Members naona wengi wamekuwa wakichanganywa na maelezo ya mara kwa mara yaani post nyingi halafu kila moja inaelezea hali tofauti niliyonayo.
Nimeona niweke full mkanda:
Nilipelekwa hospital nilikiwa sijitambui kwa case ya kupata pumzi yaani kuhema sana pumzi fupi fupi na hewa yaani shida nilihudumia na masindano dakika kadhaa nilihisi napata pumzi vyema, nilipoongea na doctor kumuuliza hii ni nini akasema ni PNEUMONIA hiyo basi nilipigwa sindano kila baada ya masaa 6 na dawa nyngne nikajihisi nipo fresh na hata wao waliniruhusu wakijua tatizo limekwisha na mimi nikiamini naenda kusikilizia siku kadhaa nasimama vizuri na nilikuwa nishafanya Xray tayari.
Sasa ajabu ni kwamba baada ya kurud home naweza sema homa ilizidi zaidi maana wakati naruhusiwa nilikuwa naweza hata kutembea ila hapa nyumbani nilikuwa nashindwa hata kukaa na kusimama muda wote nilikuwa nalala tu kuhema so niliwasiliana na doctor kumuelewesha hiyo hali aliniambia baadhi ya antibiotics zikagonga mwamba hapo ndo akanishauri nikapime TB aliniongoza nikapime wap nilipelekwa lakini wakati huo mimi nilikuwa sina kikohozi chochote mpaka kule hospital walishindwa kunipima waliamua kunianzisha dozi kutokana na maelezo na ile hali ya kushindwa kukaa na kukutembea na kuhema sana kohozi sikuwapatia wakanambia hyo ni TB wewe nenda katumie baada ya wiki mbili utaanza kuwa fresh basi nilizichukua nikaanza jumanne ile ile.
Sasa nikiwa kwenye hii tiba ndio matatizo yanazidi maana ile hali ya kushndwa kuinuka bado ipo na nahema kwa shida sana na dawa nazingatia
siku ya jana nilihema hema usku kucha nikahc nikitumia dawa za tb ndan y muda wake itatulia lkn nilitumia na nilihema sana na kikohoz ambcho kilitokana na kukosa hewa y kutoshaa ikaonekana itanpa shida maana ukiwa unatumia dawa za tb lazma ule na chakula ni shida maana pumzi imebanwa
nilikimbizwa hospital kupewa huduma y kwnza kupumua nilipotulia nkapelekwa hospital moja y wilaya hpa dar
sasa hawa jamaa wanachodeal nacho ni pumzi na wameniweka kitengo cha pumzi na mashine y kupumulia na kujisaidia na wkt huo dawa za TB nazitumia ila wanadeal sana na pumzi na mimi ninavyojiona changamoto yngu ni pumzi ndo imebak i tu
Nikifkria mchakato wa mimi kuanzishwa dawa za TB na nikiangalia kinachonisumbua naona tofauti inawezekana sina kutokana kwamba sina dalili zake au imo kwahyo natumia dawa za TB nikiwa sina uhakika
Sent using
Jamii Forums mobile app