Msaada :Nimetumia dawa na kufanya vipimo mara kadhaa lakini vipele haviponi

Msaada :Nimetumia dawa na kufanya vipimo mara kadhaa lakini vipele haviponi

A.J

Senior Member
Joined
Jun 9, 2015
Posts
140
Reaction score
147
IMG_20180221_155447.jpg

Wakuu nimekuwa na wakati mgumu sana, naombeni ushauri miezi kama mitano hapo nyuma kuna kama vipele vilinitoka kimoja kimoja nikachukulia poa tuu nikaenda navyo vikaisha ila vikaacha makovo.

Baadae vikarudi tena nikawasiliana na Dr flan hivi akanambia ni staphylococ bacteria, nikatumia Ampicox dozi zikakataa nikatumia tena dozi ya pili zikakataa nikapima HIV hakuna pia, nikaamua niende hosptali nikaambiwa nifanye blood culture.

Majib yakaja sina bacteria kwenye damu, kuna jamaa akanambia nitumie pen v, zikaisha hakuna matumaini nikamtafuta tena doctor mwengine akanambia nipime Full blood count na VDRL vipimo vyote vimetoka vipo sawa lakini bado ninasumbuliwa na hivi vipele.

Naombeni mwenye kujua dawa au nichukue tena kipimo gani anambie, au hata ushauri tuu nifanye nini?
 
Daaah aisee mkuu unahitaji uchunguzi wa kina zaidi lakini hili tatizo huwa linasababishwa na uwepo wa bacteria kwenye damu na pia HIV huwa na EARLY SYMPATOMS za namna hii but kama ni ya bacteria dozi ya AMPICLOX CAP 500 MG TDS ambayo hutumika FOR 5 DAYS ni antibiotic nzuri hupambana na hali hii na inaisha kabisa.
 
Daaah aisee mkuu unahitaji uchunguzi wa kina zaidi. Lakini hili tatizo huwa linasababishwa na uwepo wa bacteria kwenye damu..na pia HIV huwa na EARLY SYMPATOMS za namna hii.. but kama ni ya bacteria dozi ya AMPICLOX CAP 500 MG TDS ambayo hutumika FOR 5 DAYS ni antibiotic nzuri hupambana na hali hii na inaisha kabisa.
Yani bro nmepima HIV mara 2 kwa interval flan, nmekunywa Amplicox, Pen V, Azuma, Erythromycin, pia nimepina Blood culture ikaonekana sina bacteria kwenye damu, nimefanya pia kipimo cha Full Blood Picture cell zipo sawa mzee na pia nmechek VDRL sina gonjwa la ngono pia
 
Badilisha aina za vyakula na mafuta unayotumia hakika utapona kabisaaa
 
Yaani unaogopa ako kakipele kweli wabongo waoga sana , yaani ako mi ningekatumbua na ukucha tu afu ningesizi
 
Yaani unaogopa ako kakipele kweli wabongo waoga sana , yaani ako mi ningekatumbua na ukucha tu afu ningesizi
Mzee baba vimeanza kitambo na mapajani na mgongoni kuna makovu mengi mpk naogopa hata kumfata mwanamke, yani huwezi amini nimemuacha gal wang kisa hiki na nimevunja miadi kibao ya chumbani vinanivyimaa amani
 
Mkuu hapo dawa ni moja tu,MAZOEZI.Mi nilikuwa navyo hivyo mgongoni na mikononi lakini nilipoanza mazoezi kila siku 40mins vimepotea vyote
N.B:Hakikisha unatoka jasho sanaaaaa na kunywa maji ya kutosha
 
Back
Top Bottom