Msaada: Suzuki Grand Vitara (spea, mafuta?)

M24 Headquarters-Kigali

JF-Expert Member
Joined
Jul 9, 2012
Posts
8,199
Reaction score
8,186
Wakuu nimejichanga Sasa natafuta SUV au Double Cabin Ila Kwa bajeti yangu (27m TZS) naona nimeangukia kwenye Suzuki Grand Vitara. Mwenye utaalamu zaidi anijuze.
Crop640x480.jpeg
 
Gari nzuri, ngumu. Itunze tu.
Kama ni ya cc 2000 usitegemee ikimbie sana ila bado ni gari nzuri sana. Ya CC 2400 inakimbia ila inakula mafuta kidogo kuliko ya 2.0. Nimesafiri nayo mara kadhaa barabarani imetulia
Off road (kawaida) pia inapiga vizuri

Reliable sana
 
Gari nzuri...ingawa kwa bajeti hiyo angepata VanGuard au Klugger iliyonyooka sana
 
Gari nzuri, ngumu. Itunze tu.
Kama ni ya cc 2000 usitegemee ikimbie sana ila bado ni gari nzuri sana. Ya CC 2400 inakimbia ila inakula mafuta kidogo kuliko ya 2.0. Nimesafiri nayo mara kadhaa barabarani imetulia
Off road (kawaida) pia inapiga vizuri

Reliable sana
Na mm nataka nijiulize na grand vitara kuanzia 2011 na kuendelea yenye cc2400.

ila nimeona review YouTube kwamba zinatabia ya kuuwa head gasket, hii inanipa shaka kidogo.

Na upande wa Gearbox ipi nzuri kati ya 5 speed manual ama 4 speed automatic hasa kwa safari ndefu?!
 
Mie ninayo ya 2.4cc Mannual 5 Gears, tangu 2020 sijaona tatizo ambalo ni sugu tofauti na thermostat tu. Iliyokuepo olikufa Kila niliweka mpya inapandisha temperature, nikaamua kuitupilia mbali Kwa sasa naitumia bila thermo.
Wakati Ina thermo fuel consumption ilikuwa inanipa 12-13 km/L town trip, sasa hivi inanipa 10-12Km/L Naishi nayo hivyo hivyo.
 
Back
Top Bottom