Msaada tafadhali,Kipato cha binti cha mtoa nduki jamaa..!

Msaada tafadhali,Kipato cha binti cha mtoa nduki jamaa..!

Habari zenu wapendwa,
Kuna mkaka ni mkazi wa dar ila anafanya kazi mgodini huko mwanza huku anakuja kila baada ya miezi miwili,Alikutana na mdada huko mwanza Mdada anafanya kazi huku dar kule alienda kikazi,wakapeana kontakt, na mawasiliano yakaendelea na wakawa wapenzi.

Kwa kipindi cha miezi minne ya mahusiano yao hakuna aliyekua anajua kwa mwenzie,basi wakapanga jamaa atakapokuja dar wakaoneshane makwao,basi jamaa akarudi dar ijumaa iliyopita km kawa wakakutana na jmosi jamaa kampeleka mdada kwake tabata wakashinda huko wakapika na kupakua.

Jpili mdada naye akampeleka jamaa kwake maeneo ya Sinza hapo ndio balaa lilipoanzia kwan muda wote wakiwa pale yule mkaka alikuwa hana raha mwenzie akamuliza kulikon mbona ulikuja vizuri,yy akamuuliza pale anaishi na nani akamwambia mbona nilishakwambia naishi peke yangu.

Akamwomba amwonyeshe slip yake ya mshahara mdada akapigwa butwaa ila akamwonyesha kumbe kaharibu jamaa kanyanyuka na kuondoka akiwa amekasirika mdada hakumwelewa akambembeleza bila mafanikio,usiku wake jamaa akamtumia bint msg kuwa hamtaki tena,kwa sababu anahisi huyo mdada atamtawala maishani kwa vile kwanza ana kipato kikubwa,na ameshajijenga sana kimaisha,hivyo ni rahisi yeye kutokuwa na sauti ndani ya nyumba,au huyo dada anaweza kumwaga wakati wowote na kutoka na wenye uwezo km yy.

Mpaka ninavyoandika huu uzi jamaa hapokei simu na jana kaondoka kurudi mwanza,dada watu kachanganyikia alishampenda jamaa kupita kiasi hata hajui cha kufanya!

Asa mi nauliza hivi nyie wanaume hivi binti kuwa na kipato kikubwa kuliko mwanaume ni kweli ni tatizo kwenye mahusiano?
Na dada afanyaje ili jamaa aelewe na waendelee?

sio wote wenye suruali ni wanaume na huyo ni mmojawapo, mwambie huyo dada atafute mwanaume
 
akyanani ... hapo ni kama SS akaimu nafasi ya EL ... patatosh a kweli?? bibi sijui hata amepotea wapi leo ... naona mjukuu ana spidi ya kutisha sana ... don't do the needful bana!
Hahahahaha! Mbavu zangu wajameni!
 
Nimejikuta nacheka tu hapa maskini kaka wa watu sasa kimemuogopesha mshahara wa shosti???badala amng'ang'nie huyo huyo anamkimbia tena? dah kweli tuko tofauti
 
uzi wako wa leo una utata, hawachelewi kukuambia una mfumo dume ...!
lakini tunachopaswa kufahamu ni kuwa matatizo mengi katika mahusiano, hasa ndoa, husababishwa na:

1: fedha / kipato
2: mahusiano (baina ya wenzi / na mahusiano ya na ndugu / jamaa / marafiki)

hakuna zaidi ya hapo!
Umesomeka mkuu,
Ila hapa tatizo ni kipato kikubwa cha binti kimemkimbiza jamaa,
Inawezekana ikawa sababu au alikuwa na hila zake tu?
 
Hapo bibi chukua tano,huyu jamaa ametudhalilisha WANAUME!

Eiyer, jamaa ana inferiority complex lkn pia tunajua kwa hakika kabisa kwanini alimbia zaidi ya one-sided story?? tunafahamu historia yake kwa maana ya malezi na mahusiano yake?? hivi vitu ni involuntary na vinapelekea kutoa maamuzi kama haya ya kushangaza ... nachelea kumjadili vibaya jamaa sababu nakosa hadithi ya upande wa pili ... vinginevyo nitakuwa simtendei haki kabisa!
 
sio wote wenye suruali ni wanaume na huyo ni mmojawapo, mwambie huyo dada atafute mwanaume
Nimekusoma bibi com,
Hakika maneno yako yanaeleweka vizuri kbs.
Asante kwa ushauri.
 
Umesomeka mkuu,
Ila hapa tatizo ni kipato kikubwa cha binti kimemkimbiza jamaa,
Inawezekana ikawa sababu au alikuwa na hila zake tu?

canty, tatizo una hadithi ya upande mmoja tu, unawezaje kupima ukweli wa jambo la upande mmoja tu uliohadithiwa??
na je, ni asilimia ngapi ya wavulana/wanaume wana mawazo kama hayo??
 
Nimejikuta nacheka tu hapa maskini kaka wa watu sasa kimemuogopesha mshahara wa shosti???badala amng'ang'nie huyo huyo anamkimbia tena? dah kweli tuko tofauti
Nahic ulimkosesha ujasiri kbs,
Hakutaka hata story tena na mapenzi yakaisha gafla lol!
 
canty, tatizo una hadithi ya upande mmoja tu, unawezaje kupima ukweli wa jambo la upande mmoja tu uliohadithiwa??
na je, ni asilimia ngapi ya wavulana/wanaume wana mawazo kama hayo??
Story ya upande wa pili nitaipataje wakati jamaa hapoke simu!
Kuhusu ni asilimia ngapi,kulingana na namna watu walivyochamnia nahisi hili ni tatizo kwa asilimia kubwa ya wanaume wanaogopa kuoa mwanamke aliyemzidi kipato,
Na kuna wale wachache waelewa ambao huyacha mapenzi yajiendeshe yenyewe bila kujali mambo ya vipato,
Ambapo ktk hili inategemea na upendo uliopo kati yao.
 
Tatizo malezi ya binti ambayo atakuwa amelelewa msome Mtambuzi page ya 2 utamwelewa
Mabinti wengi wa kibongo wa sasa wamelelewa katika malezi ambayo siyo hawajalelewa malezi yale ya kumpenda mmeo hata kama anauza mchicha wewe unafanya kazi BoT huyo ndo mmeo mpende kwa moyo wako wote wa sasa hivi ni mapenzi ya kwenye video

tatizo tunalokosea ni kwamba mabinti zetu tunawalea kwa kuwaambia wasome kwa bidii ili waje kuishi independent life wakidepend kwa mwanaume watanyanyaswa, na kwa upande wa vijana wetu tunawapa yale yale malezi yetu ya kizamani kwamba wao ni wanaume na hatutaki kuwaambia ukweli dunia imeshabadilika kitambo watu wanaishi kwa kuheshimiana na kusaidiana kama familia matokeo yake wakija kuwa wakubwa na kuoana kijana anaexpect mke amtii hata kama yeye kijana ni mpumbavu na mke anajua yeye amesoma na anaweza kufanya atakalo na pesa yake matokeo ndio broken families tuzionazo sasa
 
Story ya upande wa pili nitaipataje wakati jamaa hapoke simu!
Kuhusu ni asilimia ngapi,kulingana na namna watu walivyochamnia nahisi hili ni tatizo kwa asilimia kubwa ya wanaume wanaogopa kuoa mwanamke aliyemzidi kipato,
Na kuna wale wachache waelewa ambao huyacha mapenzi yajiendeshe yenyewe bila kujali mambo ya vipato,
Ambapo ktk hili inategemea na upendo uliopo kati yao.

copied with pride ... below

Asante sana bibi.com,
Yani nimependa ulichoandika,
Hakika hujakosea kujiita bibi.com lol!
 
Story ya upande wa pili nitaipataje wakati jamaa hapoke simu!
Kuhusu ni asilimia ngapi,kulingana na namna watu walivyochamnia nahisi hili ni tatizo kwa asilimia kubwa ya wanaume wanaogopa kuoa mwanamke aliyemzidi kipato,
Na kuna wale wachache waelewa ambao huyacha mapenzi yajiendeshe yenyewe bila kujali mambo ya vipato,
Ambapo ktk hili inategemea na upendo uliopo kati yao.

mwanaume anafundishwa kuwa mwanaume from day one anapotoka kwa mama, wakati kizazi cha siku hizi mwanamke anafundishwa kuwa kama mwanaume ili aweze ku survive mfumo dume ... na kama binti anajiamini its obvious ni ngumu sana ku-bend over kuachia ego ya mwanaume iendelee ndani ya nyumba wakati yeye ndiye mwenye kipato kikubwa sana na ndiye anaye run show ya familia nzima, kuanzia bills, ada za watoto, magari, nyumba, na mendeleo yote ... hapa panakalika kweli?? na mara nyingi wanawake wa aina hii huwa wana kiburi, wajuaji sana, majivuno, kujiamini kupita kiasi, wasiojali, etc ... tabia hizo ni sumu kubwa kwa wanaume wengi (kimalezi) ... mume katika mazingira haya, ni lazima tu awe mpole, au gumegume tu! inawezekana huyo jamaa aliona huyo dada ana dalili hizo ndio maana akalianzisha mazima, sababu wanaume wengi wanapenda amani katika nyumba zao na hawapendi wanawake wenye magubu!

on the other side of it, mwanamke mwenye kipato kikubwa akiwa ni mwelewa, mwenye malezi mazuri, na mwenye staha kwa mumewe, hata awe billionea bado hutoona mumewe anakuwa inferior au na wasiwasi na kipato cha mumewe hata siku moja. na mara nyingi wamama hawa huwaachia waume zao wakimbize shoo za familia kiasi kwamba mtu baki wa nje ni ngumu sana kutambua kama mama ndio mwenye kipato kikubwa kuliko baba, mifano hai ipo, na maisha yao ni mazuri tu. wanawake wa namna hii ni lulu kwa wanaume, huwa hawatumii nguvu kupata wenzi wa kuwaoa kabisa, tofauti na aina nyingine tajwa hapo juu!
 
mmh C hapo inawezekana jamaa alitafuta sababu baada ya kupata pato
 
Kwa hiyo jamaa amesha kula mzigo tayari?
Mkuu wewe angle zako huwa zinanifurahisha sana. Yaani wewe first and foremost huwa ni kumega au sio??hehehehe jamaa atakuwa alishabandua mzigo. Kama vipi canta hebu turushie ma-contact hayo na sie tule mzigo tusepe tukatafute wa size yetu tuoe lol
 
Penzi halina uhusiano wowote ule na Pesa.

Jamaa hajampenda huyo mdada.

Mdada achape lapa, atapata anayempenda.:smash:
Kaka mkubwa nina imani kuna mtu ashakuibia password........This is definitely NOT you.
 
Mkuu unazeeka sasa nakumbuka ishu kama hii uliishupalia sana kwenye thread moja, leo naona umebadilika
Ni kweli mkuu Zanta, huyu kaka mkubwa sometimes huwa anacheki upepo hapa jamvini......Si kamuona hommie wake Fidel anasigina kwa hiyo anataka kumzingua tu.
 
Back
Top Bottom