Msaada tafadhali; Namtafuta mtu aliyeomba ushauri kuhusu pikipiki

Habari zenu waungwana,
Kuna biashara nilikuwa nafanya, yakuchukua mahindi hadi tone kumi kutoka mikoani, kuleta DSM. Sasa soko limeyumba kidogo hapa DSM, nikaamua kuanza kununulia hapahapa.

Ishu inakuja pale unapompa mtu mzigo , halafu kuikusanya ile pesa inachukua hadi wiki, ukiangalia faida yenyewe sio ya kuridhisha kabisa .

Kwa mfano unaweza mpelekea mtu tone 4, faida inakuwa kama 80,000 , inakaa siku tatu hadi wiki na zaidi ni hasara kwakweli.

Kuna mdau alileta uzi juzi hapa aliomba ushauri , alikuwa anataka kununua pikipiki aina ya boxer, watu wakamshauri vizuri sana, kuna mdau mmoja akamshauri kama kweli anataka kufanya biashara amtafute PM, faida sikumbuki vizuri kama sio kwa wiki ama kwa mwezi anaingiza laki nane.

Kama kuna mtu anayo hiyo link naiomba aniwekee hapa, ili nimtafute huyo jamaa.

Nawasilisha
Nataka nikanunue bodaboda mjini, nizingatie yapi nisije kuuziwa mbuzi kwenye gunia?

Umeomba link naona watu wanakuyeyusha kwa kumuita mtu kwa jina. [emoji12] link hiyo[emoji115] . Utuletee feedback maana mwenyewe sijui biashara gani inalipa now. Siwezi ingia kichwa kichwa.

-callmeGhost
 
Habari zenu waungwana,
Kuna biashara nilikuwa nafanya, yakuchukua mahindi hadi tone kumi kutoka mikoani, kuleta DSM. Sasa soko limeyumba kidogo hapa DSM, nikaamua kuanza kununulia hapahapa.

Ishu inakuja pale unapompa mtu mzigo , halafu kuikusanya ile pesa inachukua hadi wiki, ukiangalia faida yenyewe sio ya kuridhisha kabisa .

Kwa mfano unaweza mpelekea mtu tone 4, faida inakuwa kama 80,000 , inakaa siku tatu hadi wiki na zaidi ni hasara kwakweli.

Kuna mdau alileta uzi juzi hapa aliomba ushauri , alikuwa anataka kununua pikipiki aina ya boxer, watu wakamshauri vizuri sana, kuna mdau mmoja akamshauri kama kweli anataka kufanya biashara amtafute PM, faida sikumbuki vizuri kama sio kwa wiki ama kwa mwezi anaingiza laki nane.

Kama kuna mtu anayo hiyo link naiomba aniwekee hapa, ili nimtafute huyo jamaa.

Nawasilisha
Tafuta bajaji boss komaa nayo mjini
Nunua mikononi kwa watu zipo nyingi tu
 
Huo ni udhushi faida laki nane mm ni Bajaj nimepaki nyumbani tangu march hawa madereva wanyoa viduku ni shida
 
Mkuu, sitaki kabisa kusikia biashara ya pkpk, biashara hii kama utaifanya mwenyewe, namaanisha kama utaendesha mwenyewe inalipa vizuri, ila pkpk ya kumpa mtu mkuu, uuuwi, ninazo mbili nimeziweka stoo

Sent using Jamii Forums mobile app
Usipo muelewa huyu mdau usije rudi hapa unalialia,mm binafisi bodaboda ilinisha pamoja na kuwa nilikuwa na duka la spear!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wadau pikipiki zinalipa inategemea wewe unafanya kwa mfumo upi.
1. Mfumo wa kwanza ni wa marejesho ya kawaida ambayo huna mkataba na dereva na huwa wanaleta kwa siku wastani was tsh 7,000/= Huu sio mfumo mzuri kwasababu service na matengenezo ni juu yako mmiliki na dereva asiye mwangalifu ataiburuza piki piki mpaka iwe skrepa na utajikuta hata faida hujapata.
2. Mfumo wa pili ambao wengi tunautumia kwasasa ni wa mkataba ambao huwa inakuwa kwa miezi kumi kwa marejesho ya tsh 10,000/= kwa siku na akishamaliza mkataba pikipiki inakuwa ya kwake. Huu ni mfumo mzuri kwa kuwa dereva anakuwa makini maana mwisho wa siku hataki amiliki chombo kibovu na pia service na matengenezo ni juu ya dereva.

Kwa kifupi ni hivyo, ukipiga hesabu wastani kwa miezi kumi unaingiza kama milioni tatu na kidogo.

Hii biashara ngumu sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom