Msaada tafadhali: miaka 2 sasa nateseka na Harufu Mbaya ya Mdomo

Msaada tafadhali: miaka 2 sasa nateseka na Harufu Mbaya ya Mdomo

Pole sana.Tatizo lako liko tumboni na wala siyo kinywani.Kama utaendelea kupata dawa za kusafisha kinywa bila kuingia tumboni penye tatizo ni sawa na kazi bure.
Sasa nifanye au nitumie nn mkuu!? Niweze kupona
 
Nenda kariakoo sokoni jengo la sandaland the only one shuka ngazi basement kuna mwarabu ana duka pale hutajuta ana dawa ya meno kutoka Indonesia inakata kabisa.
Nipo mkoani(Arusha )mkuu
 
Nahisi kutengwa na watu nafkiri kujiua

Najiona Sina thaman kabisa hata kuongea na mtu ni shida Sasa nitakua mgeni wa nani mimi jamani[emoji24][emoji24][emoji24]
 
Kila siku nazidi kukonda hata chakula ninachokula sijui kinakwenda Wapi

Nakonda kwa msongo wa mawazo
 
Ndugu zanguni msiwe mnawasimanga watu wananuka mdomo.

Siyo wote wachafu, wengine tuna magonjwa.

hata nikipiga mswaki mara kumi kwa saa, kama vile sijapiga mswaki week mzima


[emoji24][emoji24][emoji24]
 
Mkuu huenda una Tonsil stones kwenye koo...

Vipande vigumu vinavyotokana na mabaki ya chakula...kama una swaki vizuri bila shaka ulishawahi viona vikitoka.. vya njano na vina harufu mbaya na kali...

Nenda hospital ukacheki..kama ndio sababu au lah..
hii inaweza kuwa sababu kama ameshafanya usafi na kutumia mouth wash.... nilishakiwa na dem ananuka mdomo ila ni msafi alikuja kugundua baadae sana kuna vipande vya chakula vinajificha kwenye koo zilipo tonsil aliingiza kidole ndipo akakuta harufu alitibiwa akapona kabisa.
 
hii inaweza kuwa sababu kama ameshafanya usafi na kutumia mouth wash.... nilishakiwa na dem ananuka mdomo ila ni msafi alikuja kugundua baadae sana kuna vipande vya chakula vinajificha kwenye koo zilipo tonsil aliingiza kidole ndipo akakuta harufu alitibiwa akapona kabisa.
Ilimgharimu kiasi Gani kupata tiba ndugu yangu
 
Habari za wakati huu ndugu zangu.

Nimekuja kwenu nikiomba ushauri juu ya kadhia hii inayonikumba mimi mdogo wenu;

Takriban miaka 2 sasa nimekuwa nikitaabika sana na harufu mbaya ya mdomo mithili ya tundu la choo kiasi kwamba nikipishana na mtu anaweza kudhani sijapiga mswaki week nzima.

Nimekua nikijitahidi sana walau kupiga mswaki kila baada ya mlo... Asubuhi, Mchana na Usiku kabla ya kulala. kunywa maji mengi, mboga mboga na matunda kwa wingi pamoja na kutumia mouth-wash.

yote hayo nimefanya lakini hali bado iko palepale.

Mwisho nimekwenda hospitali mara kadhaa na kuonana na Dentist bila mafanikio.

Mahusiano yangu yamevunjika kwa kadhia hiii.

Nahisi kukata tamaa kabisa ukizingatia mara kadhaa nimekua nikitengwa na kunyanyapaliwa na baadhi ya watu kwenye jamii inayonizunguka.

Msaada tafadhali.

Moderator tafadhalini sana nawaombeni msiunganishe uzi wangu huu.
Mkuu linaweza kuwa ni swala la kiroho jaribu kumuomba Mungu au kwenda kansani kwa wachungaji wakuombee
 
Back
Top Bottom