Msaada tafadhali: miaka 2 sasa nateseka na Harufu Mbaya ya Mdomo

Msaada tafadhali: miaka 2 sasa nateseka na Harufu Mbaya ya Mdomo

Yani pole sana mpendwa..yani mm ninavyochukia vi harufu harufu na niko very sensitive na smell... sipati picha kama unasema unanuka mdomo kama choo...duuh hebu jaribu nilichokwambia vitunguu swaumu maana vyenyewe ni ant bacteria
Vitunguu saumu au maji?
 
Utakuwa umepata bakteria ya mdomo ambayo hukupa harufu mbaya dawa yake ni ndogo sana ila sijui kama kwako inapatikana sukutua na karafu fresh kwanza kwa wiki 2 na baada ya hapo kila asubuhi unapiga mswaki na mti dawa kama utapata inasaidia sana baada ya hapo cheki kama unanuka penda chai ya tangawizi nayo huimarisha meno kuwa masafi na kutoa hiyo kitu
Asante kwa ushauri
 
Aiseee hivi vidubwasha ukivibinya huwa vinatoa harufu moja matata sana, unaweza kupata mafua aisee. Vina harufu mbaya mnooo
Vinatokana na nini hasa,kutopiga mswaki au tatizo lingine?
Vilikuwa vikinitokea miaka mingi iliyopita wakati huo nilikuwa napiga mswaki bila dawa (Ukata)
 
Habari za wakati huu ndugu zangu.

Nimekuja kwenu nikiomba ushauri juu ya kadhia hii inayonikumba mimi mdogo wenu;

Takriban miaka 2 sasa nimekuwa nikitaabika sana na harufu mbaya ya mdomo mithili ya tundu la choo kiasi kwamba nikipishana na mtu anaweza kudhani sijapiga mswaki week nzima.

Nimekua nikijitahidi sana walau kupiga mswaki kila baada ya mlo... Asubuhi, Mchana na Usiku kabla ya kulala. kunywa maji mengi, mboga mboga na matunda kwa wingi pamoja na kutumia mouth-wash.

yote hayo nimefanya lakini hali bado iko palepale.

Mwisho nimekwenda hospitali mara kadhaa na kuonana na Dentist bila mafanikio.

Mahusiano yangu yamevunjika kwa kadhia hiii.

Nahisi kukata tamaa kabisa ukizingatia mara kadhaa nimekua nikitengwa na kunyanyapaliwa na baadhi ya watu kwenye jamii inayonizunguka.

Msaada tafadhali.

Moderator tafadhalini sana nawaombeni msiunganishe uzi wangu huu.
Nenda Kwa dentist na uanze na x-ray, waangalie kama una meno mabovu au yaliyotoboka, kama yapo yang'oe yote or piga root canal, ukimaliza zingatia usafi wa mdomo wako, piga mswaki walau mara mbili kabla na baada ya kulala, na ukiwa unapiga mswaki safisha na ulimi na usisahau flossing(kiswahili sijui inaitwaje), kama hujapona harufu inawezekana itakuwa inatokea tumboni au kooni, inawezekana una bacteria wanaosababisha hiyo harufu,inabidi umwone daktari akuangalie
 
Nenda kariakoo sokoni jengo la sandaland the only one shuka ngazi basement kuna mwarabu ana duka pale hutajuta ana dawa ya meno kutoka Indonesia inakata kabisa.
 
Habari za wakati huu ndugu zangu.

Nimekuja kwenu nikiomba ushauri juu ya kadhia hii inayonikumba mimi mdogo wenu;

Takriban miaka 2 sasa nimekuwa nikitaabika sana na harufu mbaya ya mdomo mithili ya tundu la choo kiasi kwamba nikipishana na mtu anaweza kudhani sijapiga mswaki week nzima.

Nimekua nikijitahidi sana walau kupiga mswaki kila baada ya mlo... Asubuhi, Mchana na Usiku kabla ya kulala. kunywa maji mengi, mboga mboga na matunda kwa wingi pamoja na kutumia mouth-wash.

yote hayo nimefanya lakini hali bado iko palepale.

Mwisho nimekwenda hospitali mara kadhaa na kuonana na Dentist bila mafanikio.

Mahusiano yangu yamevunjika kwa kadhia hiii.

Nahisi kukata tamaa kabisa ukizingatia mara kadhaa nimekua nikitengwa na kunyanyapaliwa na baadhi ya watu kwenye jamii inayonizunguka.

Msaada tafadhali.

Moderator tafadhalini sana nawaombeni msiunganishe uzi wangu huu.
Nilikuwa na tatizo hili kwa miaka kumi ila nimetumia dawa kwa mtaalamu wa tiba asilia na nimeona kabisa. Yupo Nachingwea njoo inbox nikuunganishe nae.
 
Back
Top Bottom