Msaada: Nimepitiliza muda wa kujifungua

Msaada: Nimepitiliza muda wa kujifungua

lizdjoy

Member
Joined
Jul 3, 2015
Posts
27
Reaction score
5
Habari,

Mimi ni mwanamke nina umri wa miaka 28 na ni mjamzito. Tatizo linalonikosesha raha ni kuwa nimepitiliza tarehe yangu ya kujifungua na hata zile wiki mbili za nyongeza zimepita.

Nimeenda hospitali jana kuonana na doctor akasema nisubiri hadi tarehe 9 then kama bado niende wakajue option gani wafanye.

Msaada ninaomba, hakuna dawa inayoweza kunipa uchungu na nikajifungua kawaida, na nini aswa tatizo la kutopata uchungu kwa wakati?
 
Pole ndugu yangu ngojea madocta waje kukushauri na Mie nijifunze
 
fwata ushauri wa daktari, hizo dawa unazosema zipo lakini hujapewa labda kuna sababu maalumu dokta ameiona.

kima ulienda kwenye kizahanati tafuta hospitali ya maana unakoweza kutana na wataalamu.

pia ujuwe ikionekana mtoto hajakaa vizuri unaweza kulazimika kufanyiwa operation...
 
Nilienda hospital kubwa samahani mtoto kukaa vibaya inachangia kukosa uchungu?
 
Msikilize daktari mimba kupitiliza sio ugonjwa huwa inatokea mara nyingi usiangaike na dawa unaweza ukatundikiwa maji ya uchungu na usizae so msikilize daktari kwanza ila option itayofuata ni kupasuliwa
 
usichukue option ya kupasuliwa dada kama huna health problem yoyote wala mtoto.
ninao wengi katika familia yangu wanapitiliza siku lakini cha muhimu huwa nawashajihisha kufanya mazoezi.
jengine kanunue uwatu (funnel greek seed) chemsha asubuhi na usiku unywe au roweka kwenye maji yamoto baada ya masaa kunywa.
Lakini hakikisha sukari yako sio ya chini maana hii hushusha sukari.
unaweza ku google ukaona faida ya uwatu.
watu hutumia na huwasaiidia jaribu dada.
 
Nilienda hospital kubwa samahani mtoto kukaa vibaya inachangia kukosa uchungu?

ya kwa baadhi ya positions, ila vitu vingine ni hormone ya kusaidia nyonga kutanuka na nyingine nyingi. Sasa dokta aliyekupima ndio anajua nini hasa tatizo.
 
Kawaida unaeza kuwahi week 2 au ukachelewa week 2 kwenye ile tatehe yako ila zikipita zile week 2 wahi hospital maana placenta inakua tayari imechoka na uterus pia vile vile so mtoto anaeza akafia tumboni.
 
Nilienda hospital kubwa samahani mtoto kukaa vibaya inachangia kukosa uchungu?

ya kwa baadhi ya positions, ila vitu vingine ni hormone ya kusaidia nyonga kutanuka na nyingine nyingi. Sasa dokta aliyekupima ndio anajua nini hasa tatizo.

na kwa kuongezea kama unaweza basi fanya mazoezi ya kutembea ukiwa na mwangalizi wako. Pia fanya "breast massage" au nipple stimulation, hii husaidia oxytocin hormone ifanye kazi yake(hii ndio huleta uchungu).
Pia unaweza pewa drip ya mbadala wa oxytocin mfano Syntocinon hii pia huongeza uchungu, ila ni mpaka doctor aone ulazima wa wewe kupewa hiyo. Kuna njia pia ya kupunguza amnioc fluid ili uterus i-contract uchungu uanze lakini hizi zinahitaji mtu mtaalamu ili mtoto asidhurike.
 
Habari,

Mimi ni mwanamke nina umri wa miaka 28 na ni mjamzito. Tatizo linalonikosesha raha ni kuwa nimepitiliza tarehe yangu ya kujifungua na hata zile wiki mbili za nyongeza zimepita.

Nimeenda hospitali jana kuonana na doctor akasema nisubiri hadi tarehe 9 then kama bado niende wakajue option gani wafanye.

Msaada ninaomba, hakuna dawa inayoweza kunipa uchungu na nikajifungua kawaida, na nini aswa tatizo la kutopata uchungu kwa wakati?
Dawa ya kuweza kukufanya upate kuzaa ninayo ukiweza nitafute kwa kubonyeza hapa.Mawasiliano
 
Habari,

Mimi ni mwanamke nina umri wa miaka 28 na ni mjamzito. Tatizo linalonikosesha raha ni kuwa nimepitiliza tarehe yangu ya kujifungua na hata zile wiki mbili za nyongeza zimepita.

Nimeenda hospitali jana kuonana na doctor akasema nisubiri hadi tarehe 9 then kama bado niende wakajue option gani wafanye.

Msaada ninaomba, hakuna dawa inayoweza kunipa uchungu na nikajifungua kawaida, na nini aswa tatizo la kutopata uchungu kwa wakati?

Nitajie tarehe yako ya mwisho kupata hedhi(Last Normal Menstrual Period)
 
Dr kasema usubiri hadi tarehe 9, wewe unataka uambiwe dawa ya uchungu, sasa ya daktari hayana maana tena, kupitiliza siku hasa hizo wiki mbili ktk kujifungua ni jambo la kawaida, wala hupaswi kuwa na hofu. niliwahi kuexperience hali hiyo kwa ujauzito wangu wa kwanza, nilipitiliza wiki mbili, nikaenda hosp dr akanipa tarehe ya kurudi ila kama nitakuwa bado waamue vinginevyo, but niliumwa uchungu kabla ya hiyo tarehe niliyopewa hospital na nilijifungua salama kabisa kwa njia ya kawaida, so fuata maagizo ya daktari lizdjoy
 
Last edited by a moderator:

Ni kweli uyasemayo dada ila nazidi pata hofu coz tarehe yenyewe ni leo na bado sina dalili zozote zile
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom