Wakuu Habarini/asalaam/Shalom
Me ni kijana wa Miaka 25 Ila nipo kwenye mtihani ambao sijui nitatokaje
Nimekuwa nikiteswa na tatizo la mkojo kwa kipindi kirefu sana zaidi ya miaka 10+
Nikienda haja ndogo ninateseka sana kutoa mkojo,ninaweza kutumia mpaka dakika 10 au zaidi ndo mkojo utoke, na ukitoka natoa mkojo mdogo sana na bado mwingine nahisi upo ndani………..
nimekunywa miti shamba mbalimbali,nimekwenda hospital kubwa Kama Bugando-Mwanza lakini hali bado iko pale pale
Nilipoenda Bugando,nilikutana na urologists,walinifanyia vipimo na wakaniwekea mpaka catheter (Mrija kwenye njia ya mkojo)niliambiwa nasumbuliwa na kichocho………nikapewa vidonge nikatumia kwa muda mrefu sana lakini bado hali ikawa ile ile mpaka Leo na hakuna mabadiliko yoyote
Kama kuna mtu anapitia changamoto au alishawahi pitia karibu tushauriane ni kwa namna gani ulitoka kwenye hii dhahama
Karibuni wapendwa🙏🏿