Msaada: Ninakutana na changamoto hii kwenye Ajira Portal!

Msaada: Ninakutana na changamoto hii kwenye Ajira Portal!

Tall Guy fam

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2017
Posts
917
Reaction score
1,093
Habari wakuu,

Changamoto ninayokutana nayo kwenye ajira portal ni baadhi ya kazi zinafeli kuapply kwasababu ya kigezo cha degree ya kwanza (BSc). Nina Masters ya Environmental Science na Bachelor ya Environmental Conservation. Kwa mfano wanahitaji assistant lecturer wa Environmental science, nikiapply kwenye system inaniambia FAIL kwasababu sijatimiza kigezo cha degree ya kwanza.

Natambua Environmental Conservation na Environmental Science ni tofauti, lakini kwa kiasi kikubwa zipo related. Na pia katika kazi hiyo hiyo unakuta wanakubali other related fields kama Georgraphy, meteorology, environmental studies, n.k.

Ndugu yangu amenishauri ni edit degree ya kwanza ili kwenye account yangu isomeke BSc Environmental Science. Then niapply. Ikitokea nimeitwa kwenye usaili niwaelezee nilifanya hivyo kwa sababu gani.

Kabla sijafanya hivyo nimeona nije kwenu niombe ushauri zaidi, kama njia hii haitaleta shida huko mbele au kama kuna namna nyingine yoyote ya kufanya.

Natanguliza shukurani.

Annotation 2022-06-27 110420.png
 
Tafuta kazi kulingana na taaluma yako, acha kusumbua system.
 
Tafuta kazi kulingana na taaluma yako, acha kusumbua system.
System ndio mbovu mr/mrs... qualification unaweza kuwa nazo zote na system ikafail..cmplaints desk hawafanyii kaxi hawapokei simu wala kujibu emil..jibu lako lingekua la maana kama system ipo stable kwa vile system yenu kimeo jibu lako ni nuksi tu huna msaada
 
Tatizo wao(programmers) wameulisha mfumo tayari nini unatakiwa kujaza. Nina imani hapo kuna "scrow down" arrow unachagua hizo walozoweka wao. Ili uvuke chagua program ambayo ipo karibu na uliyofanya wewe ili uvuke kiunzi. Mengine huko kwenye usaili.
 
Shukurani mkuu.
 
Back
Top Bottom