Magari haya yanayotoka kwa wenzetu, yanakifaa maalumu kimefungwa kwenye exhaust system kwa ajili ya kuchuja exhaust gases ili mazingira yasiharibike.
Kifaa hicho kinaitwa "Catalytic fuel converter" CFC.
Hii ikiziba, huwa inahitaji replacement, lakini kwa bahati mbaya hazipatikani hapa nchini.
Matokeo ya kuziba kwake, exhaust gases hazitoki kwenye combustion chamber na hivyo kupelekea air intake kuwa ndogo.
Ukitaka kujua kama tatizo ni hilo, mwambie mtu aingie kwenye gari, ajaribu kukanyaga mafuta huku ukiwa umeweka mkono kwenye bomba la kutolea moshi ulinganishe msukumo unaotoka kwenye gari yako na ule unaotoka kwenye gari ambayo haina tatizo utagundua tofauti kubwa.
Suluhisho la tatizo hilo, ni kuwaona mafundi wafungue sehemu ya exhaust ambayo ina hiyo CFC, waitoboboe kisha waondoe chujio lililomo ndani ambalo ni kama unganga.
Baada ya hapo wazibe sehemu iliyokatwa na kurejesha kwenye gari.
Rafiki yangu aliyekuwa Harrier alikuwa na tatizo hilo na wiki iliyopita nimemsaidia gari imekuwa mpya.