Msaada tafadhali nakosa hamu ya kula

Msaada tafadhali nakosa hamu ya kula

ichumu lya

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2016
Posts
2,651
Reaction score
2,790
IMG_20171004_084545.jpg

Ninashida ya kukosa hamu ya kula kwa muda mrefu,njaa ninayo lakini sitaki chakula chochote nikila kinakuwa kichungu na ninatafuna kwa muda mrefu kabla ya kumeza,ninalazimika kutumia pilipili nyingi ili kukabiliana na uchungu,nifanyeje wakuu?
 
Tumia dawa asili na recomend
Utumie cannabis au bangi kama majani ya chai unachemsha gramme 50 Kwa robo litre tren ichemke dk 3 kisha chuja unywe dk 30 kabla ya meal itakusaidia mkuu
 
Kuna vidonge vya kuongeza hamu ya kula jaribu af pia jaribu kula kitu unachokipenda saana na visiwe vya michuzi michuzi
 
tafta multi vitamin vidonge vitaleta njaa na kupata hamu ya kula
 
Ilinitokeo iyo kipindi Niko chuo ...nilikua sina hamu ya chakula cha mighahawa....ila chanyumbani nilikua nakula fresh
 
Ilinitokeo iyo kipindi Niko chuo ...nilikua sina hamu ya chakula cha mighahawa....ila chanyumbani nilikua nakula fresh
Mimi mpaka leo ninayo! Nikiwa mjini sina hamu ya kula yaani huwa najilazimisha tu ila nikienda home kijijini nakula vizuri kabisa tena chakula kingi sana! Nikirudi tu mjini hamu inapungua sana na nikila nakula chakula kidogo sana!

Huwa sijui tatizo ni nini! Nilishawahi kwenda kwa wataalamu kuulizia wakaniuliza umeoa? Nikasema hapana wakaniambia basi ukioa utaongeza ulaji pengine aina ya chakula unachokula migahawani kinakuwa hakina maandalizi mazuri au hata unavyojipikia mwenyewe unakuwa na aina moja ya chakula!
 
Hiyo pia ni dalili ya msongo wa mawazo jaribu kutafuta namna ya kupunguza mawazo hasa kwa yale mambo usiyokuwa na uwezo nayo,take it easy usilazimishe usiyoyaweza hali yenyewe ngumu na hakuna dalili za hali hii kuimarika
 
Back
Top Bottom