Msaada : Nini kazi ya usalama wa Taifa TISS?

Status
Not open for further replies.

KIBARAone

JF-Expert Member
Joined
Mar 26, 2015
Posts
642
Reaction score
243
Utangulizi
Upotevu na uharibifu wa rasilimari za nchi ni mkubwa sana kiasi kwamba wachina wamefikia hatua ya kutorosha hadi kobe kupeleka kwao. Kwa ufupi ni kwamba biashara za magendo juu ya rasilimali za nchi ni mkubwa sana.

Hapo awali hawa jamaa kazi yao ilikuwa tu kuidhibiti chadema isiweze kuharibu Uhai wa chama tawala lakini leo hii Rais mteule anaibua madudu mengi sana ili hali TISS wapo.

Kwa ufupi binafsi TISS nao ni JIPU linahitaji kutumbuliwa.
 
Hiyo idara inahitaji kubadilisha mfumo wote ,kuwe na idara inayoshghulikia mambo ya ndani ya nchi na idara inayoshughulikia mambo ya nje ya ichi ,hizi idara ziwe zinajitegemea
 
Umeuliza kazi ya TISS lakini maelezo yako hayajajipambanua badala yake umetoa shutma tu.Jaribu ku-google TISS uone wanafanya nini.
 
Hiyo idara inahitaji kubadilisha mfumo wote ,kuwe na idara inayoshghulikia mambo ya ndani ya nchi na idara inayoshughulikia mambo ya nje ya ichi ,hizi idara ziwe zinajitegemea

Uncleben wewe ni mchangiaji makini najua. . . . .Hebu jipe muda fuatilia kidogo hili jambo hususan hilo la idara. . . Pitia katiba kidogo na sheria husika

Ukiweka siasa pembeni utaona mengi zaid
 
Last edited by a moderator:
Utangulizi
Upotevu na uharibifu wa rasilimari za nchi ni mkubwa sana kiasi kwamba wachina wamefikia hatua ya kutorosha hadi kobe kupeleka kwao. Kwa ufupi ni kwamba biashara za magendo juu ya rasilimali za nchi ni mkubwa sana.

Hapo awali hawa jamaa kazi yao ilikuwa tu kuidhibiti chadema isiweze kuharibu Uhai wa chama tawala lakini leo hii Rais mteule anaibua madudu mengi sana ili hali TISS wapo.

Kwa ufupi binafsi TISS nao ni JIPU linahitaji kutumbuliwa.

kuibua kwa madudu ulimwambia wewe rais?
 
Hiyo idara inahitaji kubadilisha mfumo wote ,kuwe na idara inayoshghulikia mambo ya ndani ya nchi na idara inayoshughulikia mambo ya nje ya ichi ,hizi idara ziwe zinajitegemea

Tayari hizo idara zipo....
 
Uncleben wewe ni mchangiaji makini najua. . . . .Hebu jipe muda fuatilia kidogo hili jambo hususan hilo la idara. . . Pitia katiba kidogo na sheria husika

Ukiweka siasa pembeni utaona mengi zaid

Ki ukweli mkuu sio kwamba nawabeza ni kazi kubwa wanayoifanya ndio muda Muafuka sheria na katiba kupitiwa na kubadilishwa ili kuweza kujenga mfumo mpya kuwapunguzia majukumu yote ya nchi Kwa mfano MI5 na MI6 na kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa zaidi kama walivyo unda kitengo cha FIU
 
Last edited by a moderator:
Utangulizi
Upotevu na uharibifu wa rasilimari za nchi ni mkubwa sana kiasi kwamba wachina wamefikia hatua ya kutorosha hadi kobe kupeleka kwao. Kwa ufupi ni kwamba biashara za magendo juu ya rasilimali za nchi ni mkubwa sana.

Hapo awali hawa jamaa kazi yao ilikuwa tu kuidhibiti chadema isiweze kuharibu Uhai wa chama tawala lakini leo hii Rais mteule anaibua madudu mengi sana ili hali TISS wapo.
?
Kwa ufupi binafsi TISS nao ni JIPU linahitaji kutumbuliwa.

Haya mnayoyasifia kwa magufuli kwani ameotesha?
 
tupeni kazi zao. mie najua wakipewa meno hawa ni mashushu wa ukweli, na walio somea. lakini kwa sasa nahisi watakuwa wanakinzana kidogo na rais maana, inabidi awaweke wale anaohis atafanya kaz nao.
 
kazi za usalama wa taifa ni 3 tu

1. Kulinda viongozi
2. Kulinda uchumi
3. Kulinda utamaduni

lakini kwa miaka mingi, hayo mawili ya mwisho yalikuwa hayafanyi ndio maana uchumi wetu umeharibiwa na vilevile utamaduni wetu umechafuliwa kabisa. Kwa sasa wamebakia na kazi moja tu kulinda viongozi. Ila inavyoonekana serikali ya awamu ya 5 inaweza kurudisha kazi zao ipasavyo.

Hakuna zaidi ya kazi ni hizo. Mkuu
 
Usalama wa Taifa nao ni binadamu wana mahitaji kama wengine, mkiwasahau njaa ikawa uma kupindukia basi nao wataungana nanyi katika kupiga ufisadi. Mimi naamini ili nchi iendelee inahitaji usalama kwanza, sasa awamu iliyopita iliamua kupeleka fedha nyingi Wizara ya mambo ya nje kuratibu safari za hovyo za rais, huko kwenye vyombo vya usalama kulisahaulika mpaka mwaka wa uchaguzi ndipo wakapeleka hela na vifaa hovyo hovyo bila mpango, lengo likiwa si kulinda usalama wa nchi bali kulinda ccm isindondoke. Kwa kweli watz tumepoteza miaka kumi iliyopita.
 
Kazi kubwa ya TISS ni kuhakikisha kuwa chama chetu kinaendelea kutawala kwa gharama yoyote ile.
 
Ki ukweli mkuu sio kwamba nawabeza ni kazi kubwa wanayoifanya ndio muda Muafuka sheria na katiba kupitiwa na kubadilishwa ili kuweza kujenga mfumo mpya kuwapunguzia majukumu yote ya nchi Kwa mfano MI5 na MI6 na kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa zaidi kama walivyo unda kitengo cha FIU
Kwa minajili ya jina tu huwezi kupunguza majukumu sababu majukumu yanaongezeka na kubadilika kadri asili ya "vivunja" usalama vinayobadilika na kuongezeka. . . .

Mfumo lazima uwe flexible enough kuweza kuendana na mahitaji ya "usalama" kwa wakati huo. . . . .
NB. Wapo watu wa fani, kada "aina zooooote" zinazoweza kufikirika ili hiyo hoja yako iweze kuatamiwa. . . . . .
Wanasema kila zama na kitabu chake. . . . . tusome kilichopo sasa!!!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom