Msaada: Simu gani ina rekodi sauti vizuri ambayo naweza kuitumia ku record content you tube?

Msaada: Simu gani ina rekodi sauti vizuri ambayo naweza kuitumia ku record content you tube?

Bongotunacheza

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2018
Posts
983
Reaction score
2,306
Nahitaji simu ya kawaida kabisa bajeti yangu laki na 30.

Kikubwa iwe ina uwezo wa kutoa audio inayo sikika vizuri. Iwe Type C ambayo inaweza kutumia vile vi microphone vya sh elfu 25.

Nakumbuka mwaka 2017 nilinunua kisimu cha promotion pale Mlimani City cha VODAFONE. Nilikinunua sh elfu themanini ila kilikuwa very useful strong and powerful na kilikuwa kinatoa sauti nzuri sana ukirekodi audio.

Nilienda kukiulizia tena mwaka jana nikakuta havipo tena stock limeisha.

Now natumia simu ya mkopo ambayo ninaweza nikasema ni kama nimepigwa. Gharama yake jumla ni kama sh laki 3 na themanini. Ila up to know simu imekufa sauti mtu akipiga hamsikilizani. Audio haifanyi kazi kabisa hata ukijirekodi sauti unasikika kwa mbali sana.

Ni simu ya kihindi hawa jamaa wauzaji nahisi watakuwq walikosa soko wakaamua kurudisha gharama zao kwa kutupiga kwa staili hiyo. Sasa nauliza bandugu je ni simu gani ya gharama nafuu ambayo ukirekodi sauti inasikika vizuri?

Kama una ijua naomba unifahamishe na gharama yake tafadhali na inapopatikana ndani ya Dar es salaam.

Asante sana
 
Achana na audio kutegemea simu, nunua mic portable zile. Utapata quality nzuri zaidi.
Hiyo mic portable naitumiaje mkuu kwenye simu ama kwenye computer?

Lengo langu ni kupata vyote simu pamoja na Mic ambayo nakuwa nachomeka kwenye simu narekodi audio then baadae na isend kwenye email inaenda kuwa converted into MP4 then naipublish kwenye You Tube account yangu
 
Mic ipo hivi:
images (10).jpeg

Haizidi elfu 30
 
Asante sana mkuu sasa swali langu ni nikishakuwq na hiyo mic naitumia vipi hadi kufikisha content yangu you tube? Je naitumia yenyewe kama yenyewe au lazima na simu ihusike? Kumbuka Mimi nafanya audio tu sifanyi video
Okay utafanya hivi.

1. Unachukua iyo mic.
2. Unachukua simu unaunganisha na mic.
3. Unafungua application ya kurecord audio kwenye simu yako.
4. Unaanza kuongea.

Fanya majaribio ya kuongea na kuweka mic umbali tofauti tofauti ujue position nzuri

Record usiku, kukiwa kumetuliaaaa mfano amka saa 6 anza hadi saa 10.

Unachokiongea kiandike kwanza, usitoe maneno kichwani kama Bongo movie
 
Mic haina mpinzani mkuu. Ila achana na wireless (labda zile za bei kubwa) ila nenda wired.
Ahaa na nilikuwa najua labda kapata sound clear ni lazma utoboke Ila kwa hizo bei nimeona inawezekana.

Na kuna zile mic huwa zimekaa kama vibufa vidogo. Naona wenye podcasts wanazitumia sana Ila sijajua ni bei gani
 
Back
Top Bottom