Kuchelewa kuchanganya mara nyingi ni tatizo la engine yenyewe na si gearbox. Kwanza haishauriwi ku change oil ya gearbox na ili ku change inabidi gari iwe imetembea sana yan karibia km elf 60 huko google utaona hiki kitu na uki change nunua oil ile wanaita hydropress 68 nyeupe hivi . Angalia sana hao mafundi mchundo ndo wanaharibu magari
Ntakupa kisa changu , engine iliwahi nisumbua karibia miezi sita nimebadili sana oil, plug , coil n.k. Baadae nikaanza ku notice brake zinajishika zenyewe hasa nikitembea sana hapo fundi akasema tu change brake master, nika change ila baadae ikarudi. Siku nikaamua ku google nikapata majibu quora kwamba ni hose zinaweza kuwa na leakage, Mwisho nimekuja kutengeneza mwenyewe kwa issue ndogo tu horse ya engine kwenda kwenye brake booster ilikuwa ina leakage ambayo kwa macho huwezi ona ila engine ilikuwa haivuti vizuri toka kwenye master(iliungwa somewhere ). Nikatafuta hose nyingine kipande kwa buku 5 hapo temeke hata si cha hii gari nikakiweka jumapili moja , kuwasha gari imetulia sana na ina compression ya kutosha na ina change gear on time. Mwanzo wakati engine haiwaki vizuri na ina miss miss gear box pia ilikuwa haichange vizuri mpaka kuisikilizia. Nimekuja ku confirm mafundi ndo wanaharibu magari na wengi shule hawataki kwenda.
Kwenye haya matatizo ya magari always start with simple things kabla ya kukimbilia kwenye mambo ya gharama ambayo ndo huwa majibu ya mafundi muda wote.
Kuna jamaa yangu aliambiwa anunue engine mpya baada ya fundi mmoja ku husle siku mbili engine inagoma ku start, kama bahati nilienda kwake nikawakuta mafundi sasa katika kutizama huku na huko tukakuta kwenye camshaft kuna jino linevunjika, huwezi amini ilinunuliwa cam nyingine kwa elf 70 na tatizo likaishia hapo hapo. Kuna Mwingine alishawahi kupeleka hadi engineering tatizo la kuchemsha, kumbe ilikuwa water pump na ilikuja julikana baada ya kutumia ile leakage stopper ya rejeta, ile dawa inauzwa elf sita ila baada ya kuweka kesho yake engine ikawa inapiga kelele sana kuja kuchek kumbe ni water pump ya elf 30 tu na tatizo la kuchemsha hajawahi kulisikia tangia siku hiyo.