Wadau habari!nimekuja tena jamvini hapa kuomba ushauri wenu juu ya kujikwamua kiuchumi!nina kimtaji cha shilingi million mbili,bado sijapata wazo la uhakika ni kitu gani hasa nifanye ili niweze kujikwamua kiuchumi na kamtaji kangu hako kasije kuishia gizani!naombeni ushauri wenu wandugu!
Wadau habari!nimekuja tena jamvini hapa kuomba ushauri wenu juu ya kujikwamua kiuchumi!nina kimtaji cha shilingi million mbili,bado sijapata wazo la uhakika ni kitu gani hasa nifanye ili niweze kujikwamua kiuchumi na kamtaji kangu hako kasije kuishia gizani!naombeni ushauri wenu wandugu!
Wadau habari!nimekuja tena jamvini hapa kuomba ushauri wenu juu ya kujikwamua kiuchumi!nina kimtaji cha shilingi million mbili,bado sijapata wazo la uhakika ni kitu gani hasa nifanye ili niweze kujikwamua kiuchumi na kamtaji kangu hako kasije kuishia gizani!naombeni ushauri wenu wandugu!
mkuu huu ushauri wako siuamini!!!ulimwengu wa sasa ndo maana tuna business planners wewe unadhani kazi zao ni nini!!mdau hajakosea kuomba msaada hapa!Mkuu unaishi Mwezini? Make kama unaishi mtaani si dhani kama unakosa kuona Furusa, The Best Business Idea ni ya kutoka kwako wewe mwenyewe, 95% ya Entrepreners hugenerate Idea wao wenyewe,
Huwezi pata wazo kwa kutarajia watu wakupigie Lamuri humu ndani, ni wewe mwenyewe kustragle, na mara Nyingi mafanikio ya biashara hubwebwa na wazo la biashara, wazo la biashara huchua % kubwa sana ya biashara kufanikiwa,
So unahitaji kuumiza kichwa, kuna miongozo humu ya Jinsi ya Kutafuta Idea tatizo mtu anataka bado asamaraiziwe,
SO TRY KUTAFUTA YOUR OWN BEST AND SOUND BUSINESS IDEA
Mkuu kwanza nakupongeza kuja hapa jamvini na kuomba ushauri!kwa kweli mimi uwa naumizwa sana na vijana wa Tanzania wapatapo mtaji hata kidogo kukimbilia biashara za mijini kama stationaries,salon,boutique,duka nk ili hali wakikipa kisogo kilimo ili hali ndio utajiri mkubwa kwa sasa!inaumiza zaidi napo ona jirani zetu toka Kenya wanakuja hapa na kukaa vijijini kwa vimitaji vyao vidogo tu na kuweza kuwarubuni kwa visenti vichache wazawa wa eneo husika,na kuweza kufaidika na ardhi yetu na hata nguvu kazi zetu,huku sisi tukikaa pembeni na kubaki kuwasifia tu,"wakenya bwana sio mchezo"...hii kwa kweli inauma sana!vijana wa Kitanzania lazima tuchange mindset zetu,Wakenya wanakuja kulima mahindi,bustani,mpunga n.k kwenye ardhi yetu,wanatumia nguvu kazi yetu na hawauzi hizo bidhaa nchini mwetu,wanapeleka kuuza kwao na nchi nyingine,sisi tunabaki kurubuniwa na visenti vichache na kuendelea kua maskini!Wakenya wametushinda ninh sisi mpaka wao waweze na sisi tubaki kua walalamikaji?mkuu usihangaike kununua bodaboda,kuanzisha stationary wala duka,kwa ushauri wangu mimi wewe wekeza hela yako kwenye udongo,hela hiyo inatosha kulima mpunga,bustani etc,sikushauri mahindi maana hayo umechelewa kwa sasa na kuna changamoto nyingi sana!tafuta maeneo yenye mabonde,piga mpunga wako,piga bustani kama nyanya,hoho,vitunguu,carrot au hata ngogwe na ufanye kitaalamu utakuja kuniambia baada ya miezi sita tu nini matokeo yake!ila kama unapenda kung'ang'ania kukaa mjini kwa kua wewe ni graduate na utakuja kuajiriwa kama zilivyo fikra hasi za sisi vijana wengi wa Kitanzania,basi fanya hayo ya boda boda,mpesa,duka e.t.c!huo ndio ushauri wangu mkuu,hii mitandao ya kijamii tuitumie in a positive way zaidi,tuangalie fursa na mahitaji ya soko kimataifa,kuzalisha vitu kwa ubora stahiki n.k lazima tutafanikiwa tu,ilo ndilo wanalotushinda Wakenya,wepesi kufikiri na kutenda kuliko propaganda,ni wathubutu,na wana uwezo wa kuishi popote na kufanya kazi yoyote bila kujali ana elimu gani..nchi yetu bado mbichi na ina fursa lukuki
Mkuu umenena kwa kuongezea tu kama yupo mjini aende kijijini akawekeza pesa nyingi sana hiyo mjini kupata ardhi ni shida lakini kijijini unakodi ardhi kwa Tsh. 20,000/= kwa ekari moja kulima ni Tsh.50,000/= kwa eka moja mbolea ni Tsh. 60,000/= kwa mfuko akiwekeza sehemu za umwagiliaji hii pesa ndani ya mwaka itazaa mara dufu, maana atapiga tikiti maji likikomaa anatoa anapiga hoho pembeni huku anapiga nyanya chungu kule anapiga kitunguu yaani fursa kibao.
Nashukuru sana kwa kufafanua zaidi mkuu,vijijini kuna fursa sana tena sana,kilimo hasa cha umuagiliaji hakiongopi mkuu,ila wengi ya waliokua wakifanya kilimo walikua wanafanya ili mradi tu,ukosefu wa elimu ulikua unawagharimu!ila kwa sisi angalau tulio futa ujinga,kujua kusoma na kuandika,kupata exposure za nchi tofauti tofauti tujitahidi kutumia ardhi yetu yenye rutuba tele kujikomboa kimaisha na kuikomboa jamihi inayotuzunguka,uzuri wa kilimo ni kua soko lake ni kila pembe ya dunia na hitaji lake ni la kila siku!inategemea wewe mwenyewe umelenga nini!Watanzania ni wazito kuthubutu,tumepungukiwa marengo ya dhati,hatupendi kujituma ila tunapenda short cut,na la mwisho tunapenda sana anasa kuliko tunachoingiza!me siamini kama boda boda au salon zitamfanya mtu awe na ndoto za kuja kufanikiwa!kilimo na ufugaji ndio mpango mzima,unalima hata ufugaji wake ni rahisi sana!tutumie ardhi za mikoa yenye rutuba kama Mbeya,Shinyanga,Iringa na Morogoro tuweze kujikomboa na kufikia malengo yetu!uamuzi ni wako ndugu Nyamburi maana hela rafiki yake matatizo,bora uamue haraka,ukiendelea kukaa nayo bila kuamua!mwisho wa siku hela itakata na haujafanya kitu
Kweli mkuu kwa mfano mimi nimejiwekea mkakati kila mwaka nataka niwe nanua ardhi eka 10 ambayo kwa kule kijijini wanauza Tsh. 100,000/= kwa hiyo kwa ekari 10 sawa na Milioni moja napanda miti na mche mmoja ni tsh. 100/= ghalama ya kupanda kwa kutwa kibarua ni tsh.5000/= na hii miti nitavuna baada ya miaka 10-15 ijayo huu ni mkakati wa muda mrefu, mkakati wa muda mfupi ni kuangalia mazao yanayo komaa kwa kipindi cha miezi 3-5
sijui watanzania tumerogwa?!! mimi hata sijui yaani huku mjini tunakupenda kuliko kiasi wakati kiukweli hakutusaidii. mimi naiona hiyo na nimeshajaribu kwenye kilimo lakini mapungufu ninayoyaona wengi wetu hatuwekezi kwa kujiamini yani tunaingia kwa kujaribu.
hivyo hebu tuingie vizuri tutaona faida yake kwenye kilimo.
binafsi nimelima na mwezi watisa nategemea kupata mavuno yangu ya kwanza ya uhakika baada ya kuaangaika na shamba kwa miaka 3
Ila hapo yeye amelenga kwenye business idea ambayo kimsingi unatakiwa uanze kuwa nayo mhusikamkuu huu ushauri wako siuamini!!!ulimwengu wa sasa ndo maana tuna business planners wewe unadhani kazi zao ni nini!!mdau hajakosea kuomba msaada hapa!
Mkuu wewe una mtazamo kama wangu kabisa,na uzuri wa jamiiforums ndio huu,unapotoa wazo au kuomba ushauri unapata darasa la kutosha na hata wengine nao wanafaidika pia!vijijini ardhi ni rahisi sana,hasa ukishajiandikisha kwenye serikali za vijiji!kwa watu wenye mitazamo ya mbali wengi wanakimbilia kuwekeza kwenye ardhi hasa vijijini!mkuu mwenyewe nina wazo ilo la kua na heka za kutosha na nipande miti kama mkakati wa muda mrefu,na target yangu ilikua ni mitiki,ila naona miti hii kama ina changamoto nyingi kidogo,kwa hiyo nilichopanga,niendelee na kilimo cha kawaida,na nianze kupanda miti ya kawaida pia,lakini within 5 years niwe nimeanza kupanda na miteak pia!je mkuu wewe umedhamiria kuanza na miti gani kama utakua na utaalamu wa kutosha?