A.J
Senior Member
- Jun 9, 2015
- 140
- 147
Wakuu nimekuwa na wakati mgumu sana, naombeni ushauri miezi kama mitano hapo nyuma kuna kama vipele vilinitoka kimoja kimoja nikachukulia poa tuu nikaenda navyo vikaisha ila vikaacha makovo.
Baadae vikarudi tena nikawasiliana na Dr flan hivi akanambia ni staphylococ bacteria, nikatumia Ampicox dozi zikakataa nikatumia tena dozi ya pili zikakataa nikapima HIV hakuna pia, nikaamua niende hosptali nikaambiwa nifanye blood culture.
Majib yakaja sina bacteria kwenye damu, kuna jamaa akanambia nitumie pen v, zikaisha hakuna matumaini nikamtafuta tena doctor mwengine akanambia nipime Full blood count na VDRL vipimo vyote vimetoka vipo sawa lakini bado ninasumbuliwa na hivi vipele.
Naombeni mwenye kujua dawa au nichukue tena kipimo gani anambie, au hata ushauri tuu nifanye nini?