Habari ndugu zangu.
Mara ya mwisho kuingia siku zangu ni Octoba 30, hadi leo hii December kimya inapita tu siielewi na nimepima UPT sina ujauzito, wakati chuchu zinauma na wajati mwingine timboni najihisi kama nakaribia period lakini hakuna chochote kinachotoka. hali hii inanichanganya,
Kuna rafiki kuniambia yaweza kuwa homon imbalance sasa sijui ni sahihi au la na sijui matibabu yake ni yapi ili niweze kuona ada yangu ya kila mwezi
Kwa mwenye kuelewa naomba unisaidie tafadhali.
Niaze kwa kusema pole kwa tatizo ulilolipata....kitendo cha kutopata hedhi(amonorhea).. hii husababishwa na vitu lakina jambo ambalo ni kubwa na la kwanza na la msingi ni UJAUZITO(kama ulivyosema ulishapolima kipimo cha mimba UPT..sijajua ulipima lini? na baada ya mda gani? pale ulipohis hupati hedhi una umri gani? ulishawah kutoa mimba!? ushawah kupata tatizo kama hili uko nyuma? na kwenye familia je kuna mtu alishawah kupata shida kama hii!?...nigependa unipe kwanza haya majibu)..
sasa kama nilivyosema wazo la kwanza ni UJAUZITO ivyo tutakupima mimba sasa kwa kipimo cha UPT hapa sasa ili tujiridhishe ni mimba au lah!!! kama ni mimba basi tutakuanzishia clinic (RCH4) na maswala mengiene ya ujauzito yatafuta...
na pia kama kipimo kitasoma Negative(-) maana yake mimba haipo sasa hapa inabid tuangalie chanzo cha kutopata hedhi tatizo ilo linaitwa[Secondary amonorhea!!!] ambapo sasa husababishwa na vitu vingi kama vifuatavyo
1/ mvurugiko wa homoni(hormone imbalance)
2/uzito uliopitiliza (obesity)
3/vyakula(nutrition disorder)
4/ uvimbe(polys,,myoma,,,GTD)
5/mzunguko hedi usio na uwiano(irregural menstrual cycle)..
6/kutoa mimba(abortion)
7/msongo wa mawazo(stress)
na vitu vingine
SASA UFANYAJE /KIPI KIFANYIKE
nenda hosptali iliyokaribu watakupima vipimo ivi
UPT(ichi ni kipimo cha mimba ili tujue mimba ipo au haipo)
kama mimba haipo then itabid vipimo vifuatavyo
1/ Hormone profile (kucheki hormone zako zimekaaje) na kama zitakua sawa au zitaonekana zinashida utapewa dawa ya kuweka hormone sawa na mwisho wa siku mambo yatakaa sawa!!!
2/Abdominal ultrasound(USS) hii itatusaidia kutuambia tatizo nin haswa kwenye mfumo wako wa uzazi ivyo kubaini shida na kupewa huduma stahiki...
baada ya hapa kaa kutakua kuna ulazima wa vipimo vingine then vitafuata ila ivi ndo vyamsing sana
NB: sio mala zote mtu asipopata hedhi huwa ni tatizo la kiafya wakat mwingine huwa ni msongo wa mawazo mazingira ata mazoezi magumu ivyo baada ya mda mambo huwa shwari...
naamin umepata mwangaza kidogo ila uwahi hospitali mapema!!!!