Msaada Nissan xtrail inajizima sana

Msaada Nissan xtrail inajizima sana

kabla hamjanunua magari muwe mnapitia nyuzi za magari zipo humu. xtrail sio gari. pole mkuu.
Xtrail ni bonge ya gari ikizingua haihitaji kanjanja ukileta ujanja ujanja umeharibu ila kwa kusema sio gari haya gari kwako ni ipi sasa maana hata lx inazingua na hautaitamani ikisumbua
 
Cha kukushauri nenda kwa wale wazee wa kukagua gari kwa mashine utapata majibu yako safi kabisa na utaamua ufanye nini ila xtrail japo sijawahi miliki ila ni gari isiotaka ujanja ujanja wa mafundi.
 
Wakuu poleni na majukumu,

Naomba msaada wenu Gar yangu imekua na Tatizo la kuzima ninapokua naendesha na huwasha taa za check engine, taa ya gear box, handbreak na kadhalika lakini ikijizima naisha hapo hapo na inawaka bila shida naendelea na safari mpaka itakapo jizima tena.

Kwahiyo nilikua naomba kwa mwenye uelewa anisaidie mana nataka nilijue tatizo kabla sijaenda kwa fundi kuogopa kupigwa hela nyingi maana uchumi wenyewe kama mnavyoujua
Nilikuwa na tatizo kama lako, japo mimi ilikuwa ikizima haiwashi taa yeyote na ilikuwa ikizima inaweza iwake hapohapo au ikusumbue lakini inawaka.

Nilihangaika karibu miezi miwili na hilo tatizo ila fundi alikuja kubadili sensor moja inaitwa crank sensor na tatizo halijawahi kujirudia tena.
 
Dar kuna mafundi wengi sana waongo, hasa Ilala yote hakufai, ila huwezi kosa mtalaam wa X-Trail Dar, do your homework, ila ujue hakuna fundi Dar es salaam ambaye atakwambia siwezi, anataka achukue hela aende zake.
Ngoja nimuunganishe na Mbossa garage wa hapa Iringa. Fundi mzuri sana wa hizo gari hapa Iringa Mkuu.
 
Back
Top Bottom