Msaada: Nina mtaji wa 2m/= nifanye biashara gani

Nyamburi

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2011
Posts
306
Reaction score
36
Wadau habari!nimekuja tena jamvini hapa kuomba ushauri wenu juu ya kujikwamua kiuchumi!nina kimtaji cha shilingi million mbili,bado sijapata wazo la uhakika ni kitu gani hasa nifanye ili niweze kujikwamua kiuchumi na kamtaji kangu hako kasije kuishia gizani!naombeni ushauri wenu wandugu!
 
Mkuu kwanza nakupongeza kuja hapa jamvini na kuomba ushauri!kwa kweli mimi uwa naumizwa sana na vijana wa Tanzania wapatapo mtaji hata kidogo kukimbilia biashara za mijini kama stationaries,salon,boutique,duka nk ili hali wakikipa kisogo kilimo ili hali ndio utajiri mkubwa kwa sasa!inaumiza zaidi napo ona jirani zetu toka Kenya wanakuja hapa na kukaa vijijini kwa vimitaji vyao vidogo tu na kuweza kuwarubuni kwa visenti vichache wazawa wa eneo husika,na kuweza kufaidika na ardhi yetu na hata nguvu kazi zetu,huku sisi tukikaa pembeni na kubaki kuwasifia tu,"wakenya bwana sio mchezo"...hii kwa kweli inauma sana!vijana wa Kitanzania lazima tuchange mindset zetu,Wakenya wanakuja kulima mahindi,bustani,mpunga n.k kwenye ardhi yetu,wanatumia nguvu kazi yetu na hawauzi hizo bidhaa nchini mwetu,wanapeleka kuuza kwao na nchi nyingine,sisi tunabaki kurubuniwa na visenti vichache na kuendelea kua maskini!Wakenya wametushinda ninh sisi mpaka wao waweze na sisi tubaki kua walalamikaji?mkuu usihangaike kununua bodaboda,kuanzisha stationary wala duka,kwa ushauri wangu mimi wewe wekeza hela yako kwenye udongo,hela hiyo inatosha kulima mpunga,bustani etc,sikushauri mahindi maana hayo umechelewa kwa sasa na kuna changamoto nyingi sana!tafuta maeneo yenye mabonde,piga mpunga wako,piga bustani kama nyanya,hoho,vitunguu,carrot au hata ngogwe na ufanye kitaalamu utakuja kuniambia baada ya miezi sita tu nini matokeo yake!ila kama unapenda kung'ang'ania kukaa mjini kwa kua wewe ni graduate na utakuja kuajiriwa kama zilivyo fikra hasi za sisi vijana wengi wa Kitanzania,basi fanya hayo ya boda boda,mpesa,duka e.t.c!huo ndio ushauri wangu mkuu,hii mitandao ya kijamii tuitumie in a positive way zaidi,tuangalie fursa na mahitaji ya soko kimataifa,kuzalisha vitu kwa ubora stahiki n.k lazima tutafanikiwa tu,ilo ndilo wanalotushinda Wakenya,wepesi kufikiri na kutenda kuliko propaganda,ni wathubutu,na wana uwezo wa kuishi popote na kufanya kazi yoyote bila kujali ana elimu gani..nchi yetu bado mbichi na ina fursa lukuki
 
Na kwa kuanzia tu,unaweza kuomba ushauri kwa mkuu mmoja humu jamvini anaita Kubota huyu yuko deep sana anaweza kukupa ushauri wenye kujenga
 
Wadau habari!nimekuja tena jamvini hapa kuomba ushauri wenu juu ya kujikwamua kiuchumi!nina kimtaji cha shilingi million mbili,bado sijapata wazo la uhakika ni kitu gani hasa nifanye ili niweze kujikwamua kiuchumi na kamtaji kangu hako kasije kuishia gizani!naombeni ushauri wenu wandugu!

Mkuu unaishi Mwezini? Make kama unaishi mtaani si dhani kama unakosa kuona Furusa, The Best Business Idea ni ya kutoka kwako wewe mwenyewe, 95% ya Entrepreners hugenerate Idea wao wenyewe,

Huwezi pata wazo kwa kutarajia watu wakupigie Lamuri humu ndani, ni wewe mwenyewe kustragle, na mara Nyingi mafanikio ya biashara hubwebwa na wazo la biashara, wazo la biashara huchua % kubwa sana ya biashara kufanikiwa,

So unahitaji kuumiza kichwa, kuna miongozo humu ya Jinsi ya Kutafuta Idea tatizo mtu anataka bado asamaraiziwe,

SO TRY KUTAFUTA YOUR OWN BEST AND SOUND BUSINESS IDEA
 
Kama unaishi maeneo ya vijijini unaweza jikwamua kwa kufuga mifugo kama nguruwe na kuku, vile vile pesa hiyo inaweza pia kukusaidia kulima shamba la mazao hata eka mbili vile vile pesa hiyo hiyo inaweza ikakusaidia kwa uwekezaji wa muda mrefu kama kupanda miti ya mbao.
 
Mkuu unaishi Mwezini? Make kama unaishi mtaani si dhani kama unakosa kuona Furusa, The Best Business Idea ni ya kutoka kwako wewe mwenyewe, 95% ya Entrepreners hugenerate Idea wao wenyewe,

Huwezi pata wazo kwa kutarajia watu wakupigie Lamuri humu ndani, ni wewe mwenyewe kustragle, na mara Nyingi mafanikio ya biashara hubwebwa na wazo la biashara, wazo la biashara huchua % kubwa sana ya biashara kufanikiwa,

So unahitaji kuumiza kichwa, kuna miongozo humu ya Jinsi ya Kutafuta Idea tatizo mtu anataka bado asamaraiziwe,

SO TRY KUTAFUTA YOUR OWN BEST AND SOUND BUSINESS IDEA
mkuu huu ushauri wako siuamini!!!ulimwengu wa sasa ndo maana tuna business planners wewe unadhani kazi zao ni nini!!mdau hajakosea kuomba msaada hapa!
 
Mkuu kwanza nakupongeza kuja hapa jamvini na kuomba ushauri!kwa kweli mimi uwa naumizwa sana na vijana wa Tanzania wapatapo mtaji hata kidogo kukimbilia biashara za mijini kama stationaries,salon,boutique,duka nk ili hali wakikipa kisogo kilimo ili hali ndio utajiri mkubwa kwa sasa!inaumiza zaidi napo ona jirani zetu toka Kenya wanakuja hapa na kukaa vijijini kwa vimitaji vyao vidogo tu na kuweza kuwarubuni kwa visenti vichache wazawa wa eneo husika,na kuweza kufaidika na ardhi yetu na hata nguvu kazi zetu,huku sisi tukikaa pembeni na kubaki kuwasifia tu,"wakenya bwana sio mchezo"...hii kwa kweli inauma sana!vijana wa Kitanzania lazima tuchange mindset zetu,Wakenya wanakuja kulima mahindi,bustani,mpunga n.k kwenye ardhi yetu,wanatumia nguvu kazi yetu na hawauzi hizo bidhaa nchini mwetu,wanapeleka kuuza kwao na nchi nyingine,sisi tunabaki kurubuniwa na visenti vichache na kuendelea kua maskini!Wakenya wametushinda ninh sisi mpaka wao waweze na sisi tubaki kua walalamikaji?mkuu usihangaike kununua bodaboda,kuanzisha stationary wala duka,kwa ushauri wangu mimi wewe wekeza hela yako kwenye udongo,hela hiyo inatosha kulima mpunga,bustani etc,sikushauri mahindi maana hayo umechelewa kwa sasa na kuna changamoto nyingi sana!tafuta maeneo yenye mabonde,piga mpunga wako,piga bustani kama nyanya,hoho,vitunguu,carrot au hata ngogwe na ufanye kitaalamu utakuja kuniambia baada ya miezi sita tu nini matokeo yake!ila kama unapenda kung'ang'ania kukaa mjini kwa kua wewe ni graduate na utakuja kuajiriwa kama zilivyo fikra hasi za sisi vijana wengi wa Kitanzania,basi fanya hayo ya boda boda,mpesa,duka e.t.c!huo ndio ushauri wangu mkuu,hii mitandao ya kijamii tuitumie in a positive way zaidi,tuangalie fursa na mahitaji ya soko kimataifa,kuzalisha vitu kwa ubora stahiki n.k lazima tutafanikiwa tu,ilo ndilo wanalotushinda Wakenya,wepesi kufikiri na kutenda kuliko propaganda,ni wathubutu,na wana uwezo wa kuishi popote na kufanya kazi yoyote bila kujali ana elimu gani..nchi yetu bado mbichi na ina fursa lukuki

Mkuu umenena kwa kuongezea tu kama yupo mjini aende kijijini akawekeza pesa nyingi sana hiyo mjini kupata ardhi ni shida lakini kijijini unakodi ardhi kwa Tsh. 20,000/= kwa ekari moja kulima ni Tsh.50,000/= kwa eka moja mbolea ni Tsh. 60,000/= kwa mfuko akiwekeza sehemu za umwagiliaji hii pesa ndani ya mwaka itazaa mara dufu, maana atapiga tikiti maji likikomaa anatoa anapiga hoho pembeni huku anapiga nyanya chungu kule anapiga kitunguu yaani fursa kibao.
 
Nashukuru sana kwa kufafanua zaidi mkuu,vijijini kuna fursa sana tena sana,kilimo hasa cha umuagiliaji hakiongopi mkuu,ila wengi ya waliokua wakifanya kilimo walikua wanafanya ili mradi tu,ukosefu wa elimu ulikua unawagharimu!ila kwa sisi angalau tulio futa ujinga,kujua kusoma na kuandika,kupata exposure za nchi tofauti tofauti tujitahidi kutumia ardhi yetu yenye rutuba tele kujikomboa kimaisha na kuikomboa jamihi inayotuzunguka,uzuri wa kilimo ni kua soko lake ni kila pembe ya dunia na hitaji lake ni la kila siku!inategemea wewe mwenyewe umelenga nini!Watanzania ni wazito kuthubutu,tumepungukiwa marengo ya dhati,hatupendi kujituma ila tunapenda short cut,na la mwisho tunapenda sana anasa kuliko tunachoingiza!me siamini kama boda boda au salon zitamfanya mtu awe na ndoto za kuja kufanikiwa!kilimo na ufugaji ndio mpango mzima,unalima hata ufugaji wake ni rahisi sana!tutumie ardhi za mikoa yenye rutuba kama Mbeya,Shinyanga,Iringa na Morogoro tuweze kujikomboa na kufikia malengo yetu!uamuzi ni wako ndugu Nyamburi maana hela rafiki yake matatizo,bora uamue haraka,ukiendelea kukaa nayo bila kuamua!mwisho wa siku hela itakata na haujafanya kitu
 
Kweli mkuu kwa mfano mimi nimejiwekea mkakati kila mwaka nataka niwe nanua ardhi eka 10 ambayo kwa kule kijijini wanauza Tsh. 100,000/= kwa hiyo kwa ekari 10 sawa na Milioni moja napanda miti na mche mmoja ni tsh. 100/= ghalama ya kupanda kwa kutwa kibarua ni tsh.5000/= na hii miti nitavuna baada ya miaka 10-15 ijayo huu ni mkakati wa muda mrefu, mkakati wa muda mfupi ni kuangalia mazao yanayo komaa kwa kipindi cha miezi 3-5
 
sijui watanzania tumerogwa?!! mimi hata sijui yaani huku mjini tunakupenda kuliko kiasi wakati kiukweli hakutusaidii. mimi naiona hiyo na nimeshajaribu kwenye kilimo lakini mapungufu ninayoyaona wengi wetu hatuwekezi kwa kujiamini yani tunaingia kwa kujaribu.
hivyo hebu tuingie vizuri tutaona faida yake kwenye kilimo.
binafsi nimelima na mwezi watisa nategemea kupata mavuno yangu ya kwanza ya uhakika baada ya kuaangaika na shamba kwa miaka 3
 
Mkuu wewe una mtazamo kama wangu kabisa,na uzuri wa jamiiforums ndio huu,unapotoa wazo au kuomba ushauri unapata darasa la kutosha na hata wengine nao wanafaidika pia!vijijini ardhi ni rahisi sana,hasa ukishajiandikisha kwenye serikali za vijiji!kwa watu wenye mitazamo ya mbali wengi wanakimbilia kuwekeza kwenye ardhi hasa vijijini!mkuu mwenyewe nina wazo ilo la kua na heka za kutosha na nipande miti kama mkakati wa muda mrefu,na target yangu ilikua ni mitiki,ila naona miti hii kama ina changamoto nyingi kidogo,kwa hiyo nilichopanga,niendelee na kilimo cha kawaida,na nianze kupanda miti ya kawaida pia,lakini within 5 years niwe nimeanza kupanda na miteak pia!je mkuu wewe umedhamiria kuanza na miti gani kama utakua na utaalamu wa kutosha?
 
Asante mkuu,ila kidogo kidogo tu mwishowe tutaelimika na kua na mtazamo chanya juu ya kilimo!shaka yangu ni kua tu,hawa Wakenya wasije wakawahi mihanya iliyopo na kua ndio washika dau wakubwa kwenye sekta hii,sisi tukaishia kua vibarua mashambani!mimi sioni hasa Watanzania kinachosababisha kushindwa kupeleka mazao yetu hata nchi jiranitu kama Sudan Kusini,ni kutojiamini,uoga au ukosefu wa maarifa??hakuna kitu kikubwa kilichoanza na kikubwa,kila kikubwa kilianza na kidogo,tujiamini Watanzania,tukiamini kilimo na tuwekeze huko!kilimo ni stress free kuliko biashara nyingi,i mean stress free in sense of market!
 
hata biashara ya maji na soda kwa bei ya jumla inafaa kila la kheri
 
mkuu huu ushauri wako siuamini!!!ulimwengu wa sasa ndo maana tuna business planners wewe unadhani kazi zao ni nini!!mdau hajakosea kuomba msaada hapa!
Ila hapo yeye amelenga kwenye business idea ambayo kimsingi unatakiwa uanze kuwa nayo mhusika
 
Mkuu Nyamburi "shambani,shambani,shambani,mazao booraa shambaaani" unaikumbuka hiyo mkuu?kama una mtaji wako huo ambao mimi nauona ni mkubwa sana,una malengo ya dhati,una uwezo wa kuishi vijijini,basi karibu shambani tutengeneze utajiri....asikudanganye mtu kuajiriwa ni kazi sana kuja kua tajiri,wekeza shambani kwa tija na ufanisi,alafu baada ya miezi kadhaa urudi kutupa feedback hapa
 
Mkuu wewe una mtazamo kama wangu kabisa,na uzuri wa jamiiforums ndio huu,unapotoa wazo au kuomba ushauri unapata darasa la kutosha na hata wengine nao wanafaidika pia!vijijini ardhi ni rahisi sana,hasa ukishajiandikisha kwenye serikali za vijiji!kwa watu wenye mitazamo ya mbali wengi wanakimbilia kuwekeza kwenye ardhi hasa vijijini!mkuu mwenyewe nina wazo ilo la kua na heka za kutosha na nipande miti kama mkakati wa muda mrefu,na target yangu ilikua ni mitiki,ila naona miti hii kama ina changamoto nyingi kidogo,kwa hiyo nilichopanga,niendelee na kilimo cha kawaida,na nianze kupanda miti ya kawaida pia,lakini within 5 years niwe nimeanza kupanda na miteak pia!je mkuu wewe umedhamiria kuanza na miti gani kama utakua na utaalamu wa kutosha?

Ebwanee 1800 kwa sasa nimepanda sana miti ya mbao hii inaitwa PINE ila mwakani nataka nipande miti ya nguzo za umeme ile nayo wigo wa soko ni mkubwa sana na bei ya mti inalidhisha sana ndo mkakati wangu hivi sasa natafuta shamba nikipata ekari 10 zitanitosha kuwekeza kwenye miti ya nguzo za umeme, upande wa mitiki naona kama inastawi sana maeneo yenye unyevu unyevu kama wilaya za Tanga huko kama Lushoto nafikiri na Pangani ukipata ardhi maeneo hayo ni mazuri sana ila huku kwenye joto nimeona watu wameotesha lakini bado sana, mwaka jana nilikuwa na mkakati wa kutafuta shamba la kuotesha michungwa hapo Muheza nikashindwa kupata mkakati wangu bado unaendelea kuna mtu alileta thread hapa ya kilimo cha michungwa ngoja niitafute.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom