Msaada: Nimetupiwa kipande nateseka mwaka wa 3 sasa, nahitaji msaada

Nilichookoteza hapa ni kwamba mleta mada una mambo ya shiriki (ushirikina). Wengi wanasema umetupiwa kipande, kipande fyo fiki!!!.
Labda wale wa tiba asili walikuwa matapeli ( kwa kadiri unavyotafuta waganga wa kienyeji ndivyo tatizo linaongezeka, wachawi na waganga wa Jadi utofauti wao ni vilinge tu.
 
Sawa poinyi yako ni Ipi
 
Pole sana ndugu kwa masahibu,mimi si dokta lakini naiona nafasi ya kushauri jambo juu yako kwa kukuunganisha na dokta ili suala lako liingie maabara itumiayo macho ya rohoni.Kama mpaka sasa hujasaidiwa nitafute kwa 0620155494 jioni na kama sijapokea fululiza sitakuhesabu kama msumbufu kwani wewe wafaa kuwa rafiki.Wanaokukejeli hawajitambui na hivyo wasamehe bure
 
Hauwezi kuelewa ikiwa hujakutwa na situation, kwani wanaokwenda hospital hii na kubadili hospital msimamo wao unakuwa ni kutafuta nn

Hauwezi kuelewa ikiwa hujakutwa na situation, kwani wanaokwenda hospital hii na kubadili hospital msimamo wao unakuwa ni kutafuta nn?
Umeongelea hospital Mimi naongelea mambo ya kiimani elewa vizuri juu ya Connection iliyopo kati ya aliepata Tatizo na ufumbuzi wa Tatizo lenyewe.Tatizo alilonalo ni la Nguvu za kiimani na Imani inayompa misukosuko ni Imani ya Giza ambayo yeye anaiamini imemfikisha alipo So it's better kukimbilia katika Imani ya Kweli na kumrudia Mungu na siku zote Giza halijawhi kufukuza Giza bali mwanga hufukuza Giza na kuangaza kwa nuru
 
ushauri wangu
1)ni kweli kuna roho giza/nguvu za giza/mapepo/majini/vitendo vya kishirina au uchawi au ulozi au kutupiwa kipande,majini ,roho hizi za mauti asili yake ni kuzimu nguvu za giza zofuatilia maisha yako
lengo lake ni kuchinja,kuiba,kuharibu uharibifu zilikotoka ni madhabahu za giza kuzimu kiongozi wake ni shetani lucifer mawakala wake ndio hao wachawi,waganga wa kienyeji na majini mapepo.
2)njia uliyotumia ya kutafuta msaada kwa waganga wa kienyeji na kama utaitumia njia hiyo hiyo ya kuendelea kutafuta msaada kutatua tatizo hilo kwa kwenda kwa waganga wa kienyeji ni sawa na kuongeza tatizo,au kujipalia mkaa wa moto.Kwa sababu mganga wa kienyeji anatumia nguvu ya madhabahu ya kuzimu ya lucifer na wachawi madhabahu yao ni hiyo hiyo yani ni watoto wa baba mmoja,serikali moja,ni sawa na serikali ni sawa na kesi ya nyani unaipekeka kwa ngedere.Ufalme mmoja hawawezi wa shetani,pepo jini hawezi kumtoa jini mwenzake.(waganga wa kienyeji na wachawi ni ushirika mmoja chama moja)
3)SULUHISHO LA KUDUMU LA UKWELI
a/Ni kupitia jina la Yesu hakuna jina lingine tulilopewa wanadamu linaloweza kutuokoa na kufukuza hayo mapepo zaidi ya jina la YESU kwa sababu huyu Yesu ndio mwokozi wa ulimwengu.
b)tafuta kanisa lolote lenye nguvu ya Mungu na waombaji sio hao manabii wa uongo matapeli..nenda uombewe lakini inaanza na wewe mwenyewe kuomba..NAMNA YA KUOMBA
KWANZA...toba tubu dhambi ya kutegemea mwanadamu mganga na kuiendea miungu ya mganga mizimu majini ya mganga ,ungama omba msamaha wa dhambi omba Yesu akusamehe dhambi ya kuiomba miungu mizimu/majini ya mganga yakusaidie
omba toba usamehewe kupela sadaka kwa mganga zile vitu na mali pesa ulizompa mganga ni sadaka ulipeleka ambapo sadaka hizo zitatumika kukuangamiza kukuzamisha zaidi kwwnye matatizo zaidi.Kama kuna dawa ama vitu vya kuchimbia au vyovyote ambavyo mganga alikupa vitoe vichome moto,kama ulikunywa ulichanha chale,ulipaka,ulivaa,ulifukiza kama kuna vitu mganga alichukua kutoka kwako kama nywele,nyusi ,kucha mate n.k
Omba Yesu akurejeshee vyote vilivyoibwa kutoka kwako,na omba aviondoe vyote vilivyopandikizwa kwako vya giza
b)peleka sadaka kanisani kubwa zaidi ya zile ulizopeleka kwa mganga,ili kuimarisha madhabahu za Mungu wa kweli sasa ,
c)Omba YESU akusaidie akuokoe kwa imani,omba rehema,omba msaada,omba uponyaji kutoka kwa Yesu.
Dumu katika maombi sala,sadaka,ikiwemo kusaidia masikini pia ni sadaka
Amini kuwa Mungu yupo pamoja nawe anakusaidia na hakuna ubaya au madhara yoyote yatakayokupata USIOGOPE,kabla ya kulala sali,fanya kazi kwa bidii,samehe waliokukosea,okoka jiepushe na dhambi mana dhambi inafungua mlango wa mapepo kuendelea kukuandama
YESU NI DAWA,YESU NDIO MKOMBOZI WETU.
 
ni kweli kabisa waganga,wachawi,shetani na malaika zake majini,mapepo,mizimu n.k na mawakala wake ni serikali moja ni chama kimoja kitu kimoja sema vitengo tofauti.Lakini madhabahu yao na kiongozi wao ni mmoja ni shetani lucifer-mfalme wa nguvu za giza.
ambaye ufalme wa nguvu za giza unazidiwa nguvu na ufalme wa nuru(YESU KRISTI NDIO NURU)
Maisha yana pande mbili GIZA na NURU,kama haupo kwenye NURU upo kwenye GIZA.kwa MUNGU ama kwa shetani.Ila ukiwa NURUNI utashinda Giza ,mana nuru hufukuza giza.Nuru ina nguvu kuliko giza,dawa ya shetani ni Yesu
 
nimekuwa nikiota ndoto za ajabu ajabu na za kutisha mara nyingi, mara uote unazikwa mara unabeba jeneza nk.
Shida iko hapo
 
Japo wengine hufikiria kujiua ili kuondokana na hizi shida za dunia lakini mimi NASEMA KAMA MUNGU ALIRUHUSU MATATIZO HAYA KUNIPATA BASI ASIPORUHUSU KUPATA MSAADA WA KUPONA KABISA BASI NITAISHI HIVIHIVI, SIWEZI KUJIUAπŸ’ͺπŸΏπŸ”¨
 
nimekuwa nikiota ndoto za ajabu ajabu na za kutisha mara nyingi, mara uote unazikwa mara unabeba jeneza nk.
Shida iko hapo
Kuna mshenzi anakuchezea. Yalinikuta, naota nimelala ni nyoka mara nahamisha majeneza.

Kwa sasa naota nimeokota hela, na mambo kama nagonga demu. Hizi ni ndoto safi.
 
Mwanzoni nilidhani ni tatizo la customer care lakini nilivyoendelea kusoma ninaungana nawe kuwa KIPANDE kinakupiga. Ushauri wangu unaweza usiwe na maana sana kwani sitalichambua tatizo bali nitapendekeza yafuatayo:
  1. Kutupiwa KIPANDE ni kazi ya ibilisi na jamii ya walozi na waaguzi wanaotumia doctrine yake hawatakusaidia bali kukuumiza zaidi
  2. Unapomkimbilia Mungu usiende na idea pekee ya kunasuliwa na KIPANDE bali kuondolewa dhambi hususan maagano ya kimila uliyoingizwa kwa kujua ama kutokujua. Zaburi 103:3 Akusamehe maovu yako yote, Akuponya magonjwa yako yote.
  3. Simamia jambo lako, pokea ushauri, chuja ushauri kisha pambana
 
Mtaa unaoishi una makabila ya pwani na watu wa Kusini kwa wingi nn?
 
Japo wengine hufikiria kujiua ili kuondokana na hizi shida za dunia lakini mimi NASEMA KAMA MUNGU ALIRUHUSU MATATIZO HAYA KUNIPATA BASI ASIPORUHUSU KUPATA MSAADA WA KUPONA KABISA BASI NITAISHI HIVIHIVI, SIWEZI KUJIUAπŸ’ͺπŸΏπŸ”¨
Ni kweli na kwa sasa hali ni mbaya zaidi miguu nayo imeanza kunisumbua inawaka.moto na kujaa kiasi kwamba kazi unafanya kwa shida sana.
 
Ni map
Kuna mshenzi anakuchezea. Yalinikuta, naota nimelala ni nyoka mara nahamisha majeneza.

Kwa sasa naota nimeokota hela, na mambo kama nagonga demu. Hizi ni ndoto saf

Kuna mshenzi anakuchezea. Yalinikuta, naota nimelala ni nyoka mara nahamisha majeneza.

Kwa sasa naota nimeokota hela, na mambo kama nagonga demu. Hizi ni ndoto safi.
Ndo mapito ya dunia kaka
 
Asante kwa ushauri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…