Msaada nina uvimbe shavuni nimetumia dawa lakini haujapungua

Msaada nina uvimbe shavuni nimetumia dawa lakini haujapungua

Nenda real hospital na umuone real doctor
Kwa mm huwa naziamini sana hospital za serikal ebu nenda uko ukacheki vzr
 
Naona kuna watu wanamshambulia huyo jamaa aliesema akacheck cancer ila kaongea kitu Cha msingi sana. Aisee hata wewe ukijifanya ni daktari Bado huwez kujua Kila ugonjwa duniani hapa na dalili za ugonjwa fulani hazifanani Kwa watu wote.
Na pia kwani Kuna ubaya gani jamaa akienda kupima na kansa?? Vi- uvimbe uvimbe visivyoeleweka sio kitu Cha kupuuzia hata kidogo. Namimi nasisitiza, pamoja na kupima vipimo vingine aisee pima na kansa mzee.
 
Habari Wana JF, Naomba Ushauri

Niende moja kwa moja kwenye hitaji langu.

Mwezi wa saba nilipatwa na uvimbe ghafla upande wa kulia wa shavu chini ya sikio. Uvimbe ulikuwa mdogo na haukuwa na maumivu yoyote hadi nilipougusa na kuuminya minya, hivyo nikaamua kuupuuza.

Hata hivyo, baada ya miezi miwili, uvimbe ule uliongezeka na kuwa mkubwa, kiasi cha kuonekana kama mtu aliweka nyama mdomoni upande wa shavu kwa ndani.

Nikaenda hospitali na kumweleza daktari hali yangu. Alieleza kwamba ni tezi tu, jambo ambalo linatokea kitaalamu, na mwisho akanipa vidonge vifuatavyo:

1. Ampricox
2. Ibuprofen
3. Prednisone

Naomba ushauri wenu juu ya hili.

lakini hizo dawa nimetumia na Bado ivimbe uko pale pale

naomba Kwa mwenye kujua dawa ambayo inaweza nisaidia , haijalishi ni ya hospital au ya mitishamba lengo langu huu uvimbe utoke maana umeniharibia Hadi mwonekano.

sijaweka picha nimejaribu kupiga ila hazina muonekano mzuri ila naamini maelezo yameeleweka. Asanten
Ushauri:- nenda hospital kakutane na specialist wa ENT. kama uvimbe una zaidi ya wiki 2 basi unahitak uchunguzi mapema kujua n saratan ama n uvimbe wa kawaida.
 
Unaongea upuuzi mtupu, unazijua sifa za malignant tumor? Usipende kuelezea ishu zinazohusu afya ya maisha ya mtu kama wewe sio tabibu. Unakuja kumwingiza mtu ktk hofu ambayo inaweza ikaja kumpoteza kuliko tatizo halisi alilokuwa nalo.
Mpuuzi wewe - humu sio Hospital aende akapime .afya ya mtu aipigiwi ramli aende akapime full stop. Usimpe faraja aende akapime
 
Kwa hili nenda hospital kubwa kafanye vipimo ila nikutoe hofu kidogo kama hakuna mabadiliko ya rang juu ya ngozi kwa eneo hilo basi uwezekano kua ni cancer ni mdogo. Nenda hospital utupe mrejesho. Labda nikuulize hakuna maumivu ya mtoki eneo lolote?
 
Wahi isije ikawa Cancer, kabla haijawa mbaya zaidi .
 
Ndugu upo mkoa gani unaweza pata msada pia maana mwenyewe nilisaidiwa tu mwanangu alikuwa na uvimbe chini ya kidevu nilipata dawa ya kienyeji mara tatu kiliyeyuka maana sjuhi kilipoenda
 
Weka hiyo picha hivyo hivyo tutaelewa,muonekano mzuri wa nini,kwani ni picha za harusi hizo,au hujaona watu wanaweka za kwao za sehemu za siri na wanapata msaada...!
 
Waswahili bhana unatamani mzala awe na Kansa aisee...yaani uvimbe kidogo tu kansa hiyo watu wote wangekua na Kansa basi..
We jamaa jaribu kujielimisha kidogo aisee, nini uvimbe kansa inaweza kuanza kama kijiupele tu au chunusi. Uvimbe wowote usiuchukulie kawaida tu. Elimika bro
 
Pole sana ndugu. Nenda hosp ya tofauti uchekiwe tena. Ondoa hofu. You will be fine. Kila la kheri
 
Pole ndugu yangu tatizo langu sijui kama linaweza kufanana na lako ila Mimi nilihangaika sana miaka kama mitatu ilianza kama matezi baadae ikavimba upande wa kushoto nilitumia ampliclox na dawa zingine sikumbuki uvimbe ukabaki lakini Hauna maumivu , nikaja kwenda Celian Arusha kuna dokta mzungu nikaonana naye yupo makini sana yule Dada hakuwahi nipa dawa ila aliniagiza nikaenda Njiro kufanya kipimo walitumia sindano wakachoma katika ule uvimbe ili atoke na sample ya nyama wakafanya hivyo lakini vipimo vikaonesha hakuna tatizo nikamrudishia yule Dada wa kizungu akaniambia hapana na Mimi ngoja nikupime akatumia kipimo cha Endoscop ila naye hakuona tatizo akaniambia siwezi kukupa dawa maana sijui tatizo , ila nitakufanyia operesheni tutoe sample ya uvimbe biospy kama sikosei alisema Hilo jina itunzwe sehemu ili cell ziwe hai itumwe Nairobi hospital kule kuna vipimo vikubwa na wataalamu maana alisema nikikwambia uende huko gharama ni kubwa itumwe sample tu kutambua ila ilichukua wiki tatu kupata majibu, ikaonekana ile ni TB ya matezi japo alisema tatizo limeshaondolewa ambayo ni uvimbe lakini nitumie dawa miezi sita hadi Sasa nipo vizuri.
 
Back
Top Bottom