Mkuu kwanza nakupongeza kuja hapa jamvini na kuomba ushauri!kwa kweli mimi uwa naumizwa sana na vijana wa Tanzania wapatapo mtaji hata kidogo kukimbilia biashara za mijini kama stationaries,salon,boutique,duka nk ili hali wakikipa kisogo kilimo ili hali ndio utajiri mkubwa kwa sasa!inaumiza zaidi napo ona jirani zetu toka Kenya wanakuja hapa na kukaa vijijini kwa vimitaji vyao vidogo tu na kuweza kuwarubuni kwa visenti vichache wazawa wa eneo husika,na kuweza kufaidika na ardhi yetu na hata nguvu kazi zetu,huku sisi tukikaa pembeni na kubaki kuwasifia tu,"wakenya bwana sio mchezo"...hii kwa kweli inauma sana!vijana wa Kitanzania lazima tuchange mindset zetu,Wakenya wanakuja kulima mahindi,bustani,mpunga n.k kwenye ardhi yetu,wanatumia nguvu kazi yetu na hawauzi hizo bidhaa nchini mwetu,wanapeleka kuuza kwao na nchi nyingine,sisi tunabaki kurubuniwa na visenti vichache na kuendelea kua maskini!Wakenya wametushinda ninh sisi mpaka wao waweze na sisi tubaki kua walalamikaji?mkuu usihangaike kununua bodaboda,kuanzisha stationary wala duka,kwa ushauri wangu mimi wewe wekeza hela yako kwenye udongo,hela hiyo inatosha kulima mpunga,bustani etc,sikushauri mahindi maana hayo umechelewa kwa sasa na kuna changamoto nyingi sana!tafuta maeneo yenye mabonde,piga mpunga wako,piga bustani kama nyanya,hoho,vitunguu,carrot au hata ngogwe na ufanye kitaalamu utakuja kuniambia baada ya miezi sita tu nini matokeo yake!ila kama unapenda kung'ang'ania kukaa mjini kwa kua wewe ni graduate na utakuja kuajiriwa kama zilivyo fikra hasi za sisi vijana wengi wa Kitanzania,basi fanya hayo ya boda boda,mpesa,duka e.t.c!huo ndio ushauri wangu mkuu,hii mitandao ya kijamii tuitumie in a positive way zaidi,tuangalie fursa na mahitaji ya soko kimataifa,kuzalisha vitu kwa ubora stahiki n.k lazima tutafanikiwa tu,ilo ndilo wanalotushinda Wakenya,wepesi kufikiri na kutenda kuliko propaganda,ni wathubutu,na wana uwezo wa kuishi popote na kufanya kazi yoyote bila kujali ana elimu gani..nchi yetu bado mbichi na ina fursa lukuki