Msaada tafadhali: miaka 2 sasa nateseka na Harufu Mbaya ya Mdomo

Asante kwa ushauri ila sijawahi mkuu
 
Mkuu nimekwenda ila sina hizo tonses
 
Mkuu, niliwahi kuwa na rafiki wa hivo,yaani hakuwahi kumkaribia mwanamke, na darasani alitengwa akawa anakaa kivyake. Lakini tiba ipo,usiogope gharama.
Tafuta hawa watu wanauzaga bidhaa za Aloevera,wana dawa ya meno moja kiboko. Nilimuelekeza jama,katumia tu mbili,sasa hivi ana bonge la mwanamke na watoto,huwezi amini kama alikuwa na hiyo hali.
 
Yapata miaka 6 Sasa.
Utakuwa umepata bakteria ya mdomo ambayo hukupa harufu mbaya dawa yake ni ndogo sana ila sijui kama kwako inapatikana sukutua na karafu fresh kwanza kwa wiki 2 na baada ya hapo kila asubuhi unapiga mswaki na mti dawa kama utapata inasaidia sana baada ya hapo cheki kama unanuka penda chai ya tangawizi nayo huimarisha meno kuwa masafi na kutoa hiyo kitu
 
Sawa mkuu Ila nahisi inatokea ndani kabisa
 
Yani pole sana mpendwa..yani mm ninavyochukia vi harufu harufu na niko very sensitive na smell... sipati picha kama unasema unanuka mdomo kama choo...duuh hebu jaribu nilichokwambia vitunguu swaumu maana vyenyewe ni ant bacteria
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…