Msaada: Sijapata hedhi toka Oktoba 30

Tanya

JF-Expert Member
Joined
May 4, 2013
Posts
340
Reaction score
159
Habari ndugu zangu.
Mara ya mwisho kuingia siku zangu ni Octoba 30, hadi leo hii December kimya inapita tu siielewi na nimepima UPT sina ujauzito, wakati chuchu zinauma na wajati mwingine timboni najihisi kama nakaribia period lakini hakuna chochote kinachotoka. hali hii inanichanganya,

Kuna rafiki kuniambia yaweza kuwa homon imbalance sasa sijui ni sahihi au la na sijui matibabu yake ni yapi ili niweze kuona ada yangu ya kila mwezi
Kwa mwenye kuelewa naomba unisaidie tafadhali.
 
pole sana ngoja waje wataalaam, wakupe msaada dada yangu mpenzi
 
Kama hujabadilisha mazingira na ushafanya tendo la ndoa Siku za katikati tayar umesha conceive..so nenda ukapima UPT haraka!
 
Hormone imbalance pia huchangia kukaa kutokuona siku zako kwa muda muafaka,ukienda hospital kama Tatizo ni hormone imbalance utapatiwa dawa tatizo litaisha!
Je umatumia Mpango wa uzazi? Kama watumia pia huenda ndo sababu
 
Iruhusu akili yako kupata mapumziko(relaxing). Baadaye pitia kwa utaratibu maisha uliyoishi kwa kuzingatia vitu vyote vizuri na magumu yote(kama yapo) tangu hedhi ya mwisho.
Kuna uwezekano kweli wa kuwepo kwa "hormonal imbalance" . Kama maisha yalikuwa poa sawa na siku zote jaribu kupima tena ujauzito ili kujiridhisha.

Kama umewahi kutumia njia yoyote ya uzazi wa mpango,angalia ni njia gani na mara ya mwisho ilikuwa lini. Kisha mtiririko wa hedhi upoje tangu umeacha. Kama hakuna basi ni vema kuonana na daktari kwa ushauri zaidi.
Pole
 
Muone au subiri ushauri wa gynecologist nyingine zitakua ramli nyegeshi
 
bora wewe hujapata, mm mwaka wa 2 huu....
yani inatoka kutwa nzima matone matano labda...

naona bora ww haitoki kabisa


Pole sana mkuu. Mke wangu yeye mara ya mwisho aliona siku zake mwezi wa Julai 2017. Juzi ndio ameona siku zake yani anagalagala kwa maumivu ya kiuno.
 
Labda umefikia menopause! Umri wako please!
 
Niaze kwa kusema pole kwa tatizo ulilolipata....kitendo cha kutopata hedhi(amonorhea).. hii husababishwa na vitu lakina jambo ambalo ni kubwa na la kwanza na la msingi ni UJAUZITO(kama ulivyosema ulishapolima kipimo cha mimba UPT..sijajua ulipima lini? na baada ya mda gani? pale ulipohis hupati hedhi una umri gani? ulishawah kutoa mimba!? ushawah kupata tatizo kama hili uko nyuma? na kwenye familia je kuna mtu alishawah kupata shida kama hii!?...nigependa unipe kwanza haya majibu)..

sasa kama nilivyosema wazo la kwanza ni UJAUZITO ivyo tutakupima mimba sasa kwa kipimo cha UPT hapa sasa ili tujiridhishe ni mimba au lah!!! kama ni mimba basi tutakuanzishia clinic (RCH4) na maswala mengiene ya ujauzito yatafuta...
na pia kama kipimo kitasoma Negative(-) maana yake mimba haipo sasa hapa inabid tuangalie chanzo cha kutopata hedhi tatizo ilo linaitwa[Secondary amonorhea!!!] ambapo sasa husababishwa na vitu vingi kama vifuatavyo
1/ mvurugiko wa homoni(hormone imbalance)
2/uzito uliopitiliza (obesity)
3/vyakula(nutrition disorder)
4/ uvimbe(polys,,myoma,,,GTD)
5/mzunguko hedi usio na uwiano(irregural menstrual cycle)..
6/kutoa mimba(abortion)
7/msongo wa mawazo(stress)
na vitu vingine
SASA UFANYAJE /KIPI KIFANYIKE
nenda hosptali iliyokaribu watakupima vipimo ivi

UPT(ichi ni kipimo cha mimba ili tujue mimba ipo au haipo)

kama mimba haipo then itabid vipimo vifuatavyo
1/ Hormone profile (kucheki hormone zako zimekaaje) na kama zitakua sawa au zitaonekana zinashida utapewa dawa ya kuweka hormone sawa na mwisho wa siku mambo yatakaa sawa!!!

2/Abdominal ultrasound(USS) hii itatusaidia kutuambia tatizo nin haswa kwenye mfumo wako wa uzazi ivyo kubaini shida na kupewa huduma stahiki...

baada ya hapa kaa kutakua kuna ulazima wa vipimo vingine then vitafuata ila ivi ndo vyamsing sana

NB: sio mala zote mtu asipopata hedhi huwa ni tatizo la kiafya wakat mwingine huwa ni msongo wa mawazo mazingira ata mazoezi magumu ivyo baada ya mda mambo huwa shwari...

naamin umepata mwangaza kidogo ila uwahi hospitali mapema!!!!
 
Hiyo inaweza pia kusababishwa na condition yaan hali yahewa ambayo upelekea hormone imbalance
 
Pole sana mkuu. Mke wangu yeye mara ya mwisho aliona siku zake mwezi wa Julai 2017. Juzi ndio ameona siku zake yani anagalagala kwa maumivu ya kiuno.
mm nazipata ila kiuno kinauma miguu yani misuli kwanzia kiunoni kushuka chini inauma balaa...hapo chini ya kitovu ndio hata hapaelezeki ni kama kuna kidonda kikubwa
 
Fafanua vzr mkuu usaidiwe!!!
Yani napata hedhi kila mwezi, lakini sasa maumivu nnayopata acha tu..

Naumwa nyonga ,hips ,miguu inauma sana yani humu kwenye maungia na misuli inauma

chini ya kitovu ndio panauma kama kuna kidonda..
halafu inatoka kidogo sana... yani kutwa nzima ni kama matone 10 hivi pamoja na maumivu yote hayo...
yani hata nikisema nivae pedi Siku5 haijai
 
mm nazipata ila kiuno kinauma miguu yani misuli kwanzia kiunoni kushuka chini inauma balaa...hapo chini ya kitovu ndio hata hapaelezeki ni kama kuna kidonda kikubwa


Pole mkuu. Umejaribu kwenda hospitali?
 
mm nazipata ila kiuno kinauma miguu yani misuli kwanzia kiunoni kushuka chini inauma balaa...hapo chini ya kitovu ndio hata hapaelezeki ni kama kuna kidonda kikubwa
una umri gani!? tatizo lina mda gani!? ushazaa au lah!!? na maswali mengine ya uprivate siwez kiyauliza hapa ila ayo ya juu ebu nipatie majibu yake!!! mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…