Msaada: Simu gani ina rekodi sauti vizuri ambayo naweza kuitumia ku record content you tube?

Msaada: Simu gani ina rekodi sauti vizuri ambayo naweza kuitumia ku record content you tube?

Nahitaji simu ya kawaida kabisa bajeti yangu laki na 30.

Kikubwa iwe ina uwezo wa kutoa audio inayo sikika vizuri. Iwe Type C ambayo inaweza kutumia vile vi microphone vya sh elfu 25.

Nakumbuka mwaka 2017 nilinunua kisimu cha promotion pale Mlimani City cha VODAFONE. Nilikinunua sh elfu themanini ila kilikuwa very useful strong and powerful na kilikuwa kinatoa sauti nzuri sana ukirekodi audio.

Nilienda kukiulizia tena mwaka jana nikakuta havipo tena stock limeisha.

Now natumia simu ya mkopo ambayo ninaweza nikasema ni kama nimepigwa. Gharama yake jumla ni kama sh laki 3 na themanini. Ila up to know simu imekufa sauti mtu akipiga hamsikilizani. Audio haifanyi kazi kabisa hata ukijirekodi sauti unasikika kwa mbali sana.

Ni simu ya kihindi hawa jamaa wauzaji nahisi watakuwq walikosa soko wakaamua kurudisha gharama zao kwa kutupiga kwa staili hiyo. Sasa nauliza bandugu je ni simu gani ya gharama nafuu ambayo ukirekodi sauti inasikika vizuri?

Kama una ijua naomba unifahamishe na gharama yake tafadhali na inapopatikana ndani ya Dar es salaam.

Asante sana
Njoo nkupe hii package kwa 25k hutojutia
 
Attachments

  • Screenshot_20240428_013417_WhatsApp.jpg
    Screenshot_20240428_013417_WhatsApp.jpg
    171.3 KB · Views: 8
Ahaa na nilikuwa najua labda kapata sound clear ni lazma utoboke Ila kwa hizo bei nimeona inawezekana.

Na kuna zile mic huwa zimekaa kama vibufa vidogo. Naona wenye podcasts wanazitumia sana Ila sijajua ni bei gani
Kumbe ni mdau aa podcast. Safi sana.
 
Ahaa na nilikuwa najua labda kapata sound clear ni lazma utoboke Ila kwa hizo bei nimeona inawezekana.

Na kuna zile mic huwa zimekaa kama vibufa vidogo. Naona wenye podcasts wanazitumia sana Ila sijajua ni bei gani
Zile za kishua sana. Bei zake kidogo unakuta juu.
 
Okay utafanya hivi.

1. Unachukua iyo mic.
2. Unachukua simu unaunganisha na mic.
3. Unafungua application ya kurecord audio kwenye simu yako.
4. Unaanza kuongea.

Fanya majaribio ya kuongea na kuweka mic umbali tofauti tofauti ujue position nzuri

Record usiku, kukiwa kumetuliaaaa mfano amka saa 6 anza hadi saa 10.

Unachokiongea kiandike kwanza, usitoe maneno kichwani kama Bongo movie
Asante sana mkuu asubuhi nitadamkia Mlimani City kutafuta kisimu cha walau laki na nusu then niende Kariakoo nitafute hizo microphone.

Kwa hiyo mkuu unataka kuniambia nikitumia hiyo microphone sauti inatoka quality kama studio?
 
Ahaa na nilikuwa najua labda kapata sound clear ni lazma utoboke Ila kwa hizo bei nimeona inawezekana.

Na kuna zile mic huwa zimekaa kama vibufa vidogo. Naona wenye podcasts wanazitumia sana Ila sijajua ni bei gani
Aje tumpe zote zipo dulani
Kwa bei ya 25k tu
 
Attachments

  • Screenshot_20240428_013417_WhatsApp.jpg
    Screenshot_20240428_013417_WhatsApp.jpg
    171.3 KB · Views: 9
Ila mkuu sasa sawa sikatai ndio budget yako ya 130K afu upate high quality kwa ajili ya content za YouTube ?? Ninachotaka kusema kama ulichukua device uliyoko nayo saiv ya 300K afu unasema imekufa .. sembuse hiyo 130K tena Kwa Ajili ya Content...hata hao audience inabidi wawe na moyo wa kuangalia hizo content zako...No offense [emoji23]
 
Kama umesoma vizuri uzi wangu nimesema mwaka 2017 nili nunua Mlimani City simu ya elfu 80 na ilikuwa ina rekodi sauti vizuri tu.

Kingine nimesema hii simu ya mkopo nimepigwa kwa sababu hata sauti kuwasiliana na mtu hatusikilizani vizuri.
 
Asante sana mkuu asubuhi nitadamkia Mlimani City kutafuta kisimu cha walau laki na nusu then niende Kariakoo nitafute hizo microphone.

Kwa hiyo mkuu unataka kuniambia nikitumia hiyo microphone sauti inatoka quality kama studio?
Laki na nusu unaenda nayo Mlimani City kufanya nini kama sio utani?

Zama Kariakoo kajitupe kwenye ma-Tecno huko ya low budget, Mlimani City sio sehemu sahihi ya kununua bidhaa ikiwa hela Yako ni ya ngama
 
Ila mkuu sasa sawa sikatai ndio budget yako ya 130K afu upate high quality kwa ajili ya content za YouTube ?? Ninachotaka kusema kama ulichukua device uliyoko nayo saiv ya 300K afu unasema imekufa .. sembuse hiyo 130K tena Kwa Ajili ya Content...hata hao audience inabidi wawe na moyo wa kuangalia hizo content zako...No offense [emoji23]
Watanzania wanajali content sio presentation yake na ukitaka kujua angalia content za vichekesho. Nyingi zipo natural tu, hakuna lighting wala sauti nzuri Ila watu wanajali kusikia, kuona na kucheka. So ni kawaida sana
 
Kama umesoma vizuri uzi wangu nimesema mwaka 2017 nili nunua Mlimani City simu ya elfu 80 na ilikuwa ina rekodi sauti vizuri tu.

Kingine nimesema hii simu ya mkopo nimepigwa kwa sababu hata sauti kuwasiliana na mtu hatusikilizani vizuri.
Ndio maana uliporudi ukaambiwa hazipo.

2017 Whatsapp tu ilikuwa ukii download ilikuwa na 15MB

Saizi app hiyo ina 45+MB

Ushauri wangu ni kwamba utafute simu ambayo itakuwa na standard za kuendana au kukaribiana na usasa wa technology ambayo tupo.

Kwa maana usitafute simu Kawasababu tu ya kazi ya kurekodi audio halafu siku ukawa na mahitaji ya kuitumia Kwa mambo mengine ukajikuta unakwama Kawasababu Haina uwezo.

Ni ushauri tu.
 
Hiyo mic portable naitumiaje mkuu kwenye simu ama kwenye computer?

Lengo langu ni kupata vyote simu pamoja na Mic ambayo nakuwa nachomeka kwenye simu narekodi audio then baadae na isend kwenye email inaenda kuwa converted into MP4 then naipublish kwenye You Tube account yangu
IMG_9399.jpeg

Kama hichi hapa

Sauti inatoka very clear

@20,000 tu
 
Mkuu tafuta flagship za Nokia Lumia, hazina issue siku hizi matumizi ya kawaida masoko ya mtumba unazipata bei za kutupa most of time chini ya laki.

Simu kama lumia 950, 930, 925 etc zilikua na Haac mics ambazo mpaka leo ngumu sana kukuta simu ina record vizuri kama Lumia.

Unaweza cheki youtube search "Haac rich recording"

Downside ni kwamba pengine utahitaji kutumia camera kurecord hio audio,
 
Back
Top Bottom