Msaada: Siku sita tangu nianze dawa za TB nasikia maumivu makali sana ya uti wa Mgongo

Msaada: Siku sita tangu nianze dawa za TB nasikia maumivu makali sana ya uti wa Mgongo

Jamani eeh nina maumivu makali sana tena sana kwny uti wa mgongo na leo ndio sku y 6 tu tangu nianze dozi za TB

Naomben ushauri jmn hii ndio TB tu au kuna tatzo nyngne maana doctor amenijibu endelea na dawa 2 ila nateseka nimelala kitandani napata maumivu makali kwenye uti wa mgongo jamani msaada

Sent using Jamii Forums mobile app
Helloh, pole sana kwa hali unayopitia. Naomba kujua walitumia kipimo gani kugundua una TB?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inasikitisha.

Kwa jinsi inavyoonyesha huyu mwana jf mwenzetu amepoteza maisha kutokana na PROFESSIONAL NEGLIGENCE ya hali ya juu kabisa.

Huu ni mfano hai wa hali zilivyo katika mahospitali yetu. Watu wanatibiwa empirically, tena kwa kubahatisha bahatisha.

Kuna shida kubwa sana kwa madaktari wetu wa sasa.

Ingekuwa huu uzembe umetokea katika nchi zilizoendelea kuna watu sasa hivi nina uhakika wangekuwa tayari wanakabila na tuhuma nzito.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
r.i.p mkuu!
Umetangulia nasi tutafata...
 
Tanzania kuna "Doctor" alimwambia mtu kuwa ana TB akakndamizwa madawa akawa anazidiwa tu, ndugu zake wakampeleka India huko baada ya vipimo vya uhakika akakutwa hana TB ana acidity tu imemfanyia ulcers inamsumbua. Katibiwa siku tatu, karudi mzima wa afya.

Tanzania tiba ni majanga kusema kweli.

Hakikisha kweli una TB kama dada anavyosema hapa ni muhimu. Chukua Xray zako peleka kwa madaktari wazuri tofauti kabla ya kudandia madawa. TB haipatikani kirahisi hivyo. Unaweza ukawa na ugojwa mwingine. Vilevile TB inaambukiza inakuwaje upo tu mtaani ! Dr huyu mashakani
 
Mtoa mada amesha fariki mkuu, so sad
 
Pole kwa wafiwa JF Dar na Members Wote kwa ujumla.

Pongezi kwa Wote walioshirikiana na Marehemu kwa namna moja au nyingine.
 
Back
Top Bottom