Msaada: Nitapata wapi hospital ya mifupa tofauti na MOI?

my web

JF-Expert Member
Joined
Dec 23, 2012
Posts
1,592
Reaction score
242
nilimpeleka ndugu yangu muhu2 kitengo cha mifupa[moi] wananizungusha pesa nimelipa mizunguko kibao mgonjwa hajapata huduma na mm naona bora nitafute hosp nyingine.wana jf kuna uwezekano kwa siku mbili tatu kupata ufumbuzi.nisaidien
 
Sure nenda kibaha,au bugando ukionana na dr Isdory anafanya fasta,mpe pole jamaa najua maumivu yake kwani bado nauguza mguu nilipata ajari mwaka jana nikavunjika kuanzia kwenye paja mpaka kwenye ankel,operation ya kwanza(paja) ilifanyika peramiho songea,ya pili ndo akanifanyia Isdory!!!
 
Nenda kwa dr burhan pale burhan charitable clinic(anjuman sei fii)mtaa wa samora.
 
Nenda Kibaha kuna hospital ya Dr Baki ni bingwa wa mifupa atakusaidia

Kweli aisee, aende KIBAHA - Kwa Mathias. Kuna Hospital ya Dr. Baki Inaitwa 'BURERE HOSPITAL', niliwahi kumpeleka Bimkubwa wangu pale, alipata ajali akavunjika mguu. Nilimshuhudia Dr. Baki kwanza akiumalizia kuuvunja, kisha akaanza kupanga vipande vya mifupa kimoja baada ya kingine!. Ilimchukua miezi kama mitano Bimkubwa akapona. Ila Matibabu yake yana Gharama kubwa kidogo. Wataalam wa mifupa nasikia wapo wachache hapa bongo. Unaweza pia kwenda Moshi KCMC, Mbeya na Bugando.
 
usiende mbali sana baki hapo hapo muhi2 ila pitia mlango wa nyuma
 
Nenda hospitali ya Consolata Mission Ikonda. Hii ni internation.sithani kama bongo nzima kuna hospitali kama hii.na bei yao ni kawaida sana,inamilikiwa na waitaly,iko full loaded kwa kila kitu.ipo makete
 
Nenda hospitali ya Consolata Mission Ikonda. Hii ni internation.sithani kama bongo nzima kuna hospitali kama hii.na bei yao ni kawaida sana,inamilikiwa na waitaly,iko full loaded kwa kila kitu.ipo makete

tatizo ni kwamba madaktari wao bingwa wanatoka nje ko wana miezi yao ya kuwepo pale. Mfano huyo wa mifupa atakuwepo mwezi july, labda kama mvunjiko wake ni mdogo kiasi cha kuhitaji simple procedure. Mimi namshauri hivi, ambadilishe huyo mgonjwa to ippm na amtafute daktari wake atapata tiba mapema tu. Achana na mambo ya wagonjwa wa jumuia, utafia kwenye foleni. Serikali yetu haijaweka good means za accessible health services mpaka kwa wale wasiona uwezo wa mlo wa siku. Jaribuni kuzigharamia ili mpone haraka na mrudi kazini kwenu.
 
Poleee sana... Mpeleke ccbrt msasani... Wanahuduma nzuri sana..
 
kwa dr baki kibaha ni pazuri ila gharama zake sio za kitoto. Kcmc hapana tafadhali.
 
Uliingizwa theater?! Kiboko!
Mimi nilimshuhudia akimtapeli ndugu yangu na hajapona mguu hadi leo! Alikamata laki nane za kumfanyia upasuaji upya. Akamuingiza theater akamtoa na POP, kwa madai ameona haina haja ya kumpasua upya. P.O.P kwa laki 8!!!
 
Peramiho mission hospital ni jibu la matatizo yako. Utakutana na docta lemy mtaalamu aliyebobea kt matatizo kama yako. Huduma za kiroho kama vile maombi zinapatikana.
 
Uliingizwa theater?! Kiboko!
Mimi nilimshuhudia akimtapeli ndugu yangu na hajapona mguu hadi leo! Alikamata laki nane za kumfanyia upasuaji upya. Akamuingiza theater akamtoa na POP, kwa madai ameona haina haja ya kumpasua upya. P.O.P kwa laki 8!!!
Unayosema ni kweli kabisa na mimi yamenikuta. Mbali ya kutumia pesa znyingi zaidi ya m15 ndugu yangu hakupona na aliishia kutukejeli.
 
nilimpeleka ndugu yangu muhu2 kitengo cha mifupa[moi] wananizungusha pesa nimelipa mizunguko kibao mgonjwa hajapata huduma na mm naona bora nitafute hosp nyingine.wana jf kuna uwezekano kwa siku mbili tatu kupata ufumbuzi.nisaidien

Ndugu my web pole sana. Ninashangaa sana kwamba umelipia oparesheni MOI wakati hujapangiwa hata siku ya upasiaji. Ni jambo lisilokubalika, ikiwa kweli imetokea.
Lakini ndugu zangu wana JF, msidanganyane kuhusu kuwapo madaktari wazuri wa mifupa nje ya MOI kwa hapa Tanzania. Cream yote ya madaktari wa mifupa Tanzania inakimbilia MOI maana wanalipwa vizuri.
Nawaonea huruma watu wasemao kuna madaktari Peramiho, Ikonda et al, ambazo ni hospitali za mission. Hospitali hizi hutembelewa mara kwa mara na madaktari kama vile toka Ujerumani, ambao huja kufanya upasuaji kwa watanzania kama wanajifunza vile. Ila watu wakiguswa na mzungu huona washapona.
Dr. Baki si mzuri wa kila eneo la mifupa, na amekuwa incompetent katika mengi. Watu huishia kulalama.
TATIZO LA MOI
Tatizo lililo wazi MOI ni foleni za wagonjwa wanaolipa hizi gharama za serikali ili wapate tiba. Wagonjwa wa ajali za Bajaj na bodaboda nao wamekuwa mzigo.
USHAURI
Mtafute daktari anayehusika na tatizo alilonalo mgonjwa halafu akusaidie kumtibu mgonjwa kwa fast track. Ni gharama, lakini ina reflect gharama halisi ya tiba kwa sasa, maana gharama zile zinazolipwa na kusababisha watu wachelewe kufanyiwa operation zinahusisha cost sharing toka serikalini, kitu ambacho serikali inaelekea kushindwa.
Si shauri mgonjwa kupelekwa Mbeya, Bugando, CCBRT au KCMC kwa kuwa vitengo vyao vichanga sana, labda awe na issue ndogo.
 
Last edited by a moderator:
.....popote pale uendako Dr. Mboya kwenye ishu zinazohusu Mifupa ni mwisho wa matatizo: jamaa ni mtaalamu(ni Daktari Bingwa) haswaaa. Anapatikana MOI na pia unaweza kumpata Kairuki Hosp-Mikocheni(pale huwa ana clinic siku ya J'mosi) kama vipi ni PM nikurushie namba yake ya simu.
 
Wagonjwa 25 kwa siku jumamosi kwa kairuki ,lazima uwahi mida ya saa kumi alfajiri uwepo.

me sijaenda bado(nina issue ya mfupa pia) nachelewa kuamka!.
 
Dk Baki ndo mwisho wa matatizo ndg yangu,kuna rafiki wangu niliendaga nae pale na maendeleo yake ni mazuri kusema kweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…