa moja kwa siku, then ifike mahali unywe moja kila baada ya siku 2 na hatimaye utaacha kabisa.

Vyema ukapanga ratiba ya kunywa maji nzuri ambayo itakufanya usiku ukilala usiamke hovyo hovyo kukojoa,

Jitahidi ulale masaa 8 mfululizo kuondoa stress na misongo ya mawazo inayokuchagiza kutafuta Pepsi ilipo ukidhani inakupunguzia stress kumbe inakuongezea maradhi.
Sawa
 
Habarini za mchana,

Wakuu mimi huwa situmii pombe, ni juice na soda tu na soda yangu pendwa ni Pepsi.

Kila siku huwa nakunywa Pepsi tena napenda ikiwa baridi sana. Nilianza kunywa moja kwa siku, ikaja mbili ikaja 3 now nakunywa nne kwa siku; mbili mchana na mbili usiku. Hizo mbili nakunywa kwa mpigo.

Nifanyeje ili kuacha? Pia Mimi sio mpenz wa chai asubuhi, niko radhi nile vitafunwa vikavu au na maji au soda, na usiku siwezi kulala bila kunywa maji baridi-huwa nalala na jug la maji pembeni.

Nikinywa maji baridi akili huwa inarelax, nalala kwa haraka tofaut na nisipokunywa maji. Nifanyeje?
Jiandae kwa diabetes mellitus.
 
Back
Top Bottom