Msaada- Nimetapeliwa Kariakoo- Vitasa 100 feki za milango sawa na TSH 2.3million

Msaada- Nimetapeliwa Kariakoo- Vitasa 100 feki za milango sawa na TSH 2.3million

Fata blog na waandikie, au unaweza pia kutumia google kuwatafuta au unaweza kwenda BRELA ukapata habari zao zote kwani wamejiandikisha rasmi kama wanavyoeleza kwenye blog yao, kwani kwa sasa na wewe umeshawajuwa kuwa wapo.

Usingojee kila kitu kufanyiwa.

Niko wilaya ya Mlele.
 
nenda tume ya ushindani ofisi zao zipo ubungo siyo kweli bidhaa ikishauzwa hairudishwi sheria zipo na zinakulinda huyo mtu atarudisha gharama zako zote na vifaa vyake vitaharibiwa pia atapigwa faini sheria zipo za kuwalinda walaji ila wengi wetu hawazitambui
 
Naona Kama kuna kosa lingine Hapa! Hiyo lisiti Sio ya EFD mashine, usisahau kumpambanisha na TRA pia!
 
Mimi ni dalali mzuri sana nina ofisi na nimesajili ofisi yangu nafanya udalali profeaaional ukiwa unahitaji mzigo kkoo pls utuconsult wadau kama sisi kwa msaada zaidi wa kupata bidhaa nzuri tena kwa contrct kabisa.
 
Wapeleke tbs ugungue kesi mahakamani kama ni muhindi anaweza kukupa viyasa imara....
 
Nenda ubungo plazza kaulize FCC,fair competition commission,ina fanya kazi na ku mtetea mraji,mi niliuziwa flash feki mwaka 2012,nilienda tbs,tbs wakaniambia niende hapo,nilipoenda wakanipa barua niwapeleke walioniuzia flash fake ikisema wanipe hela au wanibadilishie,wakanikatalia kurudisha hela hata kubadilisha,nikaenda kutoa taarifa tena,ndipo nikaondoka nao kutumia gali lao hadi kariaokoo,kufika pale wakaawaambia either wanipe hela yangu au watoe faini milioni mbili,wale jamaa wakaamua kunirudishia hela yangu yote.
kama upo serious fanya hivyo,wewe nenda pale ubungo plaza kaulizie ofisi za fair competiton,watakusaidia,walikuwa hawanijui,wala siwajui,ila walinisaidia kupata haki yangu.

Upo sahihi niliweza kurudisha simu fake kwa msaada wao.!!
 
Hata hao FCC naona wanafanya kazi kisaniitu! Hakuna hatua za kisheria dhidi ya mwenye duka?...maana kumwacha atazidi kuliza watu!! Na TBS nao waliikana kazi yao,Tanzania kweli Tambarare.
 
Mimi ni dalali mzuri sana nina ofisi na nimesajili ofisi yangu nafanya udalali profeaaional ukiwa unahitaji mzigo kkoo pls utuconsult wadau kama sisi kwa msaada zaidi wa kupata bidhaa nzuri tena kwa contrct kabisa.

nyie ndio matapeli kuliko
 
Waweza pata vitasa Na kupewa guarantee pale assy abloy mwenge kituo cha ITV ni maagent was Union
 
Mtafute mwanasheria akusaidie katika hili, hyo hela sio ya kitoto
 
Uelewa wa consumer protection hapa kwetu upo chini sana sana. Wanasheria nao sio wabunifu kupanua wigo wa aina za mashauri wanayochukua, hawatoi ushaurikwa wananchi kuwa wana haki kama hawapati huduma muafaka kwa hela wanayolipa. Mifano michache ni kama insurance claims ukiangalia kwa kina utakuta wanaolipwa ni wachache na hao wanaolipwa kiasi ni kidogo sana kulingana na maumivu wanayoyapata.

. Something has to be done.

Sio tu Consumer protection hata haki ya mteja tu hakuna na ndo kauli za ki-pambaf km hizo "eti mali ikinunuliwa hairudishwi".Vipi bongo siwezi kuuza bidhaa mf km unga alafu nika-compare bei yangu na muuzaji mwingine kwa bidhaa hiyo hiyo hairuhusiwi hata km huyo mwengine anapiga watu bei mbaya ?Huko kwenye bima ndo uozo wacha tu mtu akikwaruza ki-mkweche chako salama malizaneni huko huko kitaa bima itachuka 5yrs kulipa claim ya Tsh15000.....
 
Back
Top Bottom